Kukudume2013
JF-Expert Member
- Jan 8, 2013
- 1,659
- 733
Kama mwezi mmoja nyuma nilinunua kiwanja maeneo ya Dodoma kupitia rafiki yangu, bei ya hicho kiwanja ni 8 million ni viwanja vya CDA , ambapo unainunua vocha ya kiwanja kutoka kwa mmiliki, baada ya kufanya ziara ya kwenda kukikagua nijijuta kwanini nilinunua, maaana kwenye ramani kiwanja kinaonesha ni square meters 300 na kipo ndani huko mbali sana na kile kiwanja alichooneshwa rafiki yangu sicho chenyewe ambacho kilikuwa kizuri tu kina square m.700.
Nimeongea nao jamaa wauzaji warudishe hela zangu wanasema hawana pesa na kiwanja mimi sikitaki hata kukiona maana ni kidogo na kiko mbali sana, maana baada ya pita pita na kuuliza maeneo mengine nimegundua kwa pesa ile naweza. Kupata hata sq m 1000, sasa hapa nawaza sijui niwapigie dua hawa jamaa au niwapeleke MAHAKAMANI kudai haki yangu? Au nifanye nini?
Naomba ushauri sijui nifanye nini kwa sasa maana pesa yangu inauma sana.