Kwani wakifuata sayansi na nyungu zikaendelea kupigwa kuna tatizo? Nimependa majibu ya Muhimbili. Kwamba wanaifanyia utafiti wa kisayansi nyungu kama ni tiba - sawa tu na hizi chanjo ambazo kimsingi hatujui madhara yake huko mbele ya safari hasa ukizingatia kuwa zimetengenezwa kwa kutumia tekinolojia mpya ambayo hakuna anayejua madhara yake ya muda mrefu. Kwa huu ugonjwa hakuna mwenye majibu mepesi.