GE2025 Vitali Maembe aachana na siasa

GE2025 Vitali Maembe aachana na siasa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,286
Reaction score
10,831
TAARIFA YA KUJIUZULU KUTOKA SIASA ZA VYAMA
Tarehe 20 Julai 2025, nilimuandikia barua Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ndugu Ado Shaibu, nikieleza rasmi uamuzi wangu wa kujiuzulu siasa za vyama, nafasi yangu ya Uenyekiti wa Jimbo, na uanachama wangu wa chama. Katika barua hiyo nilitoa pia sababu zilizonisukuma kufikia hatua hiyo.

Leo nimeona ni wajibu wangu kushirikisha umma kuhusu uamuzi huu. Mbali na kushiriki kwenye siasa, mimi ni msanii na mwanamuziki wa umma, hivyo nina jukumu la kuwa wazi kwa jamii inayonisikiliza na kunielewa kupitia kazi zangu.

Barua niliyomwandikia Katibu Mkuu na Katibu wa Jimbo la Bagamoyo ilikuwa mawasiliano ya ndani kati yangu na chama, hivyo siwezi kuiachia hadharani. Iwapo chama kitaona ni sahihi kuitoa kwa umma, sina pingamizi. Mimi ni mwanachama tu, na hata katika nafasi ya Uenyekiti wa Jimbo, siwezi kuwa mkubwa kuliko chama chenyewe.

Nina heshima kubwa kwa falsafa ya ACT-Wazalendo: “Taifa Kwanza, leo na kesho” na “Taifa la wote, maslahi kwa wote.” Hili ndilo chama cha kwanza nilichojiunga nacho, na nilishawahi kukiwakilisha katika chaguzi za Udiwani na Ubunge.

Kupitia ushiriki wangu kwenye siasa za vyama nimejifunza mambo mazuri na magumu pia. Silaumu mtu yeyote, wala sijutii kushiriki kwangu, kwa sababu nimejifunza mambo muhimu ambayo nisingeweza kuyapata nje ya safari hiyo. Ili vyama viwe kweli vyombo vya ukombozi wa wananchi, wanachama wake wanapaswa kuweka juhudi kuhakikisha havigeuki kuwa uwanja wa maslahi binafsi, hila na tamaa ya madaraka.

Kwa msingi huo, nimeamua kuachana na siasa za vyama na kuendeleza mapambano kupitia muziki, sanaa na harakati huru ambapo wananchi hunisikia na kunielewa moja kwa moja, bila taswira za kisiasa.

Nachukua nafasi hii pia kuutangazia umma kuwa sitashiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kama mgombea, mhamasishaji wala mpiga kampeni. Uamuzi huu unatokana na ukweli kwamba uchaguzi huu hauna dalili za kuwa huru na wa haki. Vilevile, bado sina imani na Msajili wa sasa wa Vyama vya Siasa pamoja na ofisi yake.
Ninabaki kuwa muumini thabiti wa dai la Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi.

Nitaendelea kulipigania jambo hili kupitia muziki na sanaa yangu, kama nilivyofanya kwa miaka yote iliyopita.
Kujiuzulu kwangu haina maana ya kuacha mapambano ya haki, uhuru na heshima ya mwanadamu. Kinyume chake, naamini sasa nitakuwa na nafasi pana zaidi ya kupigania haki za watu nikiwa huru na mwepesi moyoni.

Naomba radhi kwa yeyote atakayehisi kukatishwa tamaa au kuumizwa na maamuzi yangu, lakini ninaamini kila mmoja ataelewa kuwa uadilifu na uhuru wa dhamiri ni misingi nisiyoweza kuipuuza.

Vitali Maembe
Msanii, Mwanamuziki na Mwanaharakati wa Umma
Aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Jimbo la Bagamoyo
 
Kwa akili kubwa aliyonayo Maembe ilikuwa ni ngumu kukubaliana na uroho wa madaraka wa Zitto ambaye alikubali kuinajisi demokrasia kwa kuiuza ACT kwa ccm
 
Hii inakubalika. Baada ya kuona umepuuzwa na chama chako ukaona uandike public. Ungelikaa kimya tu ingelitosha
 
Back
Top Bottom