Siku moja natoka shule mchana jua limewaka hatari. Kulikuwa na matunda fulani matamu sana yanafanana na zabibu nyekundu kwa Kisukuma yanaitwa nhundwa. Basi nikayaona yameiva mtini huyo nikatupa kimfuko cha madaftari huko nikaenda kuparamia. Kumbe ndo maviota ya hawa jamaa yako pale. Ukisikia kula za uso ndo siku hiyo sasa. Walinitandika nikatoka mbio mpaka home hata mfuko wa madaftari sikuukumbuka tena. Kichwa chote moto, kamasi si kamasi na kesho yake hata shule sikwenda...heshima yao sana hawa jamaa hapo muziki wao haufikii wa nyuki wala nge!
#tbt