Kusema kweli inabidi ule. Tena ule hasa. Usipokula yaweza kuonekana pengine umewadharau hawajui kupika, unaona pengine mazingira ni machafu, unajiona na sababu zingine kibao. Kama huna uwezo wa kula ugali angalau basi ule nyama. Kawaida ni mbuzi utachinjiwa au kuku mzima mzima kila mara utakapokwenda ukweni mpaka baadaye sana utakapozoeleka. Kama huwezi kula mwambie mkeo/mchumba wako akakutetee huko kwa wapikaji!
View attachment 2075258