Vitu Rais Magufuli anavyofavya vizuri na vibaya

Vitu Rais Magufuli anavyofavya vizuri na vibaya

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,753
Reaction score
15,445
Mambo makubwa ambayo Rais Magufuli anafanya vizuri na makubwa ambayo anafanya vibaya. Rais Magufuli tofauti yake kuna mambo ambayo anafanya vizuri sana na mengine anafanya vibaya sana

Mazuri:
  • Kujaribu kupunguza vitu vinavyopunguza uwekezaji kama kodi ambazo sio nzuri, mfumuko wa bei, na vibali ambavyo si vya lazima.
  • Rushwa - Mtandao wa rushwa ulikuwa mkubwa sana. Bandarini, kwenye madini, uingizaji wa chakula, viwanja, ujenzi ambao hauendani na gharama n.k
  • Miradi mikubwa - Mradi wa Treni, umeme vijijini, pipeline ya Uganda, barabara na mradi wa bwawa la maji. Ndege sijui kama bado zitasaidia sina uhakika bado.
  • Kubadilisha utamaduni wa kuwa wazembe na kutokujiamini. Tulikuwa na utamaduni wa kutokujiamini na kufikiri rushwa na wenye nacho hawataweza kuisha.
Mabaya:
  • Kuogopa demokrasia. Mawazo ya kuogopa demokrasia na kuona kama ni adui wa maendeleo au demokrasia inaleta vurugu si ya kweli. Hayana ushahidi na yataweka nchi yetu pabaya kwa miaka mingi ijayo.
  • Kutokupenda kukosolewa. Hili ni tatizo kama Rais hutakiwi kutokupenda kukoselewa, kusema au hata kutaniwa. Hii haiendani na utamaduni wetu. Kama hupendi kukosolewa basi usipende kusifiwa.
  • Hakuna mabadiliko ya mfumo. Hakuna jitihada za kurekebisha mfumo mbaya badala yake sasa serikali inategemea sana Rais na wasiwasi akiondoka baada ya miaka mitano hatujui kama hizi jitihada zitaendelea.
  • Kilimo bado si kipaumbele bado serikali hii haijachukulia kilimo kama kitu muhimu. Kilimo kinataka uwekezaji mkubwa ili kiweze kukua.
  • Hakuna sera ya ajira na ubunifu wa utengenezaji wa ajira kwa viwanda. Kilimo cha kisasa kingeweza kuleta kazi lakini hakuna ubunifu.
 
Hizo ndege zake haziwezi kukuza uchumi kama diplomasia inamshinda.ona kwa sasa ndege hazikanyagi South Africa kuogopa kudakwa
 
Back
Top Bottom