Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Mshana ukiweza tuletee na vituko vya Manzese, ikiwezekana vya Tandale kwa tumbo na mtaa mwingine maarufu😂
 
Mshana ukiweza tuletee na vituko vya Manzese, ikiwezekana vya Tandale kwa tumbo na mtaa mwingine maarufu[emoji23]
Hii iko kwenye vituko vya dar


Jiji la Dar na vitongoji vyake: Mikasa, vituko, vitimbwi na matukio
 
Na mimi niongezee;
kama ni mgeni hasa nyinyi wa mikoani na vichench vyenu! usijidai ww ni papaa na mpenda kunjunja! ukiwa kwenye tule monde mwananyamala, unaweza kushobokewa na demu kisuu! zaidi ya beyonce! ukajiona umepata kumbe watu wako kazini!
Duuh una maana gani watu wako kazini?
 
Nimekumbuka enzi zile miaka ile ya Timu ya Lucky Rangers. Kuna ligi ilikuwa inafanyika pale Shule ya Msingi Mwananyamala B, ilikuwa mshike mshike.

Siku hizi Mwananyamala hakuna mateja sana na ukabaji, enzi zile ukijisahau, roba ya mbao. Wababe wengi wamefariki au wamepoteza uwezo.

Juzi juzi nimepita kituo cha basi cha Mwananyamala A, nimemkuta mtu namjua nikiwa mtoto, hana miguu yote, yupo kwenye baiskeli ya wasiojiweza, anaomba omba. Namjua huyo miaka ile, alikuwa mbabe kweli kweli, mtu wa kazi, Konda. Niliumia sana.

Nikakumbuka enzi za Villa Motel pale Ujiji, palikuwa pamoto sana.

Nikakumbuka na enzi za Mchiriku na Mnanfa.

Mwabanyamala imepoa siku hizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…