Ukiujua huu ukweli wala hutaumiza kichwa na hiyo gender. mzabzab, Mzee wa kupambania na Shimba ya Buyenze tulishaling'amua hilo mapema na hatuna siteresi kabisa yaani. Hakuna mwanamke wa peke yako hapa duniani!
Habari za leo wadau wa Tasnia ya kuku. Nimeona picha ya mayai mengi inazunguka kwenye mitandao ya kijamii.
Maelezo ya picha hiyo yanasema kwamba mayai hayo yametengenezwa na kiwanda cha wachina kilichopo Goba, Ubungo, DSM.
Naomba kusisitiza kuwa taarifa hizo sio za kweli na watu wabaya wametengeneza kwa nia ovu ya kupotosha jamii na kuharibu Tasnia ya kuku nchini ambayo inakua kwa kasi. Goba iko katika Manispaa ya Ubungo, hakuna kitu kama hicho. Tumefuatilia DSM yote hakuna taarifa kama hizi. Tumekuja kugundua kwamba picha hiyo ilipigwa nchini Indonesia kati ya mwaka 2016 na 2017. Mtu mbaya ameipakua picha hiyo kwenye internet na kuiwekea hayo maneno na kuanza kuisambaza kwenye groups za mitandao ya kijamii. Nawaomba tuzipuuze taarifa hizo na Serikali inalifanyia kazi jambo hili. Niwaombe ndugu zangu tusiendelee kusambaza taarifa hizi za kupotosha.
Ahsanteni sana
Hezron Nonga - Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo