Vituko mitandaoni. Tupia chako

#HABARI Jeshi Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata Mariam Fransisco Renatus (22) kwa tuhuma za kumuiba mtoto wa (Miezi 10) Miracle Ayoub eneo la Gongo la Mboto, Dar es Salaam na kwenda nae Geita, kijiji cha Bugalama.

Imeelezwa kuwa Mwizi huyo alijifanya msaidizi wa kazi na baadae kupata fursa ya kumuiba mtoto huyo.

Uchunguzi wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa mtuhumiwa alimuiba mtoto huyo kwa lengo la kuwaridhisha familia ya wakwe zake baada ya kuwadanganya kuwa alijifungua mtoto tangu mwezi wa Mei, 2023 baada ya kuwa na mahusiano na kijana wao. #EastAfricaRadio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…