Naibu Katibu mkuu wa CCM Tanzania bara, Mwigulu Nchemba amekuja na staili mpya ya kupambana na CHADEMA nchini baada ya mbinu zake kadhaa za awali kuelekea kugonga mwamba.
Siku ya juzi mkoani Singida, katika wilaya ya Iramba, Mwigulu Nchemba alifanya kituko kipya baada ya kuja na staili mpya ya kufanya siasa za kupambana na CHADEMA.
Timu ya Simba Fc kutoka Dar ilifika kucheza mechi ya kirafiki wilayani Iramba kwa mwaliko wa Mwigulu Nchemba na wakati huo huo zaidi ya Askari 100 kumwaga kwenye mkutano wa CHADEMA kwa 'amri' ya Mwigulu huku wakiwa na silaha nzito nzito kwa lengo la kujenga mazingira ya hofu kwa watu ili washindwe kufika na kumsikiliza Dr.Slaa ambaye alikuwa akihutubia mkutano wa CHADEMA unaohusu rasimu ya katiba mpya.
Pamoja na kuwepo kwa askari wengi kwenye mkutano huo wa CHADEMA, inasemekana bado kulikuwa na wananchi wengi waliofika kuhudhuria mkutano huo.
Pia inasemekana Mwigulu huenda akaendelea na staili hii mpya kama njia mbadala ya kupunguza nguvu ya Ushawishi wa CHADEMA ambao kufanya harakati zao zaidi kwa njia ya mikutano ya hadhara.