Vituko mitandaoni. Tupia chako



Basi tuu huwa tunachukulia mapenzi na mahusiano kirahisi rahisi, tunamekutana, tunachat paap tayari tunahusiana kabla hata ya kufahamiana kiundani na kinagabubaga.

Sasa itokee umehusiana na mtu ambaye akili yake haielewi kwanini umemuacha na hataki kuelewa unauhuru wa kuendelea na mahusiano na mtu mwingine....

Kuna watu mkihusiana na mkaachana ubaki hivohivo singo, ukianza mahusiano mapya ana wewe...

Hio ni aina ya kichaa.

Nafikiria kufungua shirika lisilo la kiserikali NGO ambayo itakuwa linachambua haiba ya mtu unayetaka kuhusiana nae ikiwemo kupewa historia ya mahusiano yake na maamuzi yake pindi anapokuwa na hasira au na furaha sana.

Huyo binti hatokaa sawa hadi muda upite sana, kushuhudia uliohusiana nao wanakata roho ndani ya muda mfupi tena kikatili....😔😔😔

Inabidi aje vakesheni afrika kuondoa msongo ataokuwa nao.

Hapo ndugu wa wanaume wote rahisi kumtupia lawama kwamba chanzo cha hao watu kufa ni yeye...

Mungu amtie nguvu, mweeh!!
 
Dawa ya ufisadi hii hapa:



Mchoro wa karne ya 16 unaoonyesha kuchunwa ngozi akiwa hai kwa hakimu fisadi, Sisamnes, katika mwaka wa 500BC.

Sisamnes alikuwa hakimu wa kifalme fisadi wakati wa Cambyses ll katika Uajemi. Iligundulika kuwa alichukua hongo mahakamani na akatoa hukumu isiyo ya haki. Kwa sababu hiyo mfalme akaamuru akamatwe kwa ufisadi wake na akaamuru achunwe ngozi akiwa hai. Kabla ya kutoa hukumu mfalme alimuuliza Sisamnes ni nani alitaka kumteua kama mrithi wake. Sisamnes, kwa uchoyo wake, alimchagua mwanawe, Otanes. Mfalme alikubali na kumteua Otanes kuchukua nafasi ya baba yake. Baadaye alitoa hukumu na kuamuru kwamba ngozi iliyoondolewa ya Sisamnes itumike kutengeneza kiti ambacho hakimu mpya angekalia kortini ili kumkumbusha madhara yanayoweza kusababishwa na ufisadi.

Otanes, katika mashauri yake, alilazimika kukumbuka daima kwamba alikuwa ameketi kwenye ngozi ya baba yake aliyeuawa. Hii ilisaidia kuhakikisha haki na usawa katika vikao vyake vyote, mijadala na hukumu📌
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…