Wanajamvi,
Nimeshangazwa sana na watu hawa. Wiki 7 (karibu miezi 2) zilizopita lilipita gari la matangazo njia yote kutoka Mombasa hadi Moshi Bar likitaarifu kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami varabara ya Mombasa - Moshi Bar. Tangazo lilikuwa. Hivi " Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh Jerry Slaa anawatangazia kuanza kwa ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Mombasa - Moshi Bar. Anawaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa wakandarasi ".
Siku inayofuata tukaona grader likifanya kazi ya kusawazisha barabara iliyokuwa imeharibika vibaya. Baada ya siku mbili tukamwona Mbunge wa Ukonga Mh. Eugene Mwaiposa akitinga na shangingi lake ambapo alisimama maeneo ya Kota na kufanya mazungumzo (mkutano?) na kundi la wananchi waliokuwa maeneo hayo. Yeye alisema kazi ya ku-grade barabara ilikuwa sio sehemu ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami bali ilikuwa ni matengenezo ya Dharura toka mfuko wa maafa. Akijibu swali toka kwa mpigakura wake kuhusu kutolewa kwa fidia ya Nyumba zilizotakiwa kuvunjwa kupisha upanuzi wa barabara hiyo, alikwenda mbali kwa kusema hakuna dalili za kulipwa fidia hivi karibuni kwa kuwa hakuna fedha yoyote iliyotengwa na mamlaka husika kwa kazi hiyo. Aliwataka wote walioguswa na zoezi hilo kuendeleza maeneo hayo kama kawaida na kusema iwapo serikali ikitaka kufanya zoezi hilo basi litaanza upya. Siku inayofuata tuliona vifusi vikimwagwa ktk baadhi ya sehemu za barabara hiyo.
Baada ya zoezi hilo la vifusi hakuna kilichoendelea hadi leo. Ukipita barabara sehemu hiyo ni marundo ya vifusi barabarani ambayo sasa imekuwa KERO kubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo. Magari na pikipiki vinasubiriana kupita maeneo hayo na kusababisha misongamano isiyokuwa na kichwa wala miguu. Kwa kweli wakazi wa maeneo haya meshindwa kuwaelewa watendaji wanaosimamia zoezi hili. NS inashindwa kuingia akilini kwa nini wamefanya hivi. Hivi lengo ilikuwa ni nini? Kama kuna tatizo ni lipi hilo? Kwa nini wansnchi wasishirikishwe angalau kusambaza vifusi hivyo Kama bajeti imebana?
Nina maswali kadhaa kwa waheshimiwa hawa yaani Jerry Slaa na Eugene Mwaiposa:
1. Barabara inatengenezwa na Manispaa ya Ilala au na Jerry Slaa? Kama ni Manispaa kwa nini atajwe yeye utafikiri fedha inatoka mfukoni mwake?
2. Pamoja na wasiwasi wa kunyang'anywa jimbo na Mh Jerry Slaa, Mh Mwaiposa amepata wapi uhalali wa kuwaruhusu wananchi kuendeleza maeneo yaliyowekwa X?
3. Hivi nini ilikuwa lengo la kazi hiyo ya barabara? Kutengeneza barabara au Kuwatamanisha na kuwaletea usumbufu wa aina mpya?
4. Kwa yeyote anayehusika na kuleta kifusi ktk barabara hii, kwa nini kifusi hakijasambazwa hadi leo?