Vitambulisho vimeokotwa Gairo

Wakati anafungua account ya benki ya posta alikuwa mrembo huyoo. Ila waweza mgugo ukapata taarifa ambazo zinaweza kurahisishia kumpata.

Itakuwa aliibiwa pochi masikini.... pole kwake.
 
AISEEE KAMA NI MKE WA MTU NA AMEPOTEZA MKOBA KWENYE HARAKATI ZA KUCHEPUKA KAISHA.
Ukute kaaga anakwenda Mtwara vitambulisho vimeokotwa gairo

Wala sio issue, mwizi anaiba Mtwara anaenda kuuza mali za wizi Gairo kisha anaenda kutumbua Dar. Yote hiyo kufuta ushahidi asitafutwe kirahisi.

Nilishawahi kuibiwa mkoba wangu ulikuwa na vitu kibao ikiwemo fedha na simu aina ya blackberry na iPhone. BlackBerry wakifanikiwa kuitumia maana sikuwa nimeweka lock incase ikiibiwa. Ile iPhone watakuwa waliuza spare au waliitupa maana kila waliyemuuzia akiwasha ilikuwa ina pop up message kwenye screen hii simu ni ya Kasinde piga namba hii 0730 683065 umrudishie na inapiga alarm hadi uzime. Kiufupi kila aliyeuziwa kwa kubambikiziwa akiiwasha ananipigia simu namwambia nirudishie hiyo simu nimeibiwa wanakimbia wa mwisho alinipigia yuko Tanga na simu iliibiwa Daslamu.

Tangu hapo sijanunua tena iPhone.
 
AISEEE KAMA NI MKE WA MTU NA AMEPOTEZA MKOBA KWENYE HARAKATI ZA KUCHEPUKA KAISHA.
Ukute kaaga anakwenda Mtwara vitambulisho vimeokotwa gairo
Mbona unatanguliza lawama baadala ya kutoa msaada kwanza,
We ungejisikiaje ingelikuwa ni mkeo kapoteza Kadi zote hizo,
Alafu atokee mtu mwenye ufikili wa chekechea kama wako
Aanze kutuhumu kuwa ni mchepuko?
 
Wakati anafungua account ya benki ya posta alikuwa mrembo huyoo. Ila waweza mgugo ukapata taarifa ambazo zinaweza kurahisishia kumpata.

Itakuwa aliibiwa pochi masikini.... pole kwake.
Dah maskini na wakati wa kupiga picha ya kitambuli cha kura alikuwa amechoooka, nadhani aliwekwa matumaini makubwa kwa Rais ajaye
 

kama wamfahamu mhusika,wasiliana kwa namba +255713563655
Ndugu msamalia Mwema, nakuombea uwe na moyo huwo daima
Pia jaribu kupita tawi la bank ya postal
lililo karibu nawe unaweza kupata mawasiliano ya huyo mteja wao
Pia kama hutajali pitia kituo cha polisi karibu na eneo ulilookota hizo kadi
Ulipoti kuhusu kuokotwa kwa vitambulisho ivyo.
Nakutakia Cku njema
 
KWENYE HIYO KADI YA MATIBABU YA AAR INAONYESHA NI MFANYAKAZI WA ATLASCOPO, HAO JAMAA WANABRANCH DAR ES SALAAM NA MWANZA PIA WANA OPERATION PALE BUZWAGI SHINYANGA.. KAMA UNA NIA YA KUMSAIDIA TAARIFA ZINATOSHA KABISA HIZO KAMA UNA NIA YA KUMSAIDIA...
 
Hivi mavitambulisho yote hayo unayajaza vipi kwenye mkoba mmoja?

Kuchagua ni kupanga....
Mko wachache sana mnatenganisha utembee na kadi hii uache ile, na hivi ulimwengu wa kadi ndo unaingia huku dunia ya tatu.... wengine tunaona ufahari kila ukifungua pochi badala ya pesa ni kadi tuu zinakutazama na muda wowote unapata huduma bila kuwa na pesa taslim. Labda ndo ushamba wenyewe maana nami ni mmoja wapo heheheheh
 
KWENYE HIYO KADI YA MATIBABU YA AAR INAONYESHA NI MFANYAKAZI WA ATLASCOPO, HAO JAMAA WANABRANCH DAR ES SALAAM NA MWANZA PIA WANA OPERATION PALE BUZWAGI SHINYANGA.. KAMA UNA NIA YA KUMSAIDIA TAARIFA ZINATOSHA KABISA HIZO KAMA UNA NIA YA KUMSAIDIA...
Raia naona mnanikomalia mara niende polisi mara benki mara kazini kwake,me nlikuwa nazurura zangu huko facebook kwa mamburula,ghafla nkakutana na tangazo serious ambalo ni hili nkaona ni vema nikalihamishia huku,itakuwa rahisi zaidi kumpata mhusika kuliko kule,na hyo namba ya simu ni ya huyo mtu alieokota wala sio yangu.
 
Mbona sura yake inabadilikabadilika kwa kila kitambulisho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…