Aisee sikumbuki. Akina nani hao? Najua Mkapa alikuwa na bifu na Jenerali Ulimwengu ila sina uhakika kama sekeseke la uhalali wa uraia wake lilikuwa kipindi cha Mkapa, J.K au Magufuli.
Jenerali Ulimwengu na Mkapa walikuwa marafiki tangu wakiwa Daily News.
Inadaiwa baada ya Mkapa kupanda cheo (urais)Jenerali alianza kumchapa kupitia magazeti yake.
Mkapa naye akaona isiwe tabu, akakinukisha.
Wakati huo Ulimwengu alikuwa mjumbe NEC akaunganishwa na wenzake akina Dr Maudline Castico, Anatoly Amani na wengine wawili nimewasahau.
Lakini wote walikuwa wajumbe wa vikao mbalimbali vya CCM.
Baadaye wakaambiwa waombe tena ili kujihalalishia uraia wao.
Waliomba.
Naona mama Castico bado yupo CCM anapiga kazi