Gini
JF-Expert Member
- Oct 11, 2018
- 398
- 385
Ndoa ni sunna na inatakiwa kuwa handled kwa namna ya kipekee mno. Naongelea Ndoa na si Mahusiano.
Mke katika safari yake ya Ndoa anahitaji vitu kadhaa ambavyo ni muhimu zaidi kwake, nitavitaja vichache
(i): Kushirikishwa,
(ii): Kusikilizwa.
(iii): Heshima
Ni muhimu kuachana na mambo kadhaa unapoamua kuanzisha Ndoa. Kwa mfano, ulizoea kurudi nyumbani usiku kwa kuwa ulikuwa na rafiki zako sehemu. Outing zenu zitakuwa za pamoja, mawasiliano yasiyo ya msingi utapunguza kama si kuachana nayo kabisa.
Mshirikishe Mwenzio.
(i): Usipomshirikisha Mkeo katika maswala ya pamoja (familia) ni kama umetengeneza bomu ndani ya nyumba. #Deborah Tannes katika kitabu chake cha “You Just Don't Understand” anatoa mfano huu, ”Siku 1 Josh alimualika wikiendi rafiki yake wa muda mrefu waliyesoma nae high school ili kuzungumza mawili matatu pamoja na mkewe Linda, wiki hiyo hiyo Linda akiwa ametoka katika maswala yake ya kibiashara. Deborah Tannes anaendelea kusema kuwa Linda (mke wa Josh) alichukia sana kwa nini Josh hakumwambia juu ya ujio wa rafiki yake”, na Linda akachukia kweli kweli na akanuna hasa. Kwamba Linda alighafirika kwa kuwa tu hakushirikishwa, “kwa nini hakuniambia, ina maana sina umuhimu kwake au ndiyo ameanza dharau", alijisemea Linda.
Alichotaka Linda si kuamua (Permission) juu ya ujio wa rafiki yake Josh bali kujulishwa (Negotiation). Unaweza kuona ni jambo dogo sana lakini kwa Mwanamke si hivyo. Kutomshirikisha mambo yanayowaunganisha kunaibua hisia za kudharauliwa, anahisi kutoheshimika, anajiona kutokuwa sehemu ya familia, anajiona kutengwa.
Kisaikolojia hii ni mbaya sana, Mke ni mfano wa mche wa mti uliouotesha katika bustani, namna unaulinda na kuutunza ndivyo unachipua na kuimarika. Bahati mbaya Wanaume wa sasa tuna msemo “We tafuta hela mzee, mambo mengine yataji-set”. Hii nadharia sio sahihii sana, pesa ina nafasi tu katika kutekeleza mahitaji ila haina nafasi ya kuitunza ndoa. Itakuwa na nafasi katika dates, katika ndoa pesa ni matumizi ya kila siku. Tuwashirikishe hata kama ni mambo unayoona kuwa ni ya kipuuzi, ndiye mshauri wako wa kwanza (Mke na sio Mpenzi), naomba nileleweke tafadhali.
(ii): Kusikilizwa
Katika Chapisho/Kitabu cha “The Female Brain” lililochapishwa mwaka 2006, Louann Brizendine, M.D anasema katika andiko lake kuwa kwa siku mwanamke ana maneno 20,000 ya kuzungumza wakati mwanaume akiwa na maneno 7,000 tu. Ndipo inapokuja dhana ya umbea waachie wanawake. Tenga muda wakumsikiliza mkeo, haijalishi anazungumza nini, maneno 20,000 sio mchezo, yakibaki ndani yanakuwa sumu. Msikilize tu hata kama huyapi kupaumbele ila usimuoneshe kuwa hapa umeongea pumba. Onesha kum support halafu uoneshe kushauri na si kumpuuzia. Na ndiyo maana wakati mwingine atakuita “Mume wangu” unaitika ndiyo baby, ghafla anakwambia “Au basi”, wewe mchukulie vivyo hivyo. Ukimpuuza na akagundua, atakachokifanya ni kuhamia sehemu anayopewa attention, huko sasa atayaongea yote, ni kama anakuchongea “yaani wanaume wengine Bwana, yuko busy muda wote, mke wake kila nikimwambia hili yuko busy”.
Hakuna mwanamke utakaejitahidi kumuonesha unajali hata kile ukionacho wewe ni upuuzi akakengeuka, otherwise ni tabia yake tu, nimewahi kuandika juu ya ugumu uliopo kumbadilisha mtu tabia. Kikubwa ni kuhakikisha unapoingia katika Ndoa wote mpendane, yaani upendo usiegemee upande mmoja, ni rahisi kuelekezana. Usiolewe/kuoa kisa tu umri umeenda, Ndoa ni commitment hasa za Kikristo. Mjue mwenzio, wapi, kwa nini, saa ngapi, lini na nini anapedelea, anahitaji aidha ufanye kwake. Tutafute pesa wazee ila tusiasahau kuwa pesa ni kwa ajili ya ku pay bills na sio vinginevyo, ukim ignore kisa anaongeaga utumbo, kuna wenzako utumbo huo wanampa muda wa kumsikiliza kisha unaanza kutumia pesa zako kuomba ushauri kwa wana n.k unnecessarily.
Mwl. George Sylvester Wambura.