Vita ya Marekani na Mashariki ya Kati

Elly official

JF-Expert Member
Sep 16, 2018
464
1,000
JENERALI QASSEM SOLEIMANI MWIBA AMBAO UMEMKWAMA KOONI TRUMP

Bado sijaamini ni ujinga wa kiwango gani uliomsukuma Rais Donald Trump wa Marekani kupitisha chaguo la kumuua kigaidi Meja Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC akiwa pamoja na Naibu Mkuu wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi wa Iraq ya Hashdu sh-Sha’abi, Abu Mahdi al Muhandes katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mjini Baghdad, Iraq usiku wa Ijumaa iliyopita.

Taarifa za awali zinaeleza kwamba Trump akiwa jimboni Florida, alifuatwa na Mike Pompeo, Waziri wake wa Mambo ya Nje na Mark Esper, Waziri wake wa Ulinzi, ambao walimfikishia machaguo kadhaa kumuhusu Jenerali Qassem Soleimani.

Inasemekana baada ya kumpa mapendekezo kadhaa, Trump ghafla akapitisha chaguo la kumuua jenerali huyo, licha ya kwamba walikuwa wamemuonya kutokana na hatma mbaya ya uamuzi wake huo.
Baada ya hapo kulitolewa agizo kwenda kwa askari wa Marekani walioko nchini Iraq la kumuua baada tu ya kushuka ndege uwanjani hapo.

KWA NINI TRUMP ALIPITISHA CHAGUO LA MAUAJI?

Ifahamike kwamba hivi sasa Trump ndiye rais pekee ambaye yupo madarakani ndani ya Marekani si kwa kura za wananchi bali kwa kura za maseneta. Hii ikiwa na maana kwamba licha ya mamilioni ya raia wa Marekani kupanga foleni ndefu mwaka 2016 ili kumchagua rais, lakini kura zao zilipuuzwa kisha akatangazwa yeye licha ya kwamba mshindani wake Hillary Clinton alikuwa amemzidi Trump kwa zaidi ya kura milioni tatu.

Hapo ndio utajua hata neno ‘Demokrasia’ linalotamkwa sana na Washington na kuzikosoa nchi nyingine, ni uongo mtupu, na Marekani ndio nchi ambayo haina demokrasia duniani. Lakini mbali na hayo Trump ndiye rais wa Marekani anayeandamwa na kashfa na matatizo lukuki ndani na nje ya Marekani, kama ambavyo ndiye rais ambaye hajafanikiwa hata jambo moja tangu alipoingia madarakani na kila kitu anachokifanya kinamwendea mrama.

Upande wa ndani taarifa za kiuchunguzi zinathibitisha kwamba amefeli kubuni nafasi za kazi na badala yake maelfu ya fursa za kazi zinazidi kutoweka huku umasikini ukishika kasi jambo ambalo limekuwa chanzo cha kupanda kiwango cha mauaji ya silaha za moto (bunduki) nchini humo. Aidha Trump anakabiliwa na kadhia ya kusailiwa na Bunge la Seneti ambapo iwapo mambo yatamuendea kombo, basi atauzuliwa kwenye urais. Kwa upande wa nje Trump amefeli kuanzia Venezuela, Korea Kaskazini, Mashariki ya Kati kwa ujumla na hapa nikimaanisha Iran, Iraq, Syria, Yemen, Lebanon nk.

Hii ni kwa kuwa baada ya kuiondoa nchi yake kwenye mapatano ya nyuklia na Iran mwezi Mei 2018, Trump aliamini kwamba atailazimisha Iran ikubaliane na matakwa mapya ya Washington kupitia vikwazo vikali alivyoiwekea Tehran, Lakini hadi leo hajaambulia kitu na kinyume chake Iran imezidi kusonga mbele zaidi. Sasa Iran inazidi kupendwa na kukubalika katika nchi zote za eneo la Mashariki ya Kati kinyume kabisa na ilivyodhaniwa kuwa baada ya kuzikataza nchi zote za dunia kufanya mahusiano na Iran, Tehran ingetengwa kimataifa, lakini hali imekuwa ndivyo sivyo.

Katika mazingira hayo Trump aliamini kwamba kwa kumuua Meja Jenerali Qassem Soleimani, ingemsaidia kusafisha jina lake angalau aweze kuungwa mkono nchini Marekani.

JENERALI SOLEIMANI AGEUKA MWIBA ULIOMKWAMA TRUMP

Hata hivyo na licha ya Washington kueneza propaganda kwa kiwango cha juu kwamba Jenerai Soleimani eti alikuwa ni gaidi nk, lakini Wamarekani na dunia kwa ujumla imekataa porojo hiyo na sasa watu wote duniani wameamka na kutangaza wazi kumuunga mkono jenerali huyo. Sasa maandamano duniani kote hadi ndani ya Marekani kwenyewe yanafanyika kumlaani Trump na serikali yake yote huku walimwengu wakitangaza wazi kwamba nao wanachagua njia ya Qassem Soleimani.

Kitu ambacho hakikudhaniwa ni kwamba suala la mauaji ya Meja Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al Muhandes lingepita kirahisi na lingemuongezea zaidi itibari Trump. Lakini ndio kwanza limeanza. Limeanza kwa kuwa Iran imeweka wazi msimamo wake kwamba italipa kisasi kikali kwa Marekani. Kama hiyo haitoshi Harakati ya Kujitolea ya Wananchi nchini Iraq, Hashdu sh-Sha’abi nayo imesema kuwa kamwe haitokubali hadi ilipize kisasi kikali kwa askari wa Marekani waliomo nchini Iraq.

Taarifa iliyotolewa leo na Msemaji wa Harakati hiyo imeweka wazi kuwa iwapo bunge la Iraq ambalo linakaa kikao cha dharura hivi sasa mjini Baghdad kujadili suala la kuwatimua askari wa Kimarekani nchini humo, litashindwa kupitisha sheria ya kuwatimua Wamarekani, basi yenyewe italipiza kisasi kikali na kuwatia adabu askari wa Marekani.

Mbali na hayo majenerali wengi wa kijeshi nchini Marekani wamemtahadharisha Trump kwamba hakuna kosa kubwa alilowahi kulitenda kama hili, kwa sababu askari wa Marekani walioko Afghanistan, Syria, Iraq, Qatar, Kuwait nk wote wako katika shabaha ya Wairaki na Wairan na kwamba ima iwaondoe au ijiweke tayari kuingia vitani na Iran. Na wakamsihi kwamba kuingia vitani na Iran ni ndoto ya mchana kweupe kwa kuwa Iran ni nchi yenye uwezo mkubwa sana.
Lakini huku hali ikiwa hivyo Trump na Pompeo wamechanganyikiwa na sasa wameanza kupiga simu nchi mbalimbali kuomba msaada angalau waungwe mkono, ingawa hata hivyo wamejikuta wametengwa na hii ni baada ya Umoja wa Ulaya, China na Russia kutangaza msimamo wake wa kutoiunga mkono katika kadhia hiyo. Sasa Washington imebakia yenyewe ikiwa na vibaraka wake wa Saudia, Imarati, lsrael, Bahrain na Misri. Jiulize je swali hili, kwamba je kati ya Marekani na lran nani aliyefeli na kupoteza?

Je Marekani anaweza kuingia vitani kwa sasa na lran ilhali nchi dhaifu sana ya Yemen imewashinda Marekani, Saudia, lmarati, lsrael, Misri nk? Je wataiweza lran?

Hebu tazama ukubwa wa nafasi aliyokuwa nayo Qassem Soleimani ambapo kila eneo duniani linamlilia kutokana na mchango wake alioutoa wa kuwaangamiza magaidi wa ISISI ambao walikuwa ni vibaraka wa Marekani.

Karibu kila nchi watu wamekuwa wakipeperusha picha zake na kuzipeleka kwenye balozi za lran au hata za Marekani na kuwasha mishumaa na kumuombea dua apumzike kwa amani huko alipo.

Hivi sasa kinachosubiriwa ni jibu kali lililoahidiwa na lran na harakati ya wananchi ya lraq.

Mungu endelea kufichua uovu wa Marekani na Mungu ibariki lran na nchi zote zinazopigania uhuru duniani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Jorojik

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
3,159
2,000
You are not credible to write this long wordy story while you are uninformed shithole person. Kaa kimya wakati mataifa zenye machineries za kutosha kitaifa na kimataifa zinapofanya maamuzi ya kimataifa. Wewe endelea kutetea mambo ya TACAIDS ili Prof Maboko aendelee kukumbuka na post zako za maambukizi mkoani Njombe. She.nzi kabisa.
 

pureView Zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
4,661
2,000
Bunge la Iraq jioni hii wamepitisha azimio la pamoja kuondoa vikosi vyote vya kigeni nchini mwao na pia katika azimio Lao wamepiga marufuku kutumika Kwa ardhi,maji na mipaka Yao isitumiwe na vikosi vya kigeni....
Kabla ya Hali mbaya haijatokea EU wamemwita waziri Mkuu wa Iran huko Brussels ili kutuliza vita...

Mungu aepushe mbali hii vita
 

kawoli

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
5,932
2,000
Kwahiyo Trump na washauri wake wabobevu kwenye midani ya ujasusi na Vita hawakuiona risk hii mpaka wewe uwatoe tongo tongo?
 

Atkins Mendel

JF-Expert Member
Feb 12, 2017
619
1,000
Bunge la Iraq jioni hii wamepitisha azimio la pamoja kuondoa vikosi vyote vya kigeni nchini mwao na pia katika azimio Lao wamepiga marufuku kutumika Kwa ardhi,maji na mipaka Yao isitumiwe na vikosi vya kigeni....
Kabla ya Hali mbaya haijatokea EU wamemwita waziri Mkuu wa Iran huko Brussels ili kutuliza vita...

Mungu aepushe mbali hii vita
Mye ningependa watu tujikite hapa, je nn impact ya hii sheria kwa marekani

Sent using Jamii Forums mobile app
 

niko said

Member
Dec 15, 2019
26
75
Bunge la Iraq jioni hii wamepitisha azimio la pamoja kuondoa vikosi vyote vya kigeni nchini mwao na pia katika azimio Lao wamepiga marufuku kutumika Kwa ardhi,maji na mipaka Yao isitumiwe na vikosi vya kigeni....
Kabla ya Hali mbaya haijatokea EU wamemwita waziri Mkuu wa Iran huko Brussels ili kutuliza vita...

Mungu aepushe mbali hii vita
Natamani lile combola ra urusi linalo kimbia zaidi ya sauti iran alitumie kulipiza kisasi lipige mji mmoja mkubwa huko Marekani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

MTOTO WA KUKU

JF-Expert Member
May 3, 2012
2,581
2,000
Acha kujifanya unajua kuliko marekani wenyewe.... Waliofanya maamuzi ya kumuua huyo gaidi wanajua kwanini wamemuua na hawana presha na wamekili wao ndo wamemuua...
 

MTOTO WA KUKU

JF-Expert Member
May 3, 2012
2,581
2,000
Marekani amezamilia kuiponda this time Iran wakijichanganya tu watafurahia shoo
Bunge la Iraq jioni hii wamepitisha azimio la pamoja kuondoa vikosi vyote vya kigeni nchini mwao na pia katika azimio Lao wamepiga marufuku kutumika Kwa ardhi,maji na mipaka Yao isitumiwe na vikosi vya kigeni....
Kabla ya Hali mbaya haijatokea EU wamemwita waziri Mkuu wa Iran huko Brussels ili kutuliza vita...

Mungu aepushe mbali hii vita

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom