Vituko vya Nahodha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vituko vya Nahodha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BASIASI, Aug 14, 2011.

 1. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,102
  Likes Received: 341
  Trophy Points: 180
  MUUWAJI AMETULIA TABATA-ZOMBE UNALETA SIASA NANI ALIMUUA HUU NIUHUNISIDHAN KAMA TUTAWEZA KUVUMILIA
  KUWA NA MAWAZIRI WAHUNI KWENYE SERIKALI HIII, KIKWETE WAKATI UNACHAGUA LIST ULIMSHIRIKISHA MIRAJI AMA?

  SIDHAN KAMA ULIFIKIIRIA KUWA NA WASAANII KAMA HUU ATI LEO NDIO ANAULIZA AALIEWAUA WAHANGA WA MAHENGE, NENDA MCHUKUE
  ZOMBE AKAKUONYESHE HADI SEHEMU WALIPOPIGWA NA AKIKATAA BANENI HIZO PU@# MNAZOBANA WATOTO WA WENZENU KAMA
  AJASEMA UKWELI

  Nahodha: Polisi wasakeni walioua wachimba madini wa Mahenge


  Na Hellen Mwango  13th August 2011

  Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha (kushoto), akitoa maelekezo kwa Kamishna wa Polisi anayeshughulikia masuala ya Fedha na Utawala, Clodwig Mtweve, kufuatilia maafisa 2 wa polisi waliotoroka kwenye kesi iliyokuwa ikimkabili Abdallah Zombe na wenzake.

  Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kuwatafuta Koplo Saad na Sajenti Frank, kama Mahakama Kuu Tanzania ilivyoagiza watafutwe waliofanya mauaji ya wafanyabiashara wa madini watatu wa Mahenge na dereva mmoja wa teksi.

  Kadhalika, Waziri Nahodha ameliagiza jeshi hilo kulishughulikia suala kama askari polisi hao bado wanalipwa mishahara na posho.

  Alitoa maagizo hayo baada ya kuhojiwa na NIPASHE kwamba suala la kukamatwa kwa askari polisi hao waliotajwa mahakamani kufanya mauaji hayo limefikia wapi.

  Wafanyabiashara hao waliouawa ni Ephrahim Chigumbi, Sabinus Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva wa tekesi Juma Ndugu.

  Mahakama iliwaachia huru askari polisi 12 baada ya ushahidi kushindwa kuthibitisha makosa dhidi yao na sasa rufaa yao inasubiri kusikilizwa.

  Pia alihojiwa suala la tuhuma zilizotolewa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Dar es Salaam, (wakati huo), Kamishna Msaidizi Abdallah Zombe, kwamba Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema ni kinara wa mtandao wa majambazi wa wizi wa magari nchini.

  Alisema alisikia tuhuma hizo dhidi ya Lema ambapo aliliagiza jeshi hilo kupata maelezo ya kina kutoka kwa Zombe ili liweze kufanyiwa kazi.

  "Naagiza mlishughulikie hilo suala la hawa askari wawili na kuhusu mishahara yao kama bado wanalipwa pia, nataka kupata taarifa yake haraka iwezekanavyo…mimi sikumbuki vizuri kama mahakama ililiagiza jeshi langu kuwatafuta walioua na kama iliagiza mfanye hivyo" alisema.

  Aliongeza: "Kuhusu suala la Lema, Zombe alikuwa ofisa wetu mwandamizi ni kitu gani kilimzuia kutoa taarifa hii wakati akiwa madarakani na leo ni nini kimemsukuma kusema haya… naagiza kwa kuwa ni mwenzetu, tukae naye ili atoe taarifa za kina na tuzifanyie kazi."

  Waziri Nahodha alikuwa akizungumzia mafanikio ya miaka 50 ya Jeshi la Polisi tangu kupata Uhuru.

  Alisema ili kuhakikisha Jeshi la Polisi, Magereza na Idara ya Uhamiaji vinaendelea kufanya kazi kwa mujibu wa maadili ya kazi, anahitaji ushirikiano na jamii.

  Alisema ofisi yake iko wazi kupokea taarifa za kuaminika iwapo kuna ofisa wake
  yeyote anajihusisha na rushwa atamfuta kazi mara moja.
  Alisema akipokea taarifa kwa watu watatu tofauti kuhusu ofisa wake kujihusisha na rushwa, hatasita kumuachisha kazi mara moja.

  Akizungumzia miaka 50 ya Uhuru, alisema Jeshi la Polisi limefanya kazi ya kuimarisha usalama wa raia na mali zao unaimarishwa ikiwemo programu ya miaka 10 ya maboresho ya jeshi kwa kulijengea weledi, mazingira bora ya kazi na kuendeleza dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi.

  Hata hivyo, alisema bado kuna malalamiko katika sehemu kuu mbili, ile ya upelelezi wa makosa ya jinai ambayo inachukua muda mrefu jambo linaloathiri uendeshaji wa kesi mahakamani.

  Kasoro nyingine aliitaja kuwa ni baadhi ya askari wa jeshi hilo kushindwa kusimamia kikamilifu majukumu yao.

  "Nimepokea malalamiko mengi kuhusu kuwepo kwa upendeleo katika kupandisha vyeo, jambo hili lisiposimamiwa vizuri linaweza kuwakatisha tamaa askari wanaostahili lakini hawapandishwi vyeo kutokana na utendaji mzuri wa kazi," alisema.

  Kwa upande wa Jeshi la Magereza alisema lina jukumu la kuwahifadhi na kuwahudumia wafungwa na mahabusu ambapo ili kuwajengea wafungwa uwezo linawapatia mafunzo ya ushonaji wa nguo, utengenezaji sabuni, na uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na mkonge.  TATIZO ULE MGAO AKULA ZOMBE PEKEE NDIO MAANA WAMEKAA KIMYA NI ZAIDI YA ZOMBE KAMAA UNATAAKA KUFWATILIA
   
 2. p

  politiki JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Kuna watu kama iddi simba na wenzake wanakula rushwa live, umsikii hata siku nahodha akitoa tamko lakini unataka
  lichunguzwe swala la lema huku chanzo cha habari hiyo ni mtu ambaye ameshapoteza credibility mbele ya jamii kwa uhalifu aliotenda siku za nyuma.
   
 3. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Watanzania wenzangu,nawaomba mnikubalie kwamba nchi yetu haina serikali (mawaziri na rais),haina bunge na haina mahakama.Mtu kama zombe kwa nchi zilizo makini asingeachwa huru na huyu m*zimu nahodha hana hadhi ya kuwa waziri kwa nchi ambazo zimejipanga kimaendeleo,suala la askari waliotoroka kuendelea kulipo mshahara kuhojiwa sasa hv baada ya miaka sita ya mauaji ni kithibitisho cha wazi kuwa serikali inafikiria kwa kutumia MAKALIO
   
 4. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2011
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,800
  Likes Received: 2,571
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />

  Kuhusu Simba nahisi jamaa anachukua notes sooner or later ataibuka armed with plenty of notes and no evidence to give. Bana hii ndio Tanzania yetu.
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Aug 14, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Jamani hawa jamaa vipi? mpaka chadema ipige kelele ndiyo wanashituka! kesi imeisha karibia mwaka wa pili cha ajabu leo ndiyo waziri anatoa tamko la kukamatwa wahalifu kweli hii nchi ya mazonge.
  AKILI YA KUAZIMA CHANGANYA NA ZA KWAKO
   
 6. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #6
  Aug 14, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hivi bado anaendelea kuishi New Africa hotel?..maana alikataa nyumba aliyopewa mwanzoni akidai haina hadhi ya 'waziri kiongozi'.
  Huyu anatia mashaka maana issue sensitive kama mauaji ya raia anaoneka hana habari nazo kabisaa..
  Ama kweli bongo inachosha ukiifikiria
   
 7. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,357
  Trophy Points: 280
  huyu alipewa cheo ili kumpoza baada ya zanzibar kubadilisha katiba na kufuta cheo cha waziri kiongozi,.alipewa ubunge wa kuteuliwa,..m.k.were alitaka kumpa na meghji uwaziri lakini watu wakachonga akamtosa but iam sure atampa uwaziri uko mbele ya safari..wazanzibar wengi hawana asili ya kupenda makuu lakini huyu nahodha wa nchi kavu ananishangaza kukataa nyumba,..nina shaka na swaumu yake kama amefunga..pepo ngumu sheikh
   
 8. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #8
  Aug 14, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  nchii ndiyo maana hatuendeleii, loooh!
   
 9. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #9
  Aug 14, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  mambo mengine Bana !!! acha tu yaani ..........aaah.........!!
   
 10. c

  change we need Member

  #10
  Aug 15, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 81
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mauaji yanafanyika miaka kama 6 iliyopita, watu wanaachiwa katika mazingira ya utatanishi hata baada ya ripoti ya madaktari kuthibitisha kuwa walipingwa risasi kutokea nyuma tena kwa pamoja! bado ushahidi haukutosha. Leo unaagiza maaskari kama wanalipwa mshahara au na watafutwe wakamatwe! nchi inaongozwa na watu wasio makini bado unaona tuna serikali hapo? kiini macho na ni aibu hata kujivunia miaka 50 ya jeshi la polisi ambalo limeshindwa kukamata wezi na likiwa viongozi wake waandamizi wakiwa vinara wa uhalifu akiwemo Zombe.
   
 11. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #11
  Aug 15, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Maswali ninayojiuliza ni kwamba, kesi zote zinazohusu wakubwa ambazo ofisi ya DCI imeziendesha, ni kesi ngapi imeshinda? Ukiacha kesi ya Liumba, ni wangapi wamefungwa gerezani? Competent ya wanasheria wake ikoje?
  Majibu ya haya maswali yatatusaidia kutoa +ve comment.
   
 12. S

  SOLOGWIGABA Member

  #12
  Aug 15, 2011
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Polisi wenyewe hawana mood ya kazi kutokana serikali yao kutowajali.Hao wauaji nani atahangaika nao?
   
 13. w

  wasp JF-Expert Member

  #13
  Aug 15, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni lini Mheshimiwa Naodha atalitaka Jeshi la Polisi kufuatilia wezi wa Kagoda, meremeta, etc?
   
 14. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #14
  Aug 15, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,966
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Hivi alishahama kule hotelini?
   
 15. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #15
  Aug 15, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Pelekeni ushahidi kwa DPP ili kufunguliwe kasi sio kulalama
   
 16. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #16
  Aug 15, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Ushahidi upi wakati anao? Kila mtu ana mtazamo wake katika masuala mazito na sidhani kama
  wananchi wanapoamua kusema basi watakuwa wanalalamika. Mbona mkuu wa nchi analalamika
  kila mara lakini hatusikii mkimsema? Nchi hii tunapenda kuishi kinafiki, kutenda tusichosema na
  kusema tusichotenda!
   
Loading...