Vituko mitumbani

Vituko mitumbani

LOTH HEMA

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2015
Posts
26,860
Reaction score
41,401
Watu wamejazana kusachi mifukoni ili angalau watapata hela zilizosahaulika na wenye nguo wa awali. Kuna wafanyabiashara wa nguo za mitumba ambao huwa hawachambui kwanza mitumba yao, wao hufungua palepale marobota na kuyamwaga watu wajichagulie nguo wanazozitaka. Utakuta watu wamejazana wakichagua huku wakisachi mifuko ya mitumba kumbe wengine wanasachi hela za kigeni. Wanapata sarafu na noti za nchi ambazo thamani yake haijulikani ukibadilisha na shilingi ya tanzania. Wanasachi wapate dola ya marekani, pound ya uingereza, euro, rand ya afrika kusini hawapati wanaishia kupata hela za nchi fulani ambazo hazijulikani thamani yake kubadilisha na shilingi ya tanzania na hazipo kwenye orodha ya fedha za kigeni zinazobadilishwa katika benki zetu. Ni kwamba mitumba ya marekani, uingereza haiji Tanzania, ingekuja basi dola na pound zingekutwa zimesahaulika humo mitumbani inayotoka kwenye hizo nchi. Dola ya marekani ndiyo inayotafutwa sana mitumbani
 
Siku jitu lije liifume dollar mia si litakenua mpaka tuone kidaka tonge..😂
 
Na Hatuachi kusachi ni kama Tunabeti tuu huku tukiamini

Ipo siku kanji atalia tuu😁
 
Sasa hivi kuna hela isiyojulikana thamani yake,wewe sema thamani ni ndogo,

Ndiyo madhara ya kununua smartphone kwaniaba ya kupiga picha kali
 
Back
Top Bottom