Uchaguzi 2020 Vita ya Ubunge CCM Arusha, vigogo waanza kutembeza rushwa

nyamadoke75

Member
Apr 1, 2020
87
280
Vita ya ubunge katika jimbo la Arusha mjini ndani ya chàma tawala imezidi kunoga na kuchukua sura mpya mara baada ya kuibuka suala la na kutoana kafara huku baadhi ya wafuasi wa CCM wakitumika vibaya kutokana na njaa ya pesa .

Kada wa Chama cha Mapinduzi jijini Arusha, Lebora Petro Ndarivoy ambaye pia ni katibu wa ccm kata ya Themi ameingia kwenye kashifa mbaya baada ya kutajwa kuhongwa gari aina ya Suzuki lenye namba T600 BRR kutoka kwa kigogo mmoja aliyejipanga kuwania nafasi hiyo kwa lengo la kumrahisishia katika shughuli za kumwaga fitika kwa wajumbe wa CCM,kuwachafua baadhi ya wagombea wengine wanaowania nafasi ya ubunge.

Ndarvoy ambaye anadaiwa pia kuahidiwa nafasi ya Udiwani katika Kata ya Them amekubali kutolewa kafara ili kuwachafua wagombea wengine na kumfagilia kigogo huyo ambaye ameapa iwe mvua iwe jua lazima awe mbunge wa jimbo la Arusha mjini.

Kwa kuthibitisha hayo Ndarvoy hivi karibuni alitumika kuandaa kikao cha Makatibu ,Makatibu wenezi na wenyeviti wa ccm katika kata zote za jiji la Arusha kilichofanyika katika ofisi za ccm wilaya ya Arusha huku mada kuu ni kueleza mazuri yaliyofanywa na kigogo huyo jijini Arusha.

Pamoja na mambo mengine yaliyoongelewa katika kikao hicho mkakati mkubwa ilikuwa ni kumuunga mkoano Mrisho Gambo ,ambapo Ndarvoi aliibuka na kuanza kuelezea mazuri yaliyofanya na Mkuu huyo wa mkoa na kuwataka wajumbe kumuunga mkono

Hata hivyo mkakati huo ulipingwa vikali na baadhi ya wajumbe hao huku wakihoji mpango wa kuwapigia debe wagombea wakati muda bado.

Gambo anayetajwa kuwa mtaalamu wa mipango ya fitina tiyari ameanza mapema kujiweka sawa ikiwemo kuwarubuni baadhi ya viongozi wa ccm wilaya na Mkoa wawe upande wake kama alivyofanikiwa kuwaweka mfukoni viongozi hao akiwemo mwenyekiti wa ccm wilaya ,Joseph Masawe na mwenyekiti wa ccm Mkoa Zelothe Steven ambao amekuwa akiambatana nao kwenye kila ziara kwa madai kwamba wanafuatilia utekelezaji wa ilani yao.

Kutokana na hali ya siasa kuwa mbaya inayotishia kugawanyija kwa wanaccm Arusha,katibu wa ccm Taifa Bashuru Ally ameombwa kuingilia kati na kuchukua hatua ili kunusuru chama hicho kinachojipambanua kulinyakua jimbo hilo lililopo chini ya upinzani.

Wanaotajwa kuwania ubunge jimbo la Arusha ni pamoja na Kalisti Lazaro,Mrisho Gambo,Philemon Mollel,Thomas Munis,Edmund Ngemela ,Mustapha Panju ,Mosses Mwizalubi na wengine kubao.

IMG-20200527-WA0032.jpeg
IMG-20200527-WA0031.jpeg
 
Vita ya ubunge katika jimbo la Arusha mjini ndani ya chàma tawala imezidi kunoga na kuchukua sura mpya mara baada ya kuibuka suala la na kutoana kafara huku baadhi ya wafuasi wa CCM wakitumika vibaya kutokana na njaa ya pesa .

Kada wa Chama cha Mapinduzi jijini Arusha, Lebora Petro Ndarivoy ambaye pia ni katibu wa ccm kata ya Themi ameingia kwenye kashifa mbaya baada ya kutajwa kuhongwa gari aina ya Suzuki lenye namba T600 BRR kutoka kwa kigogo mmoja aliyejipanga kuwania nafasi hiyo kwa lengo la kumrahisishia katika shughuli za kumwaga fitika kwa wajumbe wa ccm ,kuwachafua baadhi ya wagombea wengine wanaowania nafasi ya ubunge.

Ndarvoy ambaye anadaiwa pia kuahidiwa nafasi ya Udiwani katika Kata ya Them amekubali kutolewa kafara ili kuwachafua wagombea wengine na kumfagilia kigogo huyo ambaye ameapa iwe mvua iwe jua lazima awe mbunge wa jimbo la Arusha mjini.

Kwa kuthibitisha hayo Ndarvoy hivi karibuni alitumika kuandaa kikao cha Makatibu ,Makatibu wenezi na wenyeviti wa ccm katika kata zote za jiji la Arusha kilichofanyika katika ofisi za ccm wilaya ya Arusha huku mada kuu ni kueleza mazuri yaliyofanywa na kigogo huyo jijini Arusha

Pamoja na mambo mengine yaliyoongelewa katika kikao hicho mkakati mkubwa ilikuwa ni kumuunga mkoano Mrisho Gambo ,ambapo Ndarvoi aliibuka na kuanza kuelezea mazuri yaliyofanya na Mkuu huyo wa mkoa na kuwataka wajumbe kumuunga mkono

Hata hivyo mkakati huo ulipingwa vikali na baadhi ya wajumbe hao huku wakihoji mpango wa kuwapigia debe wagombea wakati muda bado.

Gambo anayetajwa kuwa mtaalamu wa mipango ya fitina tiyari ameanza mapema kujiweka sawa ikiwemo kuwarubuni baadhi ya viongozi wa ccm wilaya na Mkoa wawe upande wake kama alivyofanikiwa kuwaweka mfukoni viongozi hao akiwemo mwenyekiti wa ccm wilaya ,Joseph Masawe na mwenyekiti wa ccm Mkoa Zelothe Steven ambao amekuwa akiambatana nao kwenye kila ziara kwa madai kwamba wanafuatilia utekelezaji wa ilani yao.

Kutokana na hali ya siasa kuwa mbaya inayotishia kugawanyija kwa wanaccm Arusha,katibu wa ccm Taifa Bashuru Ally ameombwa kuingilia kati na kuchukua hatua ili kunusuru chama hicho kinachojipambanua kulinyakua jimbo hilo lililopo chini ya upinzani.

Wanaotajwa kuwania ubunge jimbo la Arusha ni pamoja na Kalisti Lazaro,Mrisho Gambo,Philemon Mollel,Thomas Munis,Edmund Ngemela ,Mustapha Panju ,Mosses Mwizalubi na wengine kubao.

Ndarvoy ambaye anadaiwa pia kuahidiwa nafasi ya Udiwani katika Kata ya Them amekubali kutolewa kafara ili kuwachafua wagombea wengine na kumfagilia kigogo huyo ambaye ameapa iwe mvua iwe jua lazima awe mbunge wa jimbo la Arusha mjini.

Kwa kuthibitisha hayo Ndarvoy hivi karibuni alitumika kuandaa kikao cha Makatibu ,Makatibu wenezi na wenyeviti wa ccm katika kata zote za jiji la Arusha kilichofanyika katika ofisi za ccm wilaya ya Arusha huku mada kuu ni kueleza mazuri yaliyofanywa na kigogo huyo jijini Arusha

Pamoja na mambo mengine yaliyoongelewa katika kikao hicho mkakati mkubwa ilikuwa ni kumuunga mkoano Mrisho Gambo ,ambapo Ndarvoi aliibuka na kuanza kuelezea mazuri yaliyofanya na Mkuu huyo wa mkoa na kuwataka wajumbe kumuunga mkono

Hata hivyo mkakati huo ulipingwa vikali na baadhi ya wajumbe hao huku wakihoji mpango wa kuwapigia debe wagombea wakati muda bado.

Gambo anayetajwa kuwa mtaalamu wa mipango ya fitina tiyari ameanza mapema kujiweka sawa ikiwemo kuwarubuni baadhi ya viongozi wa ccm wilaya na Mkoa wawe upande wake kama alivyofanikiwa kuwaweka mfukoni viongozi hao akiwemo mwenyekiti wa ccm wilaya ,Joseph Masawe na mwenyekiti wa ccm Mkoa Zelothe Steven ambao amekuwa akiambatana nao kwenye kila ziara kwa madai kwamba wanafuatilia utekelezaji wa ilani yao.

Kutokana na hali ya siasa kuwa mbaya kwa wanaccm Arusha,katibu wa ccm Taifa Bashuru Ally ameombwa kuingilia kati na kuchukua hatua ili kunusuru chama hicho jipambanua kulinyakua jimbo hilo lililopo upinzani.

Wanaotajwa kuwania ubunge jimbo la Arusha ni pamoja na Kalisti Lazaro,Mrisho Gambo,Philemon Mollel,Thomas Munis,Edmund Ngemela ,Mustapha Panju ,Mosses Mwizalubi na wengine kubao.

View attachment 1460550View attachment 1460551
Jimbo la arusha linarejea ccm mwaka huu utake usitake mwambieni lema atafute kazi nyingine ya kufanya
 
Chadema gani ipo? Mkuu acha vituko basi

Mwenzio Mbowe amesoma upepo ameona October hapati mbunge ameamua kupita na Bilion nane awekeze kwenye biashara
Chadema haifutiki mmetumia silaha zote mpaka leo ipo ni aibu kwa chama babu kuhangaika na chama mtoto
 
Hayatuhusu watajuana wenyewe acha sisi tupambane na COVID 19 kwanza.
 
Mkuu usiendelee kuwa na mawazo mgando
.nenda Arusha ndio utapata picha halisi

Chadema watu wa Arusha hata hawataki kuisikia
Hahahahahaha ndoto za mchana izo, ccm tumeshawachokaga kitamboo, hata jiwe tutalichagua sio ccm. Komaeni na Kongwa ndio kunawafaa
 
Waafrika mnawaza uchawi tu jamii ya watu wanaowaza uchawi huwa maskini sana wa fikra chadema wanakuwa vigagula kila siku kuwaza uchawi tu
Anayewaza uchawi na anayeufanya daily,nani ni shetani!?
Kuna watu wanapenda uchawi kama CCM!? Ushahidi upo wa wazi wazi.
 
Back
Top Bottom