Mbona wewe mleta mada hujasema unafanya shughuli gani?? Wewe ni mfanyakazi au mwanafunzi?..ulimaliza chuo?
Amalize chuo ndo mngeoana? hapo hujaweka muda wa kutafuta kazi, kujipanga kidogo kimaisha,n.k!
Inaonesha huyo mwanafunzi unamtunza (unamuweka mjini)..na umempa laptop, sijajua huwa unampa pesa kiasi gani kwa ajili ya matumizi,lol..???
Pia usipaniki sana. Kwa sababu bado hujaujua ukweli..usikubali maneno ya kuambia sana, pia inawezekana umekuwa msumbufu mno, yaani kila wakati unataka kuwasiliana naye, wewe mwenyewe jichunguze.,
Mpe nafasi na muda ajipange, akuweke mambo yote wazi. Kama inawezakana, omba mkutane naye uso kwa uso mzungumze. usimuogope wala kunyong'onyea mbele yake (maana wasichana wengi mkiwa mbele ya wanaume mnajiumauma)..mwambie msimamo wako. Pia huwezi kujua imekuwaje huyo msichana amekuwa akikujibu..Chunguza vizuri kabla ya kuamua kama kweli unampenda.
Usiogope, tulia chini..muombee kwa Mungu, na wewe pia uwe na amani..