Ngaliba Dume
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,710
- 3,675
Wakuu kweli Uswahili kuna vitukooo...,Yaani ni bandika bandua.
Leo nilikuwa kwenye jopo la kusuruhisha mgogoro wa jamaa kutaka kupigwa mapanga kwa kudhaniwa tu ni mpiga chabo.
Huyu jamaa ni jirani hapa mitaa yetu,yeye amepanga nyumba jirani na ana shughuli zake huko Down Town.Sasa muda wake wa kurudi ni around saa mbili hadi tatu usiku akichelewa basi saa nne usiku.Na muda wa kuondoka kwenda katika mihangaiko yake ni mida ya saa moja hadi mbili asubuhi.
Sasa ili ufike mahali anapokaa jamaa kuna kiuchochoro katikati ya nyumba mbili.Hiyo ndio huwa jia ya jamaa...Upande mmoja wa kichochoro kuna dirisha la chumba cha wakazi wa hiyo nyumba.
Sasa inaonekana vijana wa mtaani wamekuwa wanawapiga sana chabo watu ktk hiyo nyumba.
Sasa yaliyomkuta huyu jamaa ni kuwa yeye kila alipokuwa anapita pale uchochoroni usiku,alikuwa anasikia sauti kama ya cherehani ikilia mle chumbani.Kila jioni akipita anaisikia hiyo sauti,mpaka akawa anajiuliza,huyu fundi cherehani huwa hachoki?
Kumbe ile sauti huwa si cherehani,bali ni sauti ya feni mbovu ambayo huwashwa kila jioni,ile feni imelegea kwa hiyo kila inapozunguka inakuwa inapiga kelele kama vile mtu anashona.Basi jamaa akawa anajua kile kinacholia ni cherehani na mule kuna mtu anashona.
Sasa weekend jamaa hupumzika,alikuwa na jeans (suruali) yake anataka ipunguzwe,ikabidi aichukue mida ya mchana akaenda kwenye ile nyumba.Kufika akaulizia fundi cherehani wa kumpunguzia nguo yake.
Alipofika pale yeye kwa uhakika akasema tu nimeleta nguo,vipi fundi nimemkuta,??Kuulizwa fundi gani?akasema wa kushona nguo...akaambiwa hapa hakuna fundi wala hajawahi kuishi fundi.
Jamaa analazimisha kuwa kuna fundi,mbona kila siku akipita kwenye dirisha (anaonyeshea) huwa ansikia suti ya cherehani?Tena zaidi ya mara mia anaisikia.Akulizwa chumba gani?akaonyesha...akaulizwa umejuaje?aksema huwa nasikia kupitia dirishani!!
Duuuh!!Kumbe hapo juzi yake watu walifurumushwa kwa kupiga chabo,wacha jamaa aanze kubanwa,sasa kujieleza zero,akawa anajichanganya maelezo,akaonekana ni mpiga chabo na pale alikuja tu kusoma alama za usiku.
Kilishushwa kipigo,mpaka kuja kumsaidia jamaa katoka nundu mbili tatu...Msisitizo ukawa;We ulijuaje ndani kuna cherehani wakati hujawahi kufika?Jamaa asijue kumbe ilikuwa feni mbovu inayolia kama cherehani.