Vitu Vine ili tuendelee

Jibaba Bonge

JF-Expert Member
May 6, 2008
1,246
401
Kuna msemo huu 'Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne:-
1. Ardhi
2. Watu
3. Siasa Safi
4. Uongozi bora

Wana JF nina uhakika na namba 1&2 kwamba vipo. sijui namba kuhusu namba 3&4. nisaidieni wapi tumekwama.
 
Last edited:
Ili uweze kujiuliza kama tuna "siasa safi", lazima upambanue kwanza "siasa" ni nini. Kwani tuna siasa gani kwa sasa? Ukijibu hilo kwa makini, basi itakwa rahisi kusema kama hiyo siasa ni bora.

Tuna uhakika wa vitu vitatu, na sio viwili. Tuna uhakika kwamba tuna ardhi, tuna watu, na hatuna viongozi bora.
 
Kuna msemo huu 'Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne:-
1. Ardhi
2. Watu
3. Siasa Safi
4. Uongozi bora

Wana JF nina uhakika na namba 1&2 kwamba vipo. sijui namba kuhusu namba 3&4. nisaidieni wapi tumekwama.

Nadhani kuna jambo dogo sana lilikosewa hapa. Kama 3 & 4 vilipewa sifa muhimu kwanini 1&2 havikupewa? Kwa mfano 1. Ardhi nzuri -hiyo tunayo mpaka dunia nzima inataka kuhamia kwetu na majirani wanataka kutupora.
2. Watu walioelimika. Au labda niseme Taifa lililoelimika? Au lenye % kubwa ya watu wenye elimu? I am sure nimeeleweka.
Maana sioni uwezekano wa kuwa na lolote kama kutakuwa na ardhi nyingi tu ambayo ni jangwa tupu ikaleta maendeleo. Na pia kuwa na watu wachache waliosoma tena bahati mbaya siasa tupu, wakapiga siasa safi tuu waliobaki hawaelewi hakuna utaalam and no skills. Hiyo ardhi wataitumiaje? Hii inaleta yale ya Meremeta kutusuta zaidi, madini tunayo lakini tunaenda kuita wageni waje kuyachukua wakatajirikie kwao. Na kwa kukosa kuelimika wanaturudishia shukrani ya bunduki ili tuzitumie kuuana wenyewe kwa wenyewe na tunazipokea.

Kwahiyo ningesema:
1. Ardhi nzuri
2.Watu walioelimika
3.Siasa safi na
4.Uongozi bora
FULL STOP!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom