Vita ya ujirani wa mapenzi

Vita ya ujirani wa mapenzi

mwanzo wetu

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2014
Posts
1,587
Reaction score
466
Wakuu habari.

Naombeni ushauri ndugu zangu, mimi na familia fulani tuko marafiki wa muda mrefu, kuanzia baba wafamilia husika na vijana wa familia Hiyo tunaishi kama ndugu.

Kijana mmoja wa familia Hiyo ana mke na mke Huyo amefanikiwa kuzaa binti, Tatizo limeanzia hapa saaa, Huyo binti ametokea kunipenda na tuko katika mahusiano mpaka sasa, nafikiria kumuoa maana na mimi nampenda Sana.

Tatizo vijana wa familia hiyo tunafahamiana tabia za kuvusha vusha wadada sasa nawaza nikimuoa siitakuwa vita maana wananijua tabia zangu, au nawaza siwatanifanyia timbwili mpaka tuachane wakiona nimemuoa wakiamini mimi nitakuwa na msaliti mtoto wao, nilitamani kufuata taratibu ila nawaza sindio nitaharibu zaidi.

Naomba ushauri nifanyeje ndugu zangu.
 
Unataka kusema ukimuoa huyo binti utaendelea kuishi hapo!? muoe kaishi mbali hicho unachowaza hakiwezi kujitokeza.

Au katika hao unaowavusha Kuna unaye mpenda kuzidi huyo unayefikiria kumuoa?
 
Jaribu wakikataaa basi.

Ukisha oa lazima mashemeji wakuheshimu. Mengine yaliyopita hayawahusu
 
Unataka kusema ukimuoa huyo binti utaendelea kuishi hapo!? muoe kaishi mbali hicho unachowaza hakiwezi kujitokeza.

Au katika hao unaowavusha Kuna unaye mpenda kuzidi huyo unayefikiria kumuoa?
Apana sinazaidi,,, Kimsingi mimi siishi na familia hii ila shida nimewekeza mambo mengi eneo hili sasa nitaenda mbali aje kaka
 
Jaribu wakikataaa basi.

Ukisha oa lazima mashemeji wakuheshimu. Mengine yaliyopita hayawahusu
Maaana yake vijana wenzangu hawa ambao ni ma Rafiki siyo mashemeji nikimuoa watakuwa wakwe zangu duh maaana Huyu ni binti wa miongoni mwa vijana wa mzee Huyu.
 
Mpe mimba afu kwao kuwa karibu na mzee wake sio kaka zake utakuja kunishukuru badae
 
Unaogopa nini? Hawawezi kukataa kama ukiamua kwenda na mshenga kupeleka barua watakuona serious
 
Back
Top Bottom