Vitu gani humpagawisha mwanaume/ mwanamke!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vitu gani humpagawisha mwanaume/ mwanamke!!!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jpinduzi, Oct 8, 2011.

 1. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #1
  Oct 8, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  habar za wkend wadau!leo katika pitapita kwenye mablog nikaona maneno matamu matamu yakanivutia kuyaweka hapa JF!Samahanin kama yalishakwishwa wekwa hapa JF!bas tujimvuzishe.

  Kila mwanaume anapaswa kujua nini kinachomfanya mwanamke/msichana apagawe kunako sita kwa sita, hali kadhalika mwanamke anapaswa kufahamu mambo kadha wa kadhaa ambayo akimfanyia mwenza wake atamfanya avishinde vishawishi vya kumsaliti. Hii inamaanisha nini?

  Inamaanisha kuwa, kila mwanaume na mwanamke anapaswa kufahamu jinsi gani wanaume walivyo tofauti na wanawake.

  Mwanamke anapaswa kufahamu kwamba wanaume huamsha hisia za mapenzi kutokana na kile wanachokiona. Hivyo pindi anapoona msichana mwenye shepu akiwa amevaa nguo inayoiweka shepu yake bayana, ghafla hisia kali za mapenzi humjia, hata kama anajua baadhi ya utu ama tabia zake mbaya.

  Kuona tu jinsi binti alivyoumbika, hiyo ni tosha kwake kumfanya ahitaji kuwa naye faragha na hapo ndipo atakapoanza kupigana na mhemuko wa mwili wake kujizuia kuingia katika kishawishi cha kufanya ngono na mrembo aliyemuona.

  Kwa upande mwingine, wanaume wanapaswa kufahamu kwamba wanawake wapo tofauti. Hisia za mapenzi za mwanamke huamka pindi mwanaume anapomtimizia mahitaji yake ya moyo wake. Huhisi kupagawa pindi anapokutana na mtu ambaye anaweka kipaumbele mawasiliano baina yao na kujali hisia ama mawazo yake.

  Kwa mwanamke muelewa mara nyingi muonekano wenye mvuto pekee kwake haumuingizi kwenye vishawishi kwa kiasi kikubwa kama ilivyo kwa wanaume. Kitu pekee kwake kinachoamsha hisia zake za mapenzi kwa haraka zaidi ni kuwa na mwanaume anayeongea naye, kumsikiliza, kuthamini mawazo yake, na kufikiria mahitaji yake muhimu. Pindi mwanaume wa aina hii anapomwambia “ Nakupenda..muache mumeo tutumia usiku wa leo pamoja,” huhitaji kutumia busara na hekima kuweza kuvishinda vishawishi vya kutoa penzi kwa mwanaume wa aina hiyo!


  Aidha, watu wengi walio katika mahusiano hujikuta wakikumbwa na matatizo kadha wa kadha wawapo faragha kwa sababu tu mwanaume na mwanamke hawajui tofauti iliyopo baina ya mwanaume na mwanamke. Mfano, mwanamke anaweza kupanda kitandani akiwa amevaa pajama ambalo halioneshi shepu yake huku mwanaume akitamani kumuona mpenzi wake akiwa amevalia nguo ya usiku inayomtia hamasa ya mapenzi ama kumuona akiwa hajavaa chochote! Anahitaji kumuona mpenzi wake vema hivyo kumuona akiwa katika vazi lisilompa nafasi hiyo kunamkwaza.

  Hapa kosa kubwa lipo miongoni mwa wanawake wengi ni kuwa “ Ameshaniona mwili wangu zaidi ya mara 1000.” Hivyo kwao kumpa nafasi mwenza wake kuuona mwili wake hakuna umuhimu.

  Kimsingi wanawake wa namna hii ndio mara nyingi hujikuta waume zao pindi wanaporejea nyumbani huishia sebuleni na kusoma gazeti. Anajihisi kuchoka, hahitaji mkewe ama mtoto amsumbue na akikalibishwa mezani kwaajili ya chakula huongea maneno yasiyozidi kumi.

  Hufanya haya yote si kwa sababu anamchukia mkewe la hasha bali hugeuka kuwa mbinafsi anayetaka kutumia muda wake kujipumzisha na kufikiria mahitaji yake na si ya mwenza wake.

  Hatua hiyo ikijitokeza baina ya wapendanao mambo huharibika, hamasa ya mapenzi kwa mmoja wao hutoweka kwani inapofika wakati wa kwenda kujipumzisha kitandani. Mwanaume anapomuona mwenza wake akitoka bafuni akiwa na kanga moja iliyomshika vema maungo yake, mapigo ya moyo na damu humuenda mbio akitamani kumkumbatia bibie ili apate kitu roho inapenda!

  Wakati mwanaume akiwaza hayo, mambo huwa tofauti kwa mwanamke kwani hutawaliwa na maswali kadhaa kama “ Hivi ni kweli ananipenda? Namashaka. Haongei nami wala kunisaidia kwa lolote. Anachotaka ni kunitumia kama chombo cha starehe tu huyu.”

  Hivyo basi, mwanamke atamuachia mwenza wake mwili autumie atakavyo kutimiza haja zake, lakini hatafika kilele kamwe kwani hatahisi anapendwa bali anatumiwa kama chombo cha starehe.

  Hata hivyo, pindi mwanaume atakapokuwa akijipa raha toka kwa mwenza wake huyo, atatawaliwa na woga kwa sababu ataona wazi kuwa bibie hafurahii tendo la ndoa. Hivyo atajiuliza maswali mengi “ Kwa nini nimeshindwa kumpagawisha mamaa? Je, nyeti yangu ni ndogo?”

  Hapa ndipo mwanamke anapotakiwa kumueleza bayana kuwa, “ Uume wako upo sawa ila mawasiliano yako kwangfu ni finyu.”

  Kimsingi mwanaume anaporudi toka kazini anapaswa kuzungumza na mwenza wake, kujenga urafiki naye, kumuoneshe kuwa anamjali na kuthamini utu wake na usimfanye ajione kama mtu baki.

  Aidha, mwanaume anapaswa kumueleza mwenza wake kuwa, “ Unapokuwa kwenye jumuia, vaa nguo ambazo hazitaamsha hisia za mapenzi kwa watu baki, lakini unapokuwa nyumbani hakikisha unavaa nguo hizo kwaajili yangu tu.”

  Kufanya hivyo kutamueleza mumeo kuwa, “unampenda yeye tu na wanaume wengine hawana nafasi katika moyo wako!

  Mwisho nimalize kwa kusema kuwa, wanawake huamsha hisia za mapenzi kwa wanaume ambao huyapa kipaumbele mawasiliano, lakini mawasiliano hayo humpagawisha zaidi yakiwa ya kirafiki zaidi (fanya kama unawasiliana na rafiki yako, usiogope kumchombeza na utani inapobidi) na pia hukoshwa na wanaume wanaowajali.

  Kwa upande wa mwanaume, yeye hisia zake huamka pindi anapoona shepu (wapo wanaopenda wenye figa za kibantu na wengine za kimiss).

  Hivyo, kama mmefanikiwa kupata watoto wa wa kike hakikisheni mnawaeleza kuwa, nguo za aina fulani huamsha hisia za mapenzi kwa wanaume, kwa hivyo waache kuzivaa nyumbani hata mitaani kujiepusha na vishawishi. Wakristo wanaweza kusoma (Mathayo 5:28).
   
 2. JICHO LA 3

  JICHO LA 3 JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  in red hii nayo inachangia.........mh nieleweshe.
   
 3. AMINATA 9

  AMINATA 9 JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2011
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 2,132
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  mi naona ni kuheshimiana na kujaliana ,kuweko pale unapoitajika mfano ktk shida na raha ................kujituma mkiwa mchezoni ili kila mtu aridhike na mwenzi wake na hayo mengine sasa ni wadhamini tu muhimu ni hivi
   
 4. the grate

  the grate JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2011
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  thnx nimelearn kitu kipya
   
 5. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Makes sense.... but mi najua vingine hawakuweka hapa...
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mhhhhhhhhhhhhhhhh
   
 7. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  pamoja ya kuwa sikuimaliza kuisoma yote ila mistari michache niliyoisoma inatosha. Ushauri wako umesomeka.
   
 8. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Unabisha?
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  nabisha......lol
   
 10. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nimesha kusoma Boss, we unataka kunitega, niseme ngojanikuoneshe kama I mean it alafu ufaidi masiri yangu ya kupagawisha wanaume. Hunipati N'go! lol
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  nilijua hana kitu lol
   
 12. Bambanza jr.

  Bambanza jr. JF-Expert Member

  #12
  Oct 8, 2011
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tusaidie unayojua kwa uzoefu wako!
   
 13. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Kupagawisha ndio nini?
   
 14. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #14
  Oct 8, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ok bana waloko kwenye ndoa wafuatilie haya watuletee feedback
   
 15. M

  MyTz JF-Expert Member

  #15
  Oct 8, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nPM nikujuze...
   
 16. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #16
  Oct 8, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  si uniambie hapa hapa.
   
 17. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #17
  Oct 8, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Maana yake vinamfanya anachanganyikiwa kabisa (but utaona kuna mtu atabisha hata hii...)
   
 18. N

  Natalie Senior Member

  #18
  Oct 8, 2011
  Joined: Sep 25, 2011
  Messages: 165
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  It's right.
   
 19. Rwebangira

  Rwebangira Member

  #19
  Oct 8, 2011
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nahisi yatakuwa ni mtazamo vinginevyo onyesha uzoefu wa hayo! mnh!! lakini inaweza kusaidia ingawa suala la kupenda kwa kuona ni tata mno kwani inategemea ni sehemu gani angependa kuona ili apagawe/apende.
   
 20. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #20
  Oct 8, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  umezaa umenenepeana inside you feel old and unattractive utakumbuka kweli kuvaa sexy underwear mumeo akuone???mnh i doubt ndoa nyingi ni kubakana tu kwa kwenda mbele siku zinasonga...................
   
Loading...