Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,265
- 21,443
Wana JF, nadhani wengi wetu tumetembelea kituo cha polisi, labda kwa shida fulan au hata kwa kuwekwa ndani. Hivi mmeona jambo moja ambalo mimi nimeona kwamba vituo vingi sana vya Polisi hapa nchini vina harufu mbaya sana? Vinanuka! Huwa nashindwa kuelewa hata hao Polisi wanaofanya kazi kwenye vituo hivi wanawezaje kuvumilia harufu ile muda wote. Au wameizoea? Na je harufu hiyo haiwaathiri kichwani kweli?
Wakati fulani nilidhani kwamba harufu hiyo ni jambo la kawaida kwa nchi zote, hadi nilipotembelea vituo kadhaa vya nchi nyingine, hata za hapa hapa Afrika. Nilishangaa sana kukuta hali ni tofauti sana kwenye baadhi ya nchi, kwamba vituo vyao unaweza hata udhani sio kituo cha Polisi kwa usafi na kutokuwa na harufu mbaya.
Ina maana suala ni kwamba vituo vyetu vya Polisi kunuka ni kwa sababu Polisi wanajiendekeza tu. Hakuna sababu ya vituo hivi kuwa na harufu mbaya kiasi hiki.
Natoa wito kwa Polisi kujiangalia kwa hili, wasimsubiri Magufuli. Waanze kuchukua hatua kwamba watu tusitembelee vituo vya polisi huku tumeshika pua na kukimbia kuoga kwa sababu tu tulienda kituo cha Polisi kwa shida fulani. Kwa wengine harufu hiyo mbaya inafanya hata tusite kwenda Polisi kwa shida yeyote. Kwanza nina wasiwasi sana na athali wanazopata Polisi kutokana na kuvuta harufu hiyo mbaya kila siku. Usikute ule ukatili unaofanywa na baadhi ya Polisi kwa raia ni kwa ajili ya kuvuta harufu hii mbaya!