Kwa Tanzania lo lote lawezekana mkuu. Huko kwenu baada ya Muigai hapo mwaka kesho unafikiri ni nani atachukua? Rutto? Odinga? Ila siasa zenu ngumu kidogo kwa sababu zinaingiza na mambo ya ukabila kidogo.
Siasa hutegemea na namna gani utacheza na akili za wajinga wengi ili wakupe uongozi, unaweza ukatumia ukabila, dini, rangi, ukanda, uchama na kadhalika, na hamna nchi isiyokua na hizi mbinu.
Hata Tanzania tumeshuhudia Magufuli akitumia Usukuma maana ndio wengi, alikua akiomba kura kwa Kisukuma na kujifanya mmoja wao ilhali ukweli anatoka kwa kabila ndogo lililojificha huko Usukumani, pia akatumia ukanda, na uchama na hata udini.
Hamna namna unaweza ukashinda urais hapa Afrika bila kuwalemaza watu kwenye ubongo, na huo ndio ujinga ulioko kwetu huku, pumba tupu mijitu inatokwa povu na kuvimba mishipa ikitetea kiongozi kisa katokea kwao au kanda yake.