Vitabu vya Mtobwa

nameless girl

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Posts
4,195
Reaction score
2,685
Marlone alimtazama tena King na kutabasamu. “Yaani mara moja hii umesahau kuwa hangaika yetu yote hii ni kufanikisha dhamira yako ya kwenda Ikulu?” Alimwuliza baadaye, kwa sauti ndogo.

"Ikulu!" King alicheka kwa kebehi. "Nani aliyekupa ndoto kuwa nina njaa ya Ikulu kiasi cha kukubali kufungiwa namna hii? Nani aliyekudanganya kuwa nina kiu ya Ikulu kwa kiwango cha kuburuzwa kama gari bovu? Usijidanganye ndugu yangu. Mimi ni mtu mwenye msimamo wangu na hadhi yangu.”

“Ni hayo niliyokusudia tuzungumze keshokutwa. Maadam umeamua kufanya hivyo leo si vibaya. Nitaomba unisikilize kwa makini sana, kwani maongezi yetu ya leo ni mazito na yataibadili historia ya nchi yako."

King alitulia kumsikiliza.

“Kwanza kabisa nitapenda ufahamu kwa nini nililazimika kukutoa kasi nchini mwako” alisema huku kamkazia King macho. “Unakumbuka ulifanya nini usiku wa kuamkia safari yetu kule Ndege Beach?”

Moyo wa King ulipasuka kama tufe la barafu. “Ndege Beach… Usiku… Nilifanya nini? Nadhani sielewi unachosema.” Alijikongoja kutamka kwa sauti dhaifu ambayo ilimfanya Marlone aangue kicheko.

“Huelewi ninachosema, sio?” alimwuliza baadaye. “Ungeweza kumwambia hivyo Jaji wakati zipo picha za video zinavyoonyesha waziwazi jinsi ulivyomwua yule msichana mrembo, nani vile jina lake?”

“Msichana yupi?... unajua…”

“Sijui chochote. Ni wewe unayeyajua yote. Nilichotaka kukufahamisha hapa ni kuwa picha zipo na zinatosha kabisa kukufanya ule kitanzi.” Alisita kuacha kauli yake imwingie kikamilifu. Kisha aliendelea. "Kama unavyojua, urais, hasa katika nchi zinazoendelea kama yako sio mchezo. Tangu ulipoonyesha nia ya kugombea urais umekuwa ukifuatiliwa kwa makini na aina mbili za watu; wanaokutakia mema na wanaokutakia maovu. Vijana wangu ambao wana jukumu la kuangalia usalama wako, walishindwa kuzuia picha za vitendo vyako zisichukuliwe. Lakini walifaulu kuuchukua mwili wa marehemu. Sasa hivi uko chini ya bahari ya Hindi, katika gunia lenye mawe mazito ambayo yataufanya usitokeza kamwe juu ya maji.”

King aliduwaa akiwa hajui la kusema.

“Nadhani ni habari njema kwako. Natumaini sasa utakunywa wiski yako kwa raha. Sivyo?”

“Una wazimu. Mimi sijaua mtu…”

Marlone alitabasamu. Tuachane na hayo. Ninayo habari njema zaidi kwako. Si umepata habari kuwa wagombea urais wote nchini mwako wiki ijayo watakuwa na mdahalo utakaofanyika katika hoteli ya Kilimanjaro?”

King alitikisa kichwa.

“Na kwamba tukio hilo litatangazwa moja kwa moja na televisheni na redio na kuhudhuriwa na waalikwa mbalimbali?”

"Ndiyo,"

"Mdahalo huo hautakuwepo." Marlone alisema na kuongeza. “Kwa mara ya kwanza dunia itashuhudia kitu ambacho haikupata kushuhudia. Wagombea wote watateketea mbele ya macho ya wageni waalikwa.”

Sasa King alikuwa na hakika kuwa anazungumza na mwendawazimu.

“Kwa nini unanisimulia upumbavu wote huo?”

“Kwa sababu wewe ni mhusika mkuu. Wagombea wote watakufa kwa amri na niaba yako. Na baada ya hapo wewe utarudi nchini ukiwa shujaa kwa jinsi utakavyotoa hotuba kalikali za kitendo hicho. Utanguruma katika vyombo vyote vya habari, ndani na nje, ukipalilia njia yako ya kupokelewa kama shujaa mara watakapoanza kuandikisha upya wagombea. Utatumia chama chenye nguvu, utatumia pesa na msaada tutakaokupa na kwenda zako Ikulu bila wasiwasi wowote.”.

King alimtazama mtu huyo kwa muda mrefu kabla hajamwambia taratibu, “Nadhani hujui unazungumza na nani. mimi ni Mtanzania. Nchi yangu ni masikini, lakini tunachojivunia ni amani. Kwa taarifa yako mimi nitakuwa mtu wa mwisho kuitia dosari amani hiyo kwa ajili ya tamaa ya cheo. Kama ulinitazama kwa mtazamo huo, sina budi kukupa pole.” Baada ya maelezo hayo King aliinuka na kuongeza, “Nadhani umefika wakati wa kupeana kwa heri ya kuonana.”

“Kaa chini.” Marlone alifoka.

“Samahani. Naondoka.”

“Kaa.” Alifoka tena. “Unajua kuwa una kesi ya mauaji inayokusubiri kwenu?”

King alitabasamu kwa kebehi. “Najua sana. Na najua kuwa wewe utatufaa zaidi kumpata mtu aliyemwua mpenzi wangu Lilian.”

“Keti! Bado nahitaji kuzungumza na wewe!”

King alipuuza na kujaribu kuondoka. King ni mtu mwenye uzito wa kutosha, lakini mwepesi. Hata hivyo si uzito au wepesi uliomsaidia. Sekunde moja alikuwa wima akielekea mlangoni. Sekunde ya pili alikuwa angani baada ya kuchotwa kwa staili ambayo hakuitegemea. Na kabla hajatua juu ya sakafu kama gunia, tayari alikuwa amechukua vipigo vitatu vya judo shingoni vilivyomfanya agugumie na kutapika damu.

Marlone, ambaye alisimama kando yake, mguu wake mmoja ukiwa umekikanyaga kichwa cha King, mikono yake ikiwa tayari kuongeza kipigo iwapo King angefurukuta, aliinama na kumwambia kwa sauti ndogo yenye hasira baridi, “Sikiliza kwa makini. Tangu sasa utafuata amri yangu na kutekeleza kila nitakalokuagiza. Sawa? Namtaka mtu wangu pale Ikulu. Naitaka nchi yangu...”

King hakuyasikiliza yote. Fahamu zilimtoka wakati Marlone akiendelea kufoka....



MPAKA SASA KUNA VITABU AINA 17 VYA MTOBWA AMBAVYO VINAPATIKANA.
1. SALAMU TOKA KUZIMU 10,000
2. ROHO YA PAKA 10,000
3. NAJISIKIA KUUA TENA 10,000
4. DIMBWI LA DAMU 10,000
5. SALAMU TOKA KUZIMU 10,000
6. MIKATABA YA KISHETANI 10,000
7. MALAIKA WA SHETANI 10,000
8. MIKONONI MWA NUNDA 10,000
9. NYUMA YA MAPAZIA 10,000
10. TUTARUDI NA ROHO ZETU 10,000
11. LAZIMA UFE JORAM 10,000
12. MTAMBO WA MAUTI 10,000
13. KIMBIA HELLENA 5,000
14. PESA ZAKO ZINANUKA 10,000
15. KIGUU NA NJIA 15,000
16. ZAWADI YA USHINDI 10,000
17. MHARIRI MSALABANI 6,000



VITABU HIVI VINAPATIKANA. KWA YEYOTE ANAYEHITAJI NITAFUTE KWA NAMBA 0763044459 AU 0712504985.

KARIBUNI SANA.
 
Mkuu naomba unisaidie maudhui ya hicho mhariri msalabani.
[/QUOTE]
Ni kitabu ambacho kina sehemu tatu. Sehemu ya kwanza changamoto iliyompata akiwa amefungua kampuni yake, sehemu ya pili ni historia yake na sehemu ya tatu ni baadhi ya maoni ya wapenzi wa riwaya zake.
Hii ni maisha halisi ya Mtobwa.
 
Mkuu naomba unisaidie maudhui ya hicho mhariri msalabani.
Ni kitabu ambacho kina sehemu tatu. Sehemu ya kwanza changamoto iliyompata akiwa amefungua kampuni yake, sehemu ya pili ni historia yake na sehemu ya tatu ni baadhi ya maoni ya wapenzi wa riwaya zake.
Hii ni maisha halisi ya Mtobwa.
[/QUOTE]
Hivi mkuu vitabu vyote vya Mtobwa, mbali na hicho ni vya kipelelezi? Hana vyenye maudhui mengine?

nameless girl
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…