kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,940
- 7,849
Kutokana na kushamiri mfumo wa rushwa nchini mamlaka zinazohusika na usimamizi wa vituo vya daladala jijini dar-es-salaam zimeshindwa kabisa kuweka nidhamu kwenye vituo vikuu vya daladala ambapo sasa vimegeuka kuwa masoko.
Kwa mfano kwenye kituo cha Mwenge hivi sasa mabasi yamehama kituoni na yanasimama nje baada ya kukabiliwa na msongamano mkubwa wa wafanyabiashara.
Sakafu yote ya kituo zinatandazwa bidhaa utadhani mabasi na abiria ndio wageni hapo kituoni.
Kituo cha Mwenge kilipozinduliwa baada ya matengenezo kilifunguliwa kwa mbwembwe huku wahusika na usimamizi wakitapa kuweka nidhamu. Hivi sasa wamebobea kwa kuchukua kitu kidogo kutoka kwa wafanya biashara wadogo na kufumbia macho shughuli zao hadi kituo kimegeuka soko.
Hapo mwenge hakika sasa ni soko tena kubwa karibu litakua la kimataifa. Mabasi sasa yanasimama nje ya kituo huku wananchi wakiingia hapo kituoni kwa manunuzi ya bidhaa mbalimbali.
Hakika hii ndio picha halisi ya nchi yetu, hakuna kinachoenda kwa mpango ila rushwa ndio inatawala. Ngojea tuone hiyo DART ikianza kama hatukuona madudu tu kwa ajili ya mfumo rushwa.