Vitabu 60 nilivyovisoma mwaka 2025

Vitabu 60 nilivyovisoma mwaka 2025

Nimesoma hivi
Ego is the enemy
The 48 Laws of Power
List nzuri hyo ryan holiday huwa ana madini Sana kwenye kitabu chake chake the courage is calling ameelezea jinsi bill Clinton na jf Kennedy maraisi wa marekani walivyokuwa wana penda totozi na kuhatirisha usalama wa nchi maana kama jf Kennedy ilikuwa ana date na mwanamke wa Germany ambaye alikuwa shushu ila jamaa hakuelewa na wanasema ndio miongoni mwa sababu na kupata yaliyompata ni mwandishi mzuri sana pamoja na Robert green
 
Mbona naona pdf ndio rahisi mkuu any way ukisoma soft copy unasoma vingi zaidi kuliko kwenye hard copy
Pdf haina flowable text. Na inasumbua kuscroll kwenye simu na tablets. Kila ukizoom text nyingine inajificha. Epub inasomeka vizuri hata ukizoom mara 10 bado text yote unaiona.
 
Wewe nomba list ya vitabu vilivyochange maisha yako financelly badala ya kuwekeana list ndefu ya vitabu!
Habari za weekend wadau,
Waisilamu bwana yesu asifiwe wakristo asalam alaykum marry chrismass na happy new year to all of you.

Kila mwaka huwa naleta vitabu nilivyosoma na mwaka huu ndio nimesoma idadi kubwa kuliko kipindi chote tangia nianze kusoma kama ifuatavyo:-

1.Before you quit your Job by ROBERT T. KIYOSAKI

2.Why ‘’A’’ Students Works For ‘’C’’ Students by ROBERT T. KIYOSAKI

3.I Am Malala by MALALA YOUSAFZAI

4.The business of the 21-ST century by ROBERT T.
 
Vinasaidia sana mkuu,
mimi nilianza kusoma vitabu vya "RICH DAD POOR DAD" na "THINK AND GROW RICH" mwaka 2019 vilinisaidia mawazo ya kununua kiwanja na kujenga maana kuna sehemu ilikuwa najitolea nilikuwa naweka laki moja kila mwezi, au laki mbili inategemea sometimes mishe zinanyooka baada ya mwaka nikanunua kiwanja mjini daslama.

Kwasababu vitabu vingi vinaelezea utajiri unapatikana kidogo kidogo hakuna mafanikio au utajiri wa ghafla ndio maana sichezi kamari yoyote wala sibeti na hakuna kampuni duniani iliyoanzishwa na mtu aliyepata hela za kubet wengi tuna dhani tuna tatizo la fedha ila ukweli ni kwamba tuna tatizo la elimu ya fedha.

Ndio maana gwajima alisema ukiwapa watanzania wote kiwango sawa cha hela baada ya mwaka masikini atarudi kuwa masikini na tajiri atarudi kuwa tajiri kwasababu pesa ni mindset na watanzania wengi hatuna financial education.

Lakini pia kupitia vitabu nimejifunza kwamba kuna tofauti kati ya broke na poor ndio maana watu wanaopata hela kwenye ku bet au hela za urithi wanarudi tena kwenye umasikini baada ya muda kwasababu hawana elimu ya fedha ambayo inapatikana kwenye vitabu kitabu kama "psychology of money" kimeelezea scenario hyo.

Lakini vitabu vinaondoa stress na kupunguza mihemko na hasira ambazo ni mbaya sana kwa afya.

Hizo ni za kawaida bado ki science vitabu vinaongeza kumbukumbu na ufahamu kuna daktari mmoja huko marekani anaitwa Benjamin Carson alikuwa kilaza darasani yaani alikuwa wa mwisho ila baada ya mama yake kumwambia asome vitabu alibadilika na kuwa daktari wa kwanza wa neurosurgery iliyofanikiwa duniani, mama yake alikuwa anafanya usafi kwenye nyumba za matajiri akaona wanasoma sana vitabu maana alikuwa single maza akahamishia huo utaratibu kwa wanawe.

Yaani mimi nina ushuhuda na vitabu ni kama wale waumini wa mwamposa vile.

NB : huwezi jua Faida ya kusoma vitabu mpaka uwe msomaji
Dr. Benjamin carson namjua. Kitabu chake cha gifted hands nimekisoma. Kwenye serikali ya Trump ule muhula wa kwanza alikuaga waziri kama sikosei. Vipo vitabu vingi nimesoma mfano hicho cha rich dad poor dad, the richest man in babylon, no more mr. nice guy n.k ingawa vingi huwa sivimalizi mpaka mwisho.

Ambacho nimejifunza kwenye hivi vitabu ni kwamba havipo relevant na mazingira ya bongo kama sio afrika kwa ujumla. Pia vinachukua muda mrefu kuandaliwa mpaka kiandikwe, kichapwe, kiwekwe sokoni unakutana ni mwaka mzima kipindi ambacho maarifa yaliyoandikwa kwenye kitabu yanakua tayari ni outdated, mfano leo hii Mendez wakala wa cristiano ronaldo apate wazo la kuandika kitabu kuhusu maujanja ya soko la usajiri mpaka kitoke mwakani tayari mbinu zitakua zishabadilika sokoni

Suala la kuweka akiba na kudunduliza ununue kiwanja au kujenga sidhani kama ilo ni mpaka usome kitabu cha robert kiyosaki. Kuna watu wamejenga na hawajai kusoma hata kitabu kimoja
 
. Suala la kuweka akiba na kudunduliza ununue kiwanja au kujenga sidhani kama ilo ni mpaka usome kitabu cha robert kiyosaki
Hehehe mule kumezungumzwa nyumba kama asset na sio nyuma kama nyumba tu.
Kweli nimeamini
Kunatofauti kati ya
1. Kusoma Vs kuelewa
2. Kuelewa Vs kufanyia kazi ulichokielewa kulingana na mazingira yako.
 
Hehehe mule kumezungumzwa nyumba kama asset na sio nyuma kama nyumba tu.
Kweli nimeamini
Kunatofauti kati ya
1. Kusoma Vs kuelewa
2. Kuelewa Vs kufanyia kazi ulichokielewa kulingana na mazingira yako.
Sasa mzee baba inamaanisha wewe kwa kutumia common sense tu ujui kama nyumba ni asset. Kwamba ni mpaka robert kiyosaki akuandikie kitabu kukuambia hiyo ni asset.

Haujui kama gari la kutembelea ni liability? ni mpaka robert kayosaki akuandikie kitabu?

Haujui kama hauwezi kutajirika kwa kazi ya kuajiriwa, kuwa tajiri ni mpaka uwe mjasiliamali au mwekezaji? Kujua ilo ni mpaka kiyosaki akuandikie kitabu?
 
Pdf haina flowable text. Na inasumbua kuscroll kwenye simu na tablets. Kila ukizoom text nyingine inajificha. Epub inasomeka vizuri hata ukizoom mara 10 bado text yote unaiona.
Sawa mkuu kikubwa ni kuongeza elimu mkuu
 
Wewe nomba list ya vitabu vilivyochange maisha yako financelly badala ya kuwekeana list ndefu ya vitabu!
Mkuu tatizo wengi wanakuja kwa lengo la kupinga na mimi siwezi kumlazimisha mtu asome vitabu au nimwambie Faida za vitabu financial thats is a personal attack kikubwa kila mtu ashinde mechi anayeangalia movies siku nzima yuko sahihi anayecheza game siku nzima yuko sahihi anayeangalia udaku wa uncle t na juma lokole yuko sahihi mimi nimechagua kusoma vitabu kwa hyo tueleweshane kwa staha bila kejeli wala dharau mkuu.

Siwezi Acha kusoma vitabu maana ni addiction kama pombe na madawa ya kulevya vile alamsik
 
Sasa mzee baba inamaanisha wewe kwa kutumia common sense tu ujui kama nyumba ni asset. Kwamba ni mpaka robert kiyosaki akuandikie kitabu kukuambia hiyo ni asset.
Unategemea elimu au taarifa iyo umeipata ukiwa na umri gani. Rich dad poor dad nimesoma nikiwa sekondari, kwangu ilikua ni breathtaking info.
 
Dr. Benjamin carson namjua. Kitabu chake cha gifted hands nimekisoma. Kwenye serikali ya Trump ule muhula wa kwanza alikuaga waziri kama sikosei. Vipo vitabu vingi nimesoma mfano hicho cha rich dad poor dad, the richest man in babylon, no more mr. nice guy n.k ingawa vingi huwa sivimalizi mpaka mwisho.

Ambacho nimejifunza kwenye hivi vitabu ni kwamba havipo relevant na mazingira ya bongo kama sio afrika kwa ujumla. Pia vinachukua muda mrefu kuandaliwa mpaka kiandikwe, kichapwe, kiwekwe sokoni unakutana ni mwaka mzima kipindi ambacho maarifa yaliyoandikwa kwenye kitabu yanakua tayari ni outdated, mfano leo hii Mendez wakala wa cristiano ronaldo apate wazo la kuandika kitabu kuhusu maujanja ya soko la usajiri mpaka kitoke mwakani tayari mbinu zitakua zishabadilika sokoni

Suala la kuweka akiba na kudunduliza ununue kiwanja au kujenga sidhani kama ilo ni mpaka usome kitabu cha robert kiyosaki. Kuna watu wamejenga na hawajai kusoma hata kitabu kimoja
Inawezekana havija nisaidia sana financial ila mbona kwenye point yangu huko juu nimeeleza katika kitu kikubwa vitabu vinasaidia kwenye positive mindset watanzania wengi tuna kata tamaa haraka sana ndio maana tupo hivi tulivyo sijasema vitabu vinamfanya mtu awe tajiri ila mindset inakuwa sawa.

Ila kusema kwamba vitabu vingi vipo outdated sio kweli, kitabu cha atomic habits kimeelezea namna ya kuacha addiction kama ya simu kwa kutumia 5 minutes rule.

Soma kitabu cha "emotional intelligence " jinsi kilivyo elezea intelligence quetiont na emotional intelligence na jinsi vinavyoweza kumuathiri mtu kwenye kazi biashara na maisha ya kila siku.

Alamsik
 
Hehehe mule kumezungumzwa nyumba kama asset na sio nyuma kama nyumba tu.
Kweli nimeamini
Kunatofauti kati ya
1. Kusoma Vs kuelewa
2. Kuelewa Vs kufanyia kazi ulichokielewa kulingana na mazingira yako.
Ukisoma vitabu vya Robert kiyosaki huwezi ukabaki vile vile financial yule jamaa vitabu vyake viko real sio kama theory za vitabu vinginge jamaa kwenye financial education yupo vizuri.
 
Sasa mzee baba inamaanisha wewe kwa kutumia common sense tu ujui kama nyumba ni asset. Kwamba ni mpaka robert kiyosaki akuandikie kitabu kukuambia hiyo ni asset.

Haujui kama gari la kutembelea ni liability? ni mpaka robert kayosaki akuandikie kitabu?

Haujui kama hauwezi kutajirika kwa kazi ya kuajiriwa, kuwa tajiri ni mpaka uwe mjasiliamali au mwekezaji? Kujua ilo ni mpaka kiyosaki akuandikie kitabu?
Huwezi jua mkuu labda kama ndio fani yako mtu kama kasoma kitu tofauti ni ngumu lakini pia ukiachana na assets na liabilities pia kaongelea kuhusu bad dept and good dept mtu anakopa hela ananua gari analipaki kuanzia asubuh mpaka jioni halafu uwezo wa kulihudumia hana anaenda tena kukopa kwa watu that's financial mistake.
 
Chuo nimesoma economics and finance labda ndio maana sioni maajabu ya hicho kitabu cha rich dad poor dad.
 
Kitabu SEXUS SIRI ZA NGONO TAMU by Dr Dyaboli, Mojo.
 
Mkuu tatizo wengi wanakuja kwa lengo la kupinga na mimi siwezi kumlazimisha mtu asome vitabu au nimwambie Faida za vitabu financial thats is a personal attack kikubwa kila mtu ashinde mechi anayeangalia movies siku nzima yuko sahihi anayecheza game siku nzima yuko sahihi anayeangalia udaku wa uncle t na juma lokole yuko sahihi mimi nimechagua kusoma vitabu kwa hyo tueleweshane kwa staha bila kejeli wala dharau mkuu.

Siwezi Acha kusoma vitabu maana ni addiction kama pombe na madawa ya kulevya vile alamsik
ko mimi nimekuambia uache kusoma vitabu? Au nimekukejeli? Acha hizo mzee! We nipe nilichokuomba!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom