Vitisho vya Maalim Seif kuhusu uchaguzi visipuuzwe!

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,538
Vitisho vya kutokea machafuko Zanzibar wakati wa Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu vilivyotolewa na Maalim Seif Sharif Hamad hivi karibuni siyo vya kupuuzwa. Matamshi yake ya kwamba Tume ya Uchaguzi (ZEC) inaandikisha watoto na kuruhusu wafu kupiga kura Zanzibar ndiyo mwanzo wa uchochezi na kuanzisha vurugu na uvunjifu wa amani Zanzibar.

Ndiyo, mwanzo wa kueneza propaganda za kuhalalisha kushindwa kwake na kuwaaminisha wananchi kuwa ameshindwa kwa mizengwe. Katika siasa, mwanasiasa hasa wa upinzani hupenda kutumia mbinu dhaifu ya kuhalalisha kushindwa kwao.

Kwamba wasipotengeneza mazingira yatakayoonesha kwamba, kushindwa kwao kunasababishwa na CCM, vyombo vya dola au ZEC na siyo kwa maamuzi ya wananchi.Hii ina maana kwamba, endapo kiongozi aliyeshindwa akikubali kushindwa haraka, hana sababu tena ya kuendelea kushindana kwa sababu ameshindwa kihalali.

Sasa kinachofanyika kwa Maalim Seif ni kuwa kusambaza propaganda kwa kueneza dhana ya uongo kuwa mazingira ya kushindwa yameshaandaliwa mapema. Maalim Seif hafanyi hivyo kwa kukosea la hasha, ni kujenga dhana ya kudhulumiwa hata kama dhuluma haitakuwepo

Historia ya Maalim Seif, kumuhusu kutafuta madaraka Zanzibar kwa gharama yoyote ile inafahamika. Tangu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 hadi sasa Maalim amekuwa akigombea kiti cha rais bila mafanikio, na wakati wote hakosi malalamiko na hata kusababisha machafuko na migogoro.

Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000, Maalim Seif alibwagwa, viongozi wa CUF wakiongozwa na Maalim Seif walishupaa na walijenga hoja kwa wanachama wao wote ya kutoitambua serikali ya Rais Aman Abed Karume aliyeshinda uchaguzi, hasa kutomtambua yeye binafsi kama ni rais wao.

Hili ni jambo zito la kisiasa lililoendeleza chuki, uhasama na uhasimu, kwenye jamii ya Zanziba kati ya wanachama wa CCM na CUF. Palitokea mgogoro mkubwa Zanzibar.

Lakini penye wazee wenye busara hapakuharibika jambo. Juhudi za ndani ya nchi na zile za kutoka nje ya nchi za kutatua na kuumaliza mgogoro uliokuwa umeibuka zilianza mara moja. Hivyo tarehe 10, Oktoba 2001, Maalim Seif Sharif Hamad baada ya kubanwa alitia sahihi andiko la mwafaka ambao ungemaliza mgogoro huo kwa wakati ule.

Lakini mara tu baada ya kuweka sahihi, Maalim Seif huyu huyu, hakuonyesha dalili zozote za kuuheshimu na kuutii mwafaka pamoja na kwamba yeye ndiye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mwafaka ya vyama vya CCM na CUF, na wakati huo ni Katibu Mkuu wa chama cha CUF.

Pamoja na mwafaka kutoheshimiwa na Maalim Seif, juhudi za Rais Benjamin William Mkapa, na Aman Abeid Karume za kutafuta suluhisho la kumaliza mgogoro wa Zanzibar kati ya CCM na CUF hazikusimama.

Kamati teule ya wajumbe wa pande zote mbili ya kutafuta mwafaka iliendelea na kuhimizwa kufanya vikao vyake kwa lengo la kutafuta suluhisho, aidha vikao vilifanyika jijini Dar es Salaam au mjini Zanzibar. Lakini cha kushangaza sana kwenye kila kikao kilichokuwa kinafanyika upande mmoja uliokuwa ukiongozwa na Maalim Seif, kila kikao ulikuwa unakuja na agenda mpya, agenda ya kutambuliwa kushinda uchaguzi bila ushindi wa kura za Wzanzibar.

Hilo ndilo jambo hasa lilochelewesha mwafaka kutimizwa mapema.

Jambo la pili lililochelewesha mwafaka, ni kwa Maalim Seif na viongozi wa CUF kutumia njia ya kuvuta muda, wakifikiri kwamba kwa kadri siku zilivyokuwa zinasonga mbele ndivyo wao wangeweza kushawishi na kupata wafuasi wengi kisiwani Pemba na Unguja, na hivyo kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, wangeweza kushinda kwa kishindo kiti cha urais, na viti vingi vya Wawakilishi wa Bunge la Zanzibar.

Fikra zao hizo zilishindwa kupima na kuweza kuuelewa mwenendo mzima wa siasa kwa wakati hule, ni kwamba rais Benjamin Mkapa alikuwa anamaliza kipindi chake cha utawala wa miaka kumi. Jamhuri ya Muungano ilikuwa inafanya uchaguzi wa rais mpya wa awamu ya nne kuanzia 2005.

Hivyo chama cha CCM, kwa vyovyote vile kilihitaji kuendelea kutawala Jamhuri ya Muungano, na wakati huo serikali ya Zanzibar ilkuwa ikitawaliwa na CCM. Hivyo Chama cha CCM kilihitaji madaraka hayo kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Bila kujua jinsi ya kupanga hesabu, Maalim Seif aliwania tena kiti cha urais wa Zanzibar, na kwa mara nyingine ya tatu alibwagwa. Malalamiko ya kuibiwa kwa kura, kutokuwa na imani na Tume ya Uchaguzi ya ZEC, uchaguzi kutokuwa huru, na sababu nyingine nyingi za malalamiko ziliendelea kutawala maelezo lukuki yaliyotoka kinywani mwa Maalim Seif.

Hakuwa na haja tena ya kukaa kwenye vikao vya pamoja na CCM vya kuujadili mwafaka, alizira vikao.

Kuingia Ikulu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania rais Jakaya Mrisho Kikwete, akitokea Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akiwa na uzoefu mkubwa wa jinsi ya kusuluhisha migogoro mizito ya nchi jirani za Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya na kule Zimbabwe. Kikwete hakupenda kuendelea kuusikia mgogoro wa Zanzibar akiwa mtawala mkuu wa Jamhuri ya Muungano. Ilani ya chama cha CCM, iliyomwezesha kuchaguliwa na kuingia ikulu, ilieleza bayana suala la kuutatua na kuumaliza mgogoro wa Zanzibar.

Kikwete alianza kuushugulikia mgogoro wa Zanzibar kwa kutumia mbinu zote zilizokuwa mkononi za kidiplomasia, ustaarabu, uvumilivu, usikivu, ushawishi na utashi. Wakati akitumia muda wake mwingi kutafuta suluhisho la mgogoro, wakati huo pia na mwenendo wa siasa katika jamii duniani ukawa umezaa mfumo mpya wa utawala. Mfumo wa utawala wa serikali za mseto. Vyama pinzani na vyama tawala kukubaliana kushirikiana katika kutawala dola.

Mfumo huu mpya barani Afrika ulioanzishwa ndiyo uliweza kumaliza migogoro mingi katika nchi za Ruanda, Burundi, Zimbabwe na Kenya. Nchi ambazo zilifika hatua mbaya za jamii kuuana na kumwaga damu nyingi ya wao kwa wao wakigombea madaraka. Nchi hizi zimetulia na wananchi wake wanajishugulisha kuendeleza mipango ya maendeleo badala ya kupambana, kasoro ni nchini Burundi.

Wakati haya yote yalipokuwa yanatendeka Maalim Seif alikuwa anayaona na anayasikia. Lakini alikuwa anashikwa na kigugumizi cha ni jinsi gani yeye kuweza kuwaeleza wafuasi wake wa CUF kuitambua CCM na watawala wake. Hakutaka kumeza matamshi yake ya kutoitambua serikali ya rais Karume. Lakini wakati ulifika na ulimsuta na ikabidi akubali kuitambua sarikali ya rais Karume ili mgogoro umalizike. Wanachama wa CUF walikukubali na kushiriki kupiga kura ya maoni ya kuruhusu serikali ya mseto, hii ndiyo ilikuwa nguzo kuu ya kumaliza mgogoro wa Zanzibar.

Siyo hilo tu mara zote CUF kwenye chaguzi walikuwa wanapata viti vingi vya uwakilishi lakini hawakuruhusiwa na Katiba kushiriki kutawala dola. Kwa upande wake Maalim Seif, yeye tarehe 22, Oktoba 2010, mwaka huo alisheherekea kufikisha umri wa miaka 67, mwaka huu atakuwa na miaka 72, bila shaka amezeeka. Lakini kwake ile ngazi iliyokuwa imembeba mpaka kule kileleni na akadondoka nayo tangu mwaka 1987, katika kipindi chote cha miaka 23 hakuweza kuinyanyua ikampandishe tena kuelekea kileleni. Hivyo Maalim Seif, ilimbidi atafute njia rahisi mbadala ambayo ngazi yake ingeweza kumbeba hadi juu.

Kwa juhudi zake za kuumaliza mgogoro rais Kikwete alihakikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 mgombea wa CMM wa kiti cha urais serkali ya Zanzibar anatoka Pemba. Ilikuwa ni mara ya kwanza tangu mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964. Na mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya CUF Maalim Seif ni kutoka Pemba. Hadithi ya Zanzibar ilizidi kukolea pale Rais Dkt. Shein na Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif, wote wawili kutoka Pemba walipoapishwa kushiriki kushika dola ya .

Historia ya kushawishi jamii dhidi ya serikali iliyoko madarakani ndiyo jadi ya Maalim Seif, pamoja na kwamba Maalim anapewa kila kitu na Serkali ya Umoja wa Kitaifa-SUK, nay a Jamhuri ya Muungano yakiwemo makazi, ulinzi, usafiri, matibabu, mishahara, malupulupu, na kuongozwa na jeshi la polisi kwenye misafara yake, lakini yeye hataki kuona na kusikia maendeleo ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika mchakato wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungao Inayopendekezwa, msimamo wake Maalim Seif ni kufuta Jamhuri ya Muungano ya sasa na kuwa na Muungano wa mkataba. Maana yake ni kuvunja Muungano wa sasa na kurudisha Tanganyika na Zanzibar kila moja ikiwa inajitegemea kivyake. Hamad kama Makam wa Kwanza wa Rais amekuwa akipita kila pembe ya Zanzibar akihamasisha kila anayemsikiliza kuikataa Katiba Mpya Inayopendekezwa kwa kigezo kwamba mapendekezo hayana maslahi ya nchi ya Zanzibar.

Hivyo Maalim Seif Hamad anapoibuka na madai kwamba watoto na wafu wanaruhusiwa kupiga kura Zanzibar na kuonya kwamba uchaguzi wa Oktoba vurugu zitajirudia kama yeye hatashinda , watu makini na wenye busara hawawezi kupuuza maneno yake. Mara kadhaa ameamasisha vurugu na machafuko na wananchi wanapopambana na vyombo vya dola yeye anakuwa yuko mafichoni.

Inasikitisha mzee wa umri wa miaka 72 bado anataka madaraka kupitia njia za machafuko. Fikra zake ni za kubomoa badala ya kujenga, lakini wahenga walisema siyo wazee wote wana fikra za busara za kujenga.

Chanzo: Taifa Imara
 
Watanganyika wasakatonge ambao wanajipeleka huko zanzibar kutumikishwa kupiga kura watu wazuri wa zanzibar wasirudi wamalizeni maana huo ni ujinga,utumwa na watu hao ni sawa na maadui wa zanzibar wasirudi.
 
Ushukuru huyo anayesema mdomoni kuliko anayoyasemea moyoni. Maana ya moyoni no siri kuu ndani yake.
 
Maandishi meengi lakini hakuna hata facts, yamejaa hekaya na mawazo ya kujitungia.Hivi lini ulifanya uchunguzi na kubaini kwamba ayaongeayo Seif Shariff Hamad hayana ukweli?Unamjua yule mzee Moyo wa Zanzibar mliyemfukuza uanachama?Alikiri kutumwa na CCM Zanzibar akamshawishi Seif akubali matokeo japo alishinda na ndiyo siri ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar.
Siku nyingine ujitahidi kutafuta taarifa za kutosha juu ya mada unayopanga kuiwasilisha kabla ya kuitoa ktk vyombo vya habari.hii ni pumba tupu uliyokuja nayo.
 
Malimu sefu anatakiwa afanyiwe kazi kama yule mpinzani wa burudi wachochezi kama malimu siyo wa kuvumiliwa hata kidogo tuwatwange tu.
 
Vitisho vya kutokea machafuko Zanzibar wakati wa Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu vilivyotolewa na Maalim Seif Sharif Hamad hivi karibuni siyo vya kupuuzwa. Matamshi yake ya kwamba Tume ya Uchaguzi (ZEC) inaandikisha watoto na kuruhusu wafu kupiga kura Zanzibar ndiyo mwanzo wa uchochezi na kuanzisha vurugu na uvunjifu wa amani Zanzibar.

Ndiyo, mwanzo wa kueneza propaganda za kuhalalisha kushindwa kwake na kuwaaminisha wananchi kuwa ameshindwa kwa mizengwe. Katika siasa, mwanasiasa hasa wa upinzani hupenda kutumia mbinu dhaifu ya kuhalalisha kushindwa kwao.

Kwamba wasipotengeneza mazingira yatakayoonesha kwamba, kushindwa kwao kunasababishwa na CCM, vyombo vya dola au ZEC na siyo kwa maamuzi ya wananchi.Hii ina maana kwamba, endapo kiongozi aliyeshindwa akikubali kushindwa haraka, hana sababu tena ya kuendelea kushindana kwa sababu ameshindwa kihalali.

Sasa kinachofanyika kwa Maalim Seif ni kuwa kusambaza propaganda kwa kueneza dhana ya uongo kuwa mazingira ya kushindwa yameshaandaliwa mapema. Maalim Seif hafanyi hivyo kwa kukosea la hasha, ni kujenga dhana ya kudhulumiwa hata kama dhuluma haitakuwepo

Historia ya Maalim Seif, kumuhusu kutafuta madaraka Zanzibar kwa gharama yoyote ile inafahamika. Tangu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 hadi sasa Maalim amekuwa akigombea kiti cha rais bila mafanikio, na wakati wote hakosi malalamiko na hata kusababisha machafuko na migogoro.

Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000, Maalim Seif alibwagwa, viongozi wa CUF wakiongozwa na Maalim Seif walishupaa na walijenga hoja kwa wanachama wao wote ya kutoitambua serikali ya Rais Aman Abed Karume aliyeshinda uchaguzi, hasa kutomtambua yeye binafsi kama ni rais wao.

Hili ni jambo zito la kisiasa lililoendeleza chuki, uhasama na uhasimu, kwenye jamii ya Zanziba kati ya wanachama wa CCM na CUF. Palitokea mgogoro mkubwa Zanzibar.

Lakini penye wazee wenye busara hapakuharibika jambo. Juhudi za ndani ya nchi na zile za kutoka nje ya nchi za kutatua na kuumaliza mgogoro uliokuwa umeibuka zilianza mara moja. Hivyo tarehe 10, Oktoba 2001, Maalim Seif Sharif Hamad baada ya kubanwa alitia sahihi andiko la mwafaka ambao ungemaliza mgogoro huo kwa wakati ule.

Lakini mara tu baada ya kuweka sahihi, Maalim Seif huyu huyu, hakuonyesha dalili zozote za kuuheshimu na kuutii mwafaka pamoja na kwamba yeye ndiye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mwafaka ya vyama vya CCM na CUF, na wakati huo ni Katibu Mkuu wa chama cha CUF.

Pamoja na mwafaka kutoheshimiwa na Maalim Seif, juhudi za Rais Benjamin William Mkapa, na Aman Abeid Karume za kutafuta suluhisho la kumaliza mgogoro wa Zanzibar kati ya CCM na CUF hazikusimama.

Kamati teule ya wajumbe wa pande zote mbili ya kutafuta mwafaka iliendelea na kuhimizwa kufanya vikao vyake kwa lengo la kutafuta suluhisho, aidha vikao vilifanyika jijini Dar es Salaam au mjini Zanzibar. Lakini cha kushangaza sana kwenye kila kikao kilichokuwa kinafanyika upande mmoja uliokuwa ukiongozwa na Maalim Seif, kila kikao ulikuwa unakuja na agenda mpya, agenda ya kutambuliwa kushinda uchaguzi bila ushindi wa kura za Wzanzibar.

Hilo ndilo jambo hasa lilochelewesha mwafaka kutimizwa mapema.

Jambo la pili lililochelewesha mwafaka, ni kwa Maalim Seif na viongozi wa CUF kutumia njia ya kuvuta muda, wakifikiri kwamba kwa kadri siku zilivyokuwa zinasonga mbele ndivyo wao wangeweza kushawishi na kupata wafuasi wengi kisiwani Pemba na Unguja, na hivyo kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, wangeweza kushinda kwa kishindo kiti cha urais, na viti vingi vya Wawakilishi wa Bunge la Zanzibar.

Fikra zao hizo zilishindwa kupima na kuweza kuuelewa mwenendo mzima wa siasa kwa wakati hule, ni kwamba rais Benjamin Mkapa alikuwa anamaliza kipindi chake cha utawala wa miaka kumi. Jamhuri ya Muungano ilikuwa inafanya uchaguzi wa rais mpya wa awamu ya nne kuanzia 2005.

Hivyo chama cha CCM, kwa vyovyote vile kilihitaji kuendelea kutawala Jamhuri ya Muungano, na wakati huo serikali ya Zanzibar ilkuwa ikitawaliwa na CCM. Hivyo Chama cha CCM kilihitaji madaraka hayo kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Bila kujua jinsi ya kupanga hesabu, Maalim Seif aliwania tena kiti cha urais wa Zanzibar, na kwa mara nyingine ya tatu alibwagwa. Malalamiko ya kuibiwa kwa kura, kutokuwa na imani na Tume ya Uchaguzi ya ZEC, uchaguzi kutokuwa huru, na sababu nyingine nyingi za malalamiko ziliendelea kutawala maelezo lukuki yaliyotoka kinywani mwa Maalim Seif.

Hakuwa na haja tena ya kukaa kwenye vikao vya pamoja na CCM vya kuujadili mwafaka, alizira vikao.

Kuingia Ikulu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania rais Jakaya Mrisho Kikwete, akitokea Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akiwa na uzoefu mkubwa wa jinsi ya kusuluhisha migogoro mizito ya nchi jirani za Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya na kule Zimbabwe. Kikwete hakupenda kuendelea kuusikia mgogoro wa Zanzibar akiwa mtawala mkuu wa Jamhuri ya Muungano. Ilani ya chama cha CCM, iliyomwezesha kuchaguliwa na kuingia ikulu, ilieleza bayana suala la kuutatua na kuumaliza mgogoro wa Zanzibar.

Kikwete alianza kuushugulikia mgogoro wa Zanzibar kwa kutumia mbinu zote zilizokuwa mkononi za kidiplomasia, ustaarabu, uvumilivu, usikivu, ushawishi na utashi. Wakati akitumia muda wake mwingi kutafuta suluhisho la mgogoro, wakati huo pia na mwenendo wa siasa katika jamii duniani ukawa umezaa mfumo mpya wa utawala. Mfumo wa utawala wa serikali za mseto. Vyama pinzani na vyama tawala kukubaliana kushirikiana katika kutawala dola.

Mfumo huu mpya barani Afrika ulioanzishwa ndiyo uliweza kumaliza migogoro mingi katika nchi za Ruanda, Burundi, Zimbabwe na Kenya. Nchi ambazo zilifika hatua mbaya za jamii kuuana na kumwaga damu nyingi ya wao kwa wao wakigombea madaraka. Nchi hizi zimetulia na wananchi wake wanajishugulisha kuendeleza mipango ya maendeleo badala ya kupambana, kasoro ni nchini Burundi.

Wakati haya yote yalipokuwa yanatendeka Maalim Seif alikuwa anayaona na anayasikia. Lakini alikuwa anashikwa na kigugumizi cha ni jinsi gani yeye kuweza kuwaeleza wafuasi wake wa CUF kuitambua CCM na watawala wake. Hakutaka kumeza matamshi yake ya kutoitambua serikali ya rais Karume. Lakini wakati ulifika na ulimsuta na ikabidi akubali kuitambua sarikali ya rais Karume ili mgogoro umalizike. Wanachama wa CUF walikukubali na kushiriki kupiga kura ya maoni ya kuruhusu serikali ya mseto, hii ndiyo ilikuwa nguzo kuu ya kumaliza mgogoro wa Zanzibar.

Siyo hilo tu mara zote CUF kwenye chaguzi walikuwa wanapata viti vingi vya uwakilishi lakini hawakuruhusiwa na Katiba kushiriki kutawala dola. Kwa upande wake Maalim Seif, yeye tarehe 22, Oktoba 2010, mwaka huo alisheherekea kufikisha umri wa miaka 67, mwaka huu atakuwa na miaka 72, bila shaka amezeeka. Lakini kwake ile ngazi iliyokuwa imembeba mpaka kule kileleni na akadondoka nayo tangu mwaka 1987, katika kipindi chote cha miaka 23 hakuweza kuinyanyua ikampandishe tena kuelekea kileleni. Hivyo Maalim Seif, ilimbidi atafute njia rahisi mbadala ambayo ngazi yake ingeweza kumbeba hadi juu.

Kwa juhudi zake za kuumaliza mgogoro rais Kikwete alihakikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 mgombea wa CMM wa kiti cha urais serkali ya Zanzibar anatoka Pemba. Ilikuwa ni mara ya kwanza tangu mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964. Na mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya CUF Maalim Seif ni kutoka Pemba. Hadithi ya Zanzibar ilizidi kukolea pale Rais Dkt. Shein na Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif, wote wawili kutoka Pemba walipoapishwa kushiriki kushika dola ya .

Historia ya kushawishi jamii dhidi ya serikali iliyoko madarakani ndiyo jadi ya Maalim Seif, pamoja na kwamba Maalim anapewa kila kitu na Serkali ya Umoja wa Kitaifa-SUK, nay a Jamhuri ya Muungano yakiwemo makazi, ulinzi, usafiri, matibabu, mishahara, malupulupu, na kuongozwa na jeshi la polisi kwenye misafara yake, lakini yeye hataki kuona na kusikia maendeleo ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika mchakato wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungao Inayopendekezwa, msimamo wake Maalim Seif ni kufuta Jamhuri ya Muungano ya sasa na kuwa na Muungano wa mkataba. Maana yake ni kuvunja Muungano wa sasa na kurudisha Tanganyika na Zanzibar kila moja ikiwa inajitegemea kivyake. Hamad kama Makam wa Kwanza wa Rais amekuwa akipita kila pembe ya Zanzibar akihamasisha kila anayemsikiliza kuikataa Katiba Mpya Inayopendekezwa kwa kigezo kwamba mapendekezo hayana maslahi ya nchi ya Zanzibar.

Hivyo Maalim Seif Hamad anapoibuka na madai kwamba watoto na wafu wanaruhusiwa kupiga kura Zanzibar na kuonya kwamba uchaguzi wa Oktoba vurugu zitajirudia kama yeye hatashinda , watu makini na wenye busara hawawezi kupuuza maneno yake. Mara kadhaa ameamasisha vurugu na machafuko na wananchi wanapopambana na vyombo vya dola yeye anakuwa yuko mafichoni.

Inasikitisha mzee wa umri wa miaka 72 bado anataka madaraka kupitia njia za machafuko. Fikra zake ni za kubomoa badala ya kujenga, lakini wahenga walisema siyo wazee wote wana fikra za busara za kujenga.

Chanzo: taifa imara

Unaweza kuandika hata kurasa miatano!! lakini bado ukawa hujashughulika na hoja ya msingi.Hoja hapo ni wafu na watoto kupiga. kura! JE,WALIPIGA KURA AU HAWAKUPIGA?? Unaandika ----- mwiiingi usio maana!Watanzania ssiyo wajinga kias hicho.Jipange haibiwi mtu tena mwaka huu!
 
watanganyika wasakatonge ambao wanajipeleka huko zanzibar kutumikishwa kupiga kura watu wazuri wa zanzibar wasirudi wamalizeni maana huo ni ujinga,utumwa na watu hao ni sawa na maadui wa zanzibar wasirudi.

leta ushahidi acha porojo, kule kuna wabara ambao maisha yao yapo kule zaidi ya miaka 2o kwa sasa, mbona huku kuna wapemba wanajiandikisha huku na wanapiga kura huku, tuwafukuze? Hapana kwa kuwa maisha yao yapo huku kwa miaka mingi wanapaswa kujiaqndikisha huku na kupiga kura huku
sharifu hamadi anaweweseka tu
 
Mimi nadhani tuwe wakweli tu kwa hili.nani asiejuwa kuwa ushindi huo wanaosema ccm wamepata ni wa kupora.chaguzi zote zimekuwa zikitawaliwa na udanganyifu kuhakikisha ccm wanabaki madarakani.hata pale wanaposhindwa wanatumia nguvu kubaki madarakani.lakini uvumilivu una kikomo wacha tuangalie tena mara hii.ila kwa kushinda msijis8fie hamna uchaguzi ambao mumewahi shinda dhidi ya Maalim. Na kila mzanzibari anajua hilo mpaka wewe ambae umeandika hiyo makala yako
 
Mtunga mada,maalim hajakosea alipo sema zanzibar kwanza,hebu wewe kama wewe tuwekee data zote za hela inayopata na iliyopata zanzibar kwenye muungano huu.
 
Back
Top Bottom