Vitu 5 Vya Kupewa Kipaumbele na Serikali ya 2010-2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vitu 5 Vya Kupewa Kipaumbele na Serikali ya 2010-2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chapakazi, Jun 4, 2010.

 1. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ninapokaa chini na kuwaza juu ya Tz na mwendo wetu, naona vitu 5 vinavyohitaji kupewa kipaumbele kwa serikali ijayo kwa kusudi la kuweza kupiga hatua kubwa mbele. Ningependa kuona hivi vitu vikigusiwa kwa undani zaidi hasa tunapoingia katika kipindi cha kampeni. Kusema kweli, hivi sio vitu vikubwa, kiasi cha kusema tutahitaji msaada kutoka nje, bali naamini tukifanya kazi pamoja tutaweza kuvifanyia kazi na hatimaye kuvimudu bila matatizo. Ni aibu kwa nchi itakayosherekea miaka 49 ya uhuru kuwa na mazungumzo kila siku juu ya hivi vitu. Basi vitu vyenyewe ni:

  1) Umeme

  Ningependa kuona umeme ulioa sambaa nchi nzima (kwa sasa ni asilimia 12 tu ya nchi yenye umeme), usio haba (migao) na wa bei itakayowezwa na waTz wote.
  Understandably hili litakuwa gumu hasa katika vijiji vilivyo mbali. Lakini hi indo challenge tuliyo nayo! Tuna ma-engeneer, nk kutoka UD. What are they for, if not to put their brains into usage.
  Kwa hili lote kufanyika ndani ya miaka 5 ni ngumu, lakini at least kuwe na ‘a master plan' itakayofanyiwa kazi bila kujali serikali zitakazofuata – yani a continuous program ambayo haitabadilishwa kiholela na serikali zitakazofuata!

  2) Maji

  Ningependa kuona maji yanafika katika bomba za kila nyumba Tz.
  Matatizo ni yale yale kama ya umeme, lakini yanawezekana.
  Kutengeneza ‘a master plan' kama ya umeme itafaa sana hapa.
  P.S: Hizi master plan ziwe wazi kwa kila mtu kufuatilia. Kwa mfano…ifunguliwe website, na kuwe na regular reports zake katika vyombo vya habari.

  3) Reli na Bandari

  Usafiri wa treni kuboreshwa - hasa reli ya kati, na kuboresha ufanisi wa bandari zetu.
  Kweli hii sasa imekuwa kichekesho, na imefika muda muafaka wa kuacha kukenua na nyani! Kama tuliowapa contract wameshindwa…tuwanyang'anye! Simple and clear! Hakuna haja ya kuzunguka mbuyu tena! It's time for action. Na Hili halihitaji muda mrefu kufanyikisha…it takes one sentence to break a contract!!
  Ufasihi wa reli na bandari utarahisisha usafirishaji wa bidhaa ndani ya nchi na kuelekea katika mipaka na nchi jirani….ikiwa na maana ya pesa, mapato, ajira, nk!!!

  4) Imports

  Kupunguza imports na kuwapa Watz kipaumbele katika ujenzi wa viwanda na kukazania ubora wa bidhaa za nchi
  China itaua uchumi wetu kabla ya kupiga hatua mbele. Marekani can afford to have mass imports from China, as their economy has graduated from Primary good production economy to a tertiary based economy. Sasa sisi hata level 2 hatujafika – yaani manufacturing economy. By allowing cheap imports we are simply restraining our ability to move to that stage. Manufacturing sector ni ya kupewa kipaumbele sana katika awamu ijayo!

  5) Safari za nje

  Kupunguza safari za viongozi na watumishi serikalini. Ikiwezekana, bajeti za safari za kila wizara kwenda nje ya nchi zikatwe kwa nusu. Na Rais apunguziwe muda anaoweza kutumia nje ya nchi hasa anapokuwa katika shughuli za kitaifa. Kwa mfano…roughly Rais anakuwa na madaraka kwa kipindi cha siku 1825 tu! Tukimpa siku 150 nje ya nchi ni muda wa kutosha kabisa. Huyu ni rais wetu tuliyemchagua, na hivyo tuna haki ya ku-limit muda atakao kuwa mbali nasi! Hii sio contract au nini...its a simple must do! Pia, kwa maoni yangu, Tz ina kila kitu tunachohitaji kuendelea hapahapa. Hii kwenda nje ya nchi ni upumbavu tu!

  Anyway…that is what I would look for in the next regime! Simple and basic developments. Na sitaki hizi kelele za Maisha Bora kwa kila mtanzania. Hizi ni open statements zisizo na msingi wowote wala uwezo wa kupima mafanikio yake! Kwangu mimi kama hivi vitaweza kushughulikiwa...basi that would be a successful regime!
  PS….Holla to the 1000th post!
   
 2. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  suala la reli na bandari ni aibu kwa taifa letu, kama tungeboresha hivyo vitu, kwakweli tungefaidika sana...lakini ni kama tunakosa viongozi wenye nia vileee, watu wenye uchungu na nchi
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,522
  Likes Received: 81,905
  Trophy Points: 280
  Kuboresha drainage systems ya Dar na pia kuhakikisha usafi wa jiji ambalo sasa limekithiri kwa uchafu na hata kunuka..sidhani kama tunahitaji forex au expatriates kuyafanikisha yote haya.
   
 4. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hilo mh itabidi tuwape Madiwani...maana hiyo ni kazi ya halmashauri ya mji/jiji! Hivyo ni watu wa Dar kuamka na kuweka hiyo katika TO-DO List yao by 2015!!! Kama hawawezi sijui tuwasaidiaje! Sio mkazi wa DSM mie...hahaha!
   
 5. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2010
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,498
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  Mtoto,
  Japo mi siyo baba yako lakini naomba nikurekebishe kidogo hapo namba 5 kwenye RED. Hicho si kipaumbele bali ni challenge ambayo serikali inatakiwa kui-encounter ili ionekane inawajibika mbele ya wananchi. Kuacha kula rushwa au ku-refrain from ufisadi haviwezi kuwa vipaumbele bali ni wajibu, you like it or not, you must do/not do it, basi!
   
 6. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  mhhh...mh ningependa kupingana nawe! By just looking, kila kitu hapo ni challenge...au sio? Kipaumbele - as i define it...ni kukiweka kitu at the frontline. kwa hiyo (kutumia mfano wako) kupigana na rushwa kunaweza kuwa kipaumbele cha serikali ya awamu yeyote even though ni wajibu weke! It simply means they put that upfront! Sijui wewe una-define kipaumbele vipi?
   
 7. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2010
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nina wasiwasi kama hivo vipaumbele vyako ndo VIKUU ambavyo vinaweza kuinua UCHUMI au KERO kwa 85% ya watanzania waishiyo vijiji.
   
 8. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mtoto hivyo ulivyo sema ni muhimu sana na natumai ulikaa uka tafakari ndiyo maana ukaja na hivyo vipaumbele. Kila awamu au serikali lazima iwe na vipaumbele(priorities) lakini kwetu inaelekea tuna taka kuchovya chovya kila mahari. Anyway mimi nakuja na vipau mbele vyangu mwenyewe na ni hivi vifuatavyo.

  1)Afya(Health care system)
  Kuna msemo usemao "A healthy person is a wealthy person). Tuki imarisha na kuboresha sekta ya afya nchini kuta kuwa na mafanikio na mabadiliko yafuatayo.
  A)Urefu wa maisha uta ongezeka. Hii ina maana miaka ya mtu kuwa productive itaongezeka.
  B)Watu wakiwa na afya ina maana hata katika umri wa production mtu ana kuwa na nguvu zaidi ya kimwili na kiakili kwa maana hiyo productivity haiongezeki tu bali ina imarika.
  C)Birth rate ita ongezeka. Birthrate ikiongezeka basi idadi ya watu nchini itaongezeka. Kama ilivyo wazi rasilimali kuu ya nchi yoyote ni watu wake.
  D)Viongozi hawata kuwa na sababu ya kwenda kutibiwa nje kwa kila kaugonjwa. Huko tunapo elekea hata maumizu ya kichwa kiongozi ata anza kutoka nje.

  2)Elimu
  Elimu ni lazima iboreshwe. Nadhani elimu lazima iwe kipaumbele cha nchi yoyote. Tukiwa na mfumo bora wa elimu na taifa litakavyo toa wasomi zaidi basi ndipo na sisi tuta faidika. Elimu iki imarishwa basi upeo na ufanisi utaongezeka. Kwa sasa mtu ana takiwa kufika tu lasaba kama shule ya msingi kitu ambacho kina sababisha taifa liwe na idadi weni ya watu walio ishia shule ya msingi tu. Ukiangalia siku hizi hata serikalini elimu ya chini wanayo angalia ni kidato cha nne sasa iweje kumfikisha mtoto lasaba tu ndiyo liwe lengo kuu? Haingii akilini. Tuna hitaji elimu, elimu na elimu zaidi.

  3)Miundombinu
  Kwangu mimi maji, umeme, reli na bandari zote zipo chini ya miundombinu. Pamoja na miundombino hiyo minne ambayo mkuu Mtoto umetoa mimi naongezea barabara. Lazima miundombinu yote ya nchi yaboreshwe. Ni gharama kubwa na zisizo za lazima kuendesha nchi yenye miundombinu mbovu. Gharama za umeme zinaongezeka inapo wabidi watumie umeme wa generator, barabara zikiwa mbovu basi bidhaa hazifiki zinapo takiwa katika muda unao takiwa nk. Miundombinu yote lazima iangaliwe na kuboreshwa.

  4)Biashara
  Hapa pia swala ulilo litaja la imports linaingia mkuu. Kama ulivyo sema lazima imports zipunguzwe na tuji tengezee wenyewe baadhi ya vitu. Ni aibu kama hata bidhaa kama vijiti vya meno na vibiriti vina toka nje ya nchi. Pia tuna bidi tuangalie mikataba yetu na wawekezaji wa nje. Je tuna nufaika vipi na mikataba hiyo? Pia lazima ujasiriamali uhamasishwe. Hatuwezi kupunguza imports bila kuwa na wajasiriamali ambao watakua tayari kutengeneza bidhaa au kutoa huduma tunazo hitaji.

  5)Utafiti na teknolojia
  Nadhani bado hatuna pesa ya kushindana na nchi kubwa na zilizo endelea katika sekta hii pia sidhani kama tuna elimu hiyo kwa sasa. Ila teknolojia siyo lazima iwe ya kushindana na nchi zingine. Teknologia na tafiti zetu zinaweza zika kazania kuboresha hali yetu sisi wenyewe. Mara nyingi naona kwenye t.v. Mtanzania kavumbua kitu fulani ambacho ni practical kwa maisha yetu lakini hivyo vitu sijawahi kuja kuviona sokoni hata siku moja.

  Hivyo ndiyo vingekua vipaumbele vyangu kwa sasa. Nadhani serikali ni lazima waviangalie hivi vitu kwa ukaribu. Tukisha weza kuboresha hivyo vitu vitano nilivyo orodhesha hapo juu basi tuta piga hatua kubwa.
   
 9. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #9
  Jun 4, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Kama vipaumbele vyako ni hivi basi nchi yetu itachukua miaka 1000 kuoandokana na umaskini,ujinga,maradhi na ufisadi..
   
 10. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #10
  Jun 5, 2010
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,650
  Likes Received: 517
  Trophy Points: 280
  Mtoto,

  Ahsante kwa mawazo mazuri ya uboreshaji. Hata hivyo tatizo kubwa ni viongozi kuishia kuto maneno tu lakini utekelezaji hakuna. Vipaumbele vyako vitawezekana tu kama kila mtu kwenye nafasi yake atakuwa na mawazo yenye muelekeo sawa na wako.
  Kumbuka kuwa kwa sasa nchi inaendeshwa kwa mtindo wa BORA LIENDE!
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  Jun 5, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kipaumbele cha kwanza kabisa IS TO GET RID OF POLITICS. Bila hicho kipaumbele kutekelezwa mtaendelea kulialia kuhusu matatizo yaleyale, ninyi na vizazi vyenu mpaka Yesu atakaporudi.
   
 12. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #12
  Jun 5, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nipe vya kwako basi kama unaona vya kwangu havifai...
  P.S...naona na wewe u-mgombea mtarajiwa. Tupe basi hivyo vya kwako kusudi tuweze kukupima
   
 13. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #13
  Jun 5, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Sawa...lakini mimi nime-target specific things. Elimu kuboreshwa maana yake nini? How do u measure it. Hii ni politics talk. Weka a specific target...kwa mfano...tuwe na mwalimu mmoja kwa kila wanafunzi 20 katika muda wa miaka 3. Ukishindwa unakaa pembeni! Sasa unaposema elimu iboreshwe ni sawa na kusema maisha bora kwa kila mtanzania. Ni msemo usioweza kupimika. Kikwete anaweza ku-argue kuwa kaboresha elimu. Sina figures, lakini kwa mfano ukikuta enrolment ya vyuo imeongezeka katika kipindi chake...je hajaboresha elimu hapo?
  Na kusema kweli...unapoweka such a broad list...kama biashara, elimu, nk...you are targetting yourself for failure. Unatakiwa uangalie kwa undani zaidi. Kwa mfano katika biashara...ni kitu gani unataka kikuwe katika kipindi fulani? Sasa unaposema ku-limit imports...what about necessary ones? Inabidi uwe more specific mkuu. Thats the thing! For me...hivi ni vitu specific ambavyo unaweza kupima matokeo yake kirahisi! Na baada ya hapo...una move to the next level!
   
 14. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #14
  Jun 5, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  U know that is impossible...so lets get back to reality!
   
 15. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #15
  Jun 5, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ni kipi kisichowezekana ?
   
 16. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #16
  Jun 5, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  I am not targetting everyone with these vipaumbele. But am sure their effect will be felt throughout the country! Kwa mfano...wide spread electricity coverage at cheaper rates will equate to lower cost of productions. This will equate to lower priced goods (with a bit of arm twisting to the producers or certain incentives kama lower taxes,nk)
  2. Kwa upande wa maji...its just simply ridiculous! Watu wanaishi bila maji! AIBU
  3. Reli na bandari...again...these are key means of production. Will offer a lot of ajira na uwezo wa nchi kusafirisha goods!
  do i need to say more?
  Its a simple trickle down effect! Of course we are expecting some prudence in the administration of this!
  Lakini kwangu mimi binafsi nimechoka na ujinga unaoendelea!
   
 17. M

  Mkono JF-Expert Member

  #17
  Jun 5, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tutafikiria mengi ila kama mwenyezi Mungu hatatujalia kupata kiongozi ambaye anauwezo wa kuthubutu! ikiwa ni pomoja kuwa tayari kuitwa majina kama dikiteta na mabwana wa dunia hii ambao kila kukicha wanazidi kutafuta mbinu za kuendelea kuiba raslimari za waafrika itakuwa ni kazi bure.Niliwahi kujiuliza Nyerere alikuwa na maana gani kuwashindisha watu kwenye jua wakipiga kura za NDIYO na HAPANA kuchagua kati ya MTU na GIZA bila kupata majibu ila baada ya kuona watu wanalalamika juu ya ufisadi,huduma mbaya katika afya,elimu,miundo mbinu kama barabara,reli ,mishahara isiyokidhi mahitaji ya kila siku na bado watu hao ukiwauliza chanzo cha matatizo yao watakwambia kuwa ni uongozi mbuvu tulionao .Miaka mitano inapita wanarudia kuwapa uongozi walewale waliokuwa wakiwalaumu, kwa watu wanamna hii kuna haja gani ya kuwapa nafasi ya kufanya uchaguzi kama kweli una nia njema ya kuasaidia! Mi nafikiri hizi nchi za magharibi zilikuwa zilkilazimisha demokrasia kwa maslahi yao binafsi kwa nchi kama hii ya kwetu hatustahili kuwa na demokrasia ya namna hii.Jaribu kufikiria vijana wengi walikimbia vijini na kuja mjini kuwa vibaka na wakabaji wakikamatwa wanajitetea kuwa hali ya maisha ni ngumu hivi hawa wakilazimishwa kwenda hata haya mapori ya karibu kama Mukuranga na Kilwa wakapiga jembe si kuna hatua wanaweza kusogea,eti demokrasia watoto wa kuwa kuwa shule wapo kuanzia fire hadi magomeni kazi yao ni kuomba watu wenye magari huku wenyewe wakiwa wameisha jichokea na mi trafic jam.Demokrasia watu wanaiba kama walivyo fanya EPA bado wanapelekwa mahakamani tena kesi inachukua miaka huku watuhumiwa wakiendelea kuchapa kazi kama kawaida na pesa walizo iba,natofautiana sana na mfumo wa Kikwete katika kuendesha nchi ila kwa hili la wafanyakazi nlimkubali haiwezekani mwl anafundisha yeye ameangalia ubaoni wanafunzi wengine wameangalia nyuma kama abiria wa treni useme huyo mwl yupo makini na kazi yake,askari polisi wanaamka alfajiri wanavaa sare za jeshi letu,wanachukua siraha za moto ,pikipiki wanaanza kuzunguka mitaani kukusanya pesa muda ukifika wanakabidhi shift kwa wenzao maisha yanazidi kusonga wananchi wengi wanajua ,mwema anajua na ninauhakika hata rais anajua.Mtindo ni huu hadi kwenye mahospitali manesi watumia lugha za askari magereza kuongea na wagojwa huku madaktari wakishindwa kutofautisha magojwa.Kiharali Mgaya alistahili kwenda kizuizini hakuna sababu za msingi wafanyakazi wa tz kutaka waongezewe mshahara,kwanza laiti Mgaya angelikuwa anajua vyama anavyo viongoza vilivyo jaa urasim asingaenda kujipendekeza kwa watu,vyama vimeshikiliwa na wadosi leo hii wengi tumedhulimiwa haki zetu kutokana na wanachama wa TUCTA kushilikiana na waajiri.Saa ya ukombozi ikikaribia hatutaona bwebwe kibao kama zao CCJ wala zao hao CHADEMA na oparesheni sangara.Tutakuwa tukishuhudia matendo kuliko maneno.'Mwakora waitu'
   
Loading...