Nadhani itafikia mahali hata lift kwenye majengo Marefu zitaanza kulipiwa na kama huna basi utazunguka kwa kutumia ngazi.
Hapa kuna Mambo mawili:
(1) Tatizo la mashirika yetu ya umma na hata viwanda ni kutoa huduma au bidhaa zake kwa bei kubwa kwa manufaa ya wachache.
Wananchi wengi wanaumia ili wachache wajilipe mishahara minono hata kwenye huduma au bidhaa muhimu na za msingi.
Hua najiuliza ni kwa nini kila kitu kinachotoka nje ni rahisi kuliko vya ndani. Inamaana huko hawataki faida. Mfano ukiagiza gari huko Japani ni bei rahisi lakini likishakanyaga Tanzania basi kodi juu utafikiri tuna viwanda vya magari tunavyovilinda.
Hii nchi thamani ya fedha ni kubwa kuliko utu wa mwanadam. Na ukishakua na serikali inayothaminisha pesa kwa kiwango cha juu kuliko utu wa mwanadam basi tegemea kuwa na watu wenye roho mbaya, wanaoombeana mabaya, wanaofurahia kuona wenzao wanapokutwa na mabaya, wanaoviziana kuangamizana, kuibiana , kuuana kwa malengo ya kupata pesa, ushirikina, madawa ya kulevia, uzinzi kwa tamaa ya wanawake kupata fedha , kwenye dini fedha, kuuziana bidhaa bandia, bidhaa zilizokwisha muda wake kuuzwa tena ili kusaka hela, madalali kila kona kuanzia serikalini, riba kubwa kwenye mabenki na kila aina ya usanii na utapeli.
(2) Wanyonge wamewekewa fumbo ili wajiongeze wenyewe.
Kama unaona kupita darajani ni gharama basi zunguka au endelea kutumia kivuko kama au upige mbizi.
Kuna watu wanye pesa za kulipa hata laki 50,000 kwenye daraja kwa siku. Nadhani hao ndio waliojengewa hilo daraja na wapo tayari kulipa kwani kwao tatizo ni foleni ya kivuko na sio pesa.
Daraja limejengwa kwa supper market. Kama ukiona huwezi kwenda mlimani city basi nenda kariakoo. Watu wamewekeza pesa zao na wamelenga watu wenye kipato cha juu kwa raha zao.
Nini kifanyike kwenye daraja la kigamboni!!!:
(1) Huduma za kivuko zilizozoeleka ziendelee kama kawaida ili pia kupunguza foleni.
(2) Bei ya kulipia daladala ipungue iwe ni sh. 1000/- kwa kila ruti au iwe 5000/- kwa siku nzima. Hii ni kuwasaidia wanyonge kwani daladala zinatoa huduma ndio maana zinapangiwa bei ya nauli na hata kuombwa kubeba walimu bure na wanafunzi nusu nauli. Hawa wanaumizwa sana na suala la mapato kuanzia sumatra n.k.
Magari madogo na ibaki kama ilivyo .
Pikipiki ipande na kufikia 1000/.
Hii itasaidia kulifanya daraja ama kivuko kuwa ni suala kuchagua. Ukiona daraja ni ghali basi panda kivuko.
ANGALIZO:-
Kama Serikali ya Magufuli ni ya watanzania wanyonge ,yaani wakulima na wafanyakazi basi huduma ya daraja iwe ni sh. Mia tano tu,500/- kwa magari yasiyozidi tani tatu na 1000/- kwa magari chini ya tani 7.
Kuanzia tani 7 kwenda juu yalipe 5000/-
Kuazia tani 7 kwenda juu na yaliyopakia mizigo yalipe sh. 10,000/-.
Baskeli ziwe bure ili kuhamasisha watu matumizi ya baskeli kama chombo cha usafiri cha kubana matumizi.