kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,718
- 14,152
Kuyaondoa madawa kwenye jamii kabla ya kuwatambua na kuwasaidia waathirika wote wa dawa hizo ni sawa na kubandika tangazo la kifo kwa waathirika wa dawa hizo.
Watakufa kwa arosto kama wakizikosa dawa hizo ghafla. Ni vema tuanze kwa kuongeza vituo vya kuwasaidia walevi hawa nchini hadi kwenye ngazi ya kila wilaya na kata/ dispensary nchi nzima ili kuwahudumia waathirika watakaozikosa ghafla dawa hizo baada ya dawa hizi kuadimika mitaani, kwa sasa hivi vituo vya aina hii ni vichache sana kuliko idadi ya wagonjwa waliopo nchini.
Vita hii inataka maandalizi, kule ulaya na Marekakani huwa yanaachwa maduka/hospitali maalumu ambazo yanaruhusiwa kuendelea kuuza/kuwapatia madawa hayo waathirika sugu wakati na vituo vya methodon vikiwa vimeenea kila kona ili kuepuka kutenda kosa lingine wakati wa kutatua kosa la kwanza.