Vitambulisho vya wamachinga zengwe limeanza

kandamatope

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2018
Posts
589
Reaction score
630
Namsikiliza hapa mkuu wa mkoa wa mbeya anaitwa Chalamila
Kupitia radio EFM Asubuhi hii anasema wao kama wakuu wa mikoa wamejiongeza hivi vitambulisho vya mh,Rais watapewa watu wenye sifa hizi ,,
!) wazalendo kwa Taifa lao
!!)wasio walopokaji na wale wanaopenda kutukana viongozi
!!!)hivi vitambulisho watapewa wale wenye sifa ya mauzo kwa siku elfu 11 hapa tayari Zengwe limeingia mh Rais hawa jamaa zako bado awajakuelewa biashara ya kuuza kwa siku elfu 11 labda biashara ya kuuza maji ya Kandoro na kutembeza karanga za kupima na kijiko
Lakini mama lishe mtaji wake kwa siku 200,000 mauzo ni laki tatu kwa hiyo mama lishe au baba lishe tayari sifa ya kupata hiki kitambulisho hana
Kabla zoezi alijaanza tayari naanza kuona ulasimu mapema kabisa
Mh Rais hawa jamaa zako tayari zoezi wameshaliferisha mapema tu

Aksanteni nimewasilisha,,,hoja mezani
 
Kama ni kweli...hawa wasaidizi wa ndugu Rais wanamhujumu, kwanini wao wasingetoa vya kwao? Viongozi wengine ni kichefuchefu
 
Hahaha zengwe gani, rais akiona vipi akaviandae mwenyewe atugaie mwenyewe tunaamini anaweza.
 
Rais alikuwa very precise, alitaja sifa zote za hao wafanyabiashara, sikusikia akiwabagua kama huyo RC anavyofanya, asipokuwa makini pombe yote ataitia maji na haitanyweka.
 
Hesabu zao wamekokotoa hivi wasomi wetu wa kodi
11,000 ×30 ==330,000×12 =3,960,000
hizi ndio hesabu zao
Wataalamu wa kodi ebu tupeni ufafanuzi
Mh Rais alikusudia mauzo kwa siku 11 au thamani ya biashara yako au mtaji wako chini ya million 4 upewe kitambulisho
Mtu mwenye mtaji wa million 3,999,999
Mauzo yake kwa siku hayawezi kuwa elfu 11 ,,
Mimi labda ndio sijui ebu wataalamu nipeni faida...
 
Raisi Mwenyewe ndo alizingua kwenye hotuba Jana.

Aliposema
"Wajasiliamali wenye mtaji chini ya million 4 wasisumbuliwe"

Nkajua kua Tayar RAIA washalishwa tango poli.[emoji41]
 
Raisi Mwenyewe ndo alizingua kwenye hotuba Jana.

Aliposema
"Wajasiliamali wenye mtaji chini ya million 4 wasisumbuliwe"

Nkajua kua Tayar RAIA washalishwa tango poli.[emoji41]
Na mie ni mmoja wapo
Nimerishwa tango pori nipo njia panda
 
Kama ni kweli...hawa wasaidizi wa ndugu Rais wanamhujumu, kwanini wao wasingetoa vya kwao? Viongozi wengine ni kichefuchefu
Hawamuujumu. Jna ilkuwa maigzo. Ila maelkezo wanayo nyuma ya pazia.

Magfuli mjanja sasa. Kwanza jna alkuwa anajisafisha kmjuu ya usumbufu wa TRA ila ukweli ni kuwa walkuwa wakifta maagzo yake.
 
Na mie ni mmoja wapo
Nimerishwa tango pori nipo njia panda
Nna wasiwasi na uelewa wake juu ya hii mifumo na utaratibu mzima wa utozaji wa kodi.

Na sijui kwanini wasaidizi wake hawakumrekebisha,

Mwanzoni nkidhani kapitiwa, Baada ya mda nkaona anarudia Yale Yale.

Nkajua kua mzee baba yuko serious na anachoongea.

SAHIVI KESHAZUA MTAFARUKU kati ya machinga na watoa vitambulisho.
 
Kwanza vitamburisho kasema vinatolewa bure, lakini wakuu wa mikoa wameambiwa wauze 20,000 kila ID moja.....
 
Ukiongelea mtaji wa chini ya million 4,

Watu wengi hata wenye viduka MTAANI hawatolipa kodi.

Maana viduka vingi vya MTAANI hawana mtaji wa mil 4 ila still kodi&leseni wanalipa.

Kuna machinga wako K'koo pale barabara ya kuelekea buguruni jiran na China Plaza.

Wanauza flatscreens, Home theatre, Sabufa, Music mixer, Meza za vioo, makabati ya kichina.

Mtaji wa mil 10, ila wamemwaga mzigo barabarani

Na wao utawaona wako kwenye foleni ya kuchukua kitambulisho.
 
11000 kwa siku labda muuza pipi za hamsini hamsini
Rais alimaanisha mtaji usiozidi ml 4
 
Hii na ile ya nahodha wa kivuko aliyepenyezewa chai kwenye tundu ambalo sauti haipiti vimenifungia mwaka. Next year nitajifunza Kiyunani, pengine nitaelewa malaika wakisema nami
 
11000 kwa siku labda muuza pipi za hamsini hamsini
Rais alimaanisha mtaji usiozidi ml 4
Prezdaa aliwalisha RAIA tango poli mkuu.

Tra wanakadiria mauzo yasiozidi million 4 kwa mwaka.

Na sio mtaji usiozidi million 4.
 
Ngoja tusubiri na wakwetu atasemaje! Mi nipo hapa mjili nasubiri bogi likatike nipange
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…