Vita ya miji ya Mbeya, Arusha na Mwanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita ya miji ya Mbeya, Arusha na Mwanza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fame, Dec 24, 2010.

 1. f

  fame Member

  #1
  Dec 24, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hi members! This is my first post and I hope will be given chance by MODs
  I request members to give out their views on three contested mayoral seats at the abovementioned cities and municipal. MAFIOSO style to elect their mayor at Mbeya forciing their members to go with their party's favourity but cry foul play at Mwanza in order to instruct the responsible minister to elect commission like Keenja and at the same time rob the mayor seat at Arusha...probably withhelding something like land plots at Burwack A-town and many malpractices on public funds. Angalia makala ya mwandishi hapa chini

  VITA YA UMEYA: Siri yafichuka  Paul Sarwatt, Arusha
  Disemba 22, 2010

  Ni kulinda fursa za miradi nyeti ya ulaji
  Ni vita kali Arusha, Mbeya, Mwanza
  NGUVU za ziada zinazotumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wakuu wa serikali kwa lengo la kung’ang’ania uongozi wa halmashauri za Mwanza, Arusha na Mbeya katika nafasi ya umeya, zinalenga kuficha ufisadi unaoweza kufichuka iwapo watachaguliwa mameya wapya wasioyumbishwa, Raia Mwema limeelezwa.
  Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), halmashauri nyingi nchini zimekuwa na rekodi chafu za ubadhirifu katika kipindi cha kwanza cha utawala wa Rais Jakaya Kikwete, na hali hii inatajwa kuzua hofu kwa wahusika.
  Kutokana na mazingira hayo inadaiwa kuwa katika baadhi ya halmashauri hizo, wakurugenzi wamelazimika kuingilia kati, baadhi yao wakitajwa kuwahi kushiriki kufanikisha miradi ya ufisadi ambayo sasa ipo hatarini kufichuliwa.
  Kutokana na mazingira hayo, juhudi na mbinu mbalimbali zimekuwa zikifanywa hata zilizo kinyume cha taratibu, kuzuia uwezekano wa kuchaguliwa kwa mameya wapya wenye misimamo dhidi ya ufisadi.
  Hata hivyo, gazeti hili limeelezwa kuwa katika baadhi ya maeneo wakurugenzi wamekuwa wakitishwa kwa kuambiwa kwamba wasipounga mkono mbinu za madiwani wa chama fulani, usalama wao kikazi utakuwa hatarini.
  Imedhihirika kwamba katika maeneo hayo, baadhi ya viongozi wa CCM, na hasa madiwani wake wamekuwa wakipigana ‘ kufa na kupona’ kubakisha meya ‘wao’ huku lawama zikitanda kuwa wanabomoa hadhi ya chama hicho mbele ya jamii kwa kuthibitisha uroho wa kung’ang’ania madaraka.
  Wakati lawama hizo zikitanda miongoni mwa wana-CCM kwenye halmashauri husika, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, ameliambia gazeti hili wiki hii kuwa makao makuu ya chama chake hayajatoa maelekezo yoyote kuhusu mbinu za kufikia uamuzi wa kumchagua meya.
  “Sisi kazi yetu ilikuwa kuteua majina na kuyawasilisha TAMISEMI na tumefanya hivyo. Suala la uchaguzi umeharibika au umekwenda vizuri ni la mkurugenzi wa halmashauri, siyo la kwetu,” alisema Makamba.
  Kutoka jijini Mwanza, gazeti hili limethibitishiwa kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ndiye anayepaswa kuamua kama Jiji hilo lichague meya au yeye ateue tume ya kuliongoza kama ilivyopata kutokea jijini Dar es Salaam.
  Habari zilizothibitishwa zinaeleza kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya madiwani wa halmashauri ya jiji hilo kushindwa kuchagua meya na naibu wake kutokana na kutokubaliana kulikojitokeza kuhusu taratibu za upigaji kura.
  Wakati madiwani wa CHADEMA ambao ni wengi wakitaka kupiga kura wakiwa wameketi kama inavyotokea bungeni, madiwani wa CCM walitaka kupiga kura kwa foleni kuelekea kwenye sanduku au eneo la upigaji.
  Kutokana na mvutano huo, kikao hicho cha uchaguzi kilivunjika, huku Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Wilson Kabwe, akiwa amekubaliana na utaratibu wa CCM. Madiwani wa CCM walikuwa wakiongozwa na aliyepata kuwa naibu meya na diwani wa muda mrefu wa kata ya Igogo, John Minja, kutetea msimamo wao, ambao ulipingwa na madiwani wa CHADEMA, wakiongozwa na Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje.
  CHADEMA walikuwa wakisisitiza kuwa hata bungeni wakati wa kuchagua spika na naibu wake na hata wakati wa kuthibitisha jina la Waziri Mkuu, wabunge walipiga kura wakiwa wamekaa na bado zikahesabiwa kuwa ni kura za siri na kwa hiyo, si lazima kufuata utaratibu wa CCM ndipo usiri wa kura uthibitishwe.
  Hata hivyo, imeelezwa kuwa malumbano juu ya utaratibu upi utumike katika kupiga kura yalitokana na kuwapo kwa hofu ya kuhujumiana, ikiaminika kuwa upande wa CHADEMA ulihofia kuwa iwapo zingepigwa kura za siri kwa utaratibu uliotangazwa na Mkurugenzi, CCM wangeweza kushinda ingawa wao, CHADEMA, ndio wengi.
  Kwa upande mwingine, CCM nao walihofia zingepigwa kura kwa utaratibu uliotakiwa na CHADEMA basi ilikuwa ni dhahiri kuwa wangepoteza nafasi zote za meya na naibu wake kwani CHADEMA wangedhibitiana ili kuhakikisha kuwa kila diwani wao anapiga kura kwa mgombea wao.
  CHADEMA ina jumla ya madiwani 15 pamoja na wabunge wawili hivyo kufanya idadi ya kura zao kuwa 17 wakati CCM ina madiwani 12 na mbunge mmoja wa Viti Maalum, Maria Hewa, hivyo kufanya kura zao kuwa 13.
  CUF kina diwani mmoja na mbunge mmoja wa viti maalumu ambao walikubaliana kuungana na CCM dhidi ya CHADEMA, ili diwani wa CCM kata ya Mkolani, Stanslaus Mabula achaguliwe meya na diwani wa CUF kata ya Pamba, Bhiku Kotecha, awe naibu meya.
  Hata hivyo, mkurugenzi wa jiji anatajwa kwamba ndiye aliyechangia kutofanyika kwa uchaguzi huo kutokana na kukosa msimamo. Inaelezwa kwamba mara ya kwanza alisisitiza utaratibu wa kwenda kupiga kura kwa diwani mmoja mmoja kwenye kisanduku lakini baada ya kubanwa na madiwani wa CHADEMA, akakubaliana kuwa wapige kura wakiwa wamekaa pale walipokuwa wamaketi. Lakini wakati kura zikikaribia kupigwa madiwani wa CCM walikuja juu kupinga utaratibu huo kwa madai kuwa sio wa siri, na kwa mara nyingine tena Kabwe akakubaliana nao.
  Hata hivyo, haikujulikana ni kwa nini Kabwe hakutoa fursa kwa madiwani hao kuamua utaratibu wa kutumia hata angalau kwa ya kunyoosha mikono, lakini badala yake akahitimisha kuwa madiwani walikuwa wameshindwa kutimiza wajibu wao, na akaripoti hivyo kwa Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
  Akizungumza na Raia Mwema wiki hii Kabwe alisema kuwa tayari amepeleka barua kwa waziri mwenye dhamana ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na anatarajia kuwa baada ya madiwani kushindwa kuchagua meya na naibu wake pamoja na wenyeviti na wajumbe wa kamati za kudumu za halmashauri waziri ataunda tume kuongoza jiji la Mwanza.
  Kutoka Arusha, inaripotiwa kwamba hali ni tete zaidi. Kilichotokea Ivory Coast kwa nafasi ya Rais, ndicho kilichotokea Arusha kati ya CHADEMA na CCM. Diwani wa CCM, Gaudance Lyimo alichaguliwa meya na diwani wa TLP, Michael Kivuyo, alichaguliwa naibu meya, lakini CHADEMA ikamtangaza diwani wake, Estomih Mallah, kuwa ndiye meya.
  Hata hivyo, “uchaguzi” huo wa CCM na wa CHADEMA haujakidhi matakwa ya kikanuni, kwa maana ya ula kuwa ya upigaji kura unaowahusisha angalau theluthi mbili ya madiwani wote.
  Kutoka Mbeya, inaripotiwa kwamba hali ni tete pia, ingawa huko meya na naibu wake wamekwisha kupatikana. Athanas Kapunga wa CCM ndiye aliyechaguliwa meya na Frank Mayemba, pia wa CCM, naibu meya.
  Katika uchaguzi huo mbinu zinazodaiwa kukandamiza demokrasia zilitumika ili kuhakikisha CCM kinashinda, hasa baada ya kuwapo kwa taarifa kuwa kuna madiwani 10 wa chama hicho walikuwa tayari kuungana kumchagua meya kutoka kambi ya CHADEMA.
   
Loading...