Kama unatumia App nenda kwenye settings za simu yako halafu fungua apps then app ya Jamii Forums. Fungua storage halafu clear data. Close apps.. Rudi sasa ufungue JF yenyewe na itakulazimu ulogin upya. Sasa panel yako itakuwa populated. Nenda kwenye settings na moja kwa moja kwenye signature. Just turn it off na utakuwa umemaliza kazi.
Usisahau kuleta mrejesho!
NB: Jenga tabia ya kuwa unasafisha cache za apps unazozitumia sana. Makorokocho yakirundikana huko unakuta app inakuwa nzito sana na hata ku-misbehave.
Utaratibu wa kusafisha cache ni ule ule kama wa data. Ukifika kwenye storage unachagua cache badala ya data. Na unasafisha cache kama hutaki kulogin upya kwa sababu ukisafisha data unafuta kumbukumbu zote za app.