Vitu 10 usivyovijua kuhusu 6 flying dragons

Krikichino

JF-Expert Member
Oct 5, 2019
523
1,000
Najua wengi mtakuwa mnaijua series hii hivi ni vitu 10 usivyovijua kuhusu series hii :

1. Kulingana na IMDB series hiyo ilitengenezwa kwa budget ya taktibani Won Bil 30 ambazo ni takribani Bil 60 za kitanzania. Yaani hii ni hasara waliyopata ATCL kabisa.

2. 6 Flying Dragons iliwakutanisha tena Yoo Ah In (YI BANG WON) na Shin Se Kyung (BOON YI) ambao mara ya kwanza walikutana kwenye series ya FASHION KING ya mwaka 2012.

3. Series inaitwa Six flying dragons ili kuwaenzi mashujaa sita walioleta mapinduzi kutoa utawala wa kimabavu wa Goryeo na kuleta utawala mpya wa Joseon. Mashujaa hao ni YI SEONGGYE, SAMBONG, YI BANG WON, YI BANG JI, BON YI na MOO HYUL.

4. Kwa kawaida series za kikorea huwa na episodes 16 mpaka 20 lakini kwa six flying dragons ilikuwa tofauti maana episodes zilienda hadi 50. Hii inamanisha series hii ilipendwa sana hivyo SBS haikuona hasara kuirefusha ili kukidhi matakwa ya watazamaji.

5. Kwa namna fulani Six flying Dragons inafanana na JUMONG kwa kuwa Jumong inaelezea jinsi ambavyo taifa la GOGURYEO lilivyoasisiwa huku hii Six flying dragons inaelezea jinsi taifa la JOSEON lilivyoasisiwa.

6. Huko Korea 6 Flying Dragons ilikuwa inaoneshwa Jumatatu na Jumanne, na kulingana na Nielsen Ratings inasema kiujumla series hii ilipata AUDIENCE SHARE ya 14.3% ikizishinda series nyingine kama GLAMOROUS TEMPTATION ya MBC pamoja na BABYSITTER ya KBS2zilizokuwa zinaruka muda mmoja na series hii.

7. Six flying dragons imepata jumla ya tuzo 17 na 24 nominations huko nchini Korea na kubwa kabisa ni ile aliyochukua SHIN SE KYUNG kama "Best Supporting Actress" kwenye SBS drama awards.

8. Script ya series hii Iliandikwa na KIM YOUNG HUN mwandishi bora wa series huko nchini South Korea ambaye amezaliwa mwaka 1966. Ukiachana na series pia aliandika script ya series ya JEWEL IN THE PALAACE 2003, GREAT QUEEEN SEONDEOK 2009, DEEP ROOTED TREE YA 2011 na ARTHDAL CHRONICLES YA 2019.

9. Moja ya vitu vilivyovutia watazamaji kwenye series hii ni ACTION. Sasa mtu aliyehusika kuongoza scenes zote za action ni jamaa anayeitwa KANG HYUNG MOOK ambaye ukiachana na series hii alishiriki kwenye drama ya 3 DAYS mwaka 2014.
Vitu vingi bado havijawekwa wazi kuhusiana na Director huyu ila kuna siku msishangae kuna siku nikatengeneza uzi kwa ajili yake maana alifanya kazi nzuri mno.

10. Ilibidi SBS iongeze muda wa matangazo au commercial break kwa sababu advertisers walikuwa ni wengi.

5e0ce2f6b468e1001d8851ef.jpg
six%2Bflying%2Bdragons%2Boffcial%2Bposter.jpg
45875(0).jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom