Vita ya Kificho ya Nape na Makonda sasa yafikia patamu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,216
Wakati Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akionyesha wazi wazi kuitumia Redio yenye ushawishi kwa Kundi kubwa la Wasikilizaji wake Clouds fm kufanikisha malengo na mikakati yake ya Kisiasa nchini nae Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye ameibuka na mkakati unaofanana na wa Makonda ambapo na yeye sasa ameamua wazi wazi kuonyesha mahaba yake makubwa kwa Redio inayochipukia kiushawishi jijini ya Efm.

Majabali hawa ambao sasa Uadui wao si wa kificho tena na ambao ulinogeshwa kwa kiasi kikubwa na mapambano ya Vita vya dawa za kulevya ambapo mmoja wao ( RC Makonda ) anasemekana aliamua kwa makusudi kuwataja Watu ambao walikuwa na maslahi makubwa na ya ukaribu kwa mwenzake ( Waziri Nnauye )

Kwa mara nyingi sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul Makonda amekuwa akionyesha wazi wazi si tu mapenzi yake bali mahaba yake kabisa kwa Kituo cha Redio cha Clouds fm kiasi cha hadi kuwaudhi na kuwakera Waandishi wa Habari wengine hali ambayo kimsingi imeratibiwa na ukaribu kati ya Makonda na Bosi Kiongozi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba ambaye inasemekana ndiyo think tank namba moja wa Ndugu Paul Makonda.

Baada ya kuona hali hii adui yake Waziri Nnauye nae aliamua kufanya kautafiti kidogo ili aweze kufanya counter kwa mwenzake ambapo aligundua kuwa kwa sasa Redio shindani kwa Clouds fm ni Efm na akaenda mbele zaidi kuifuatilia na kugundua kuwa endapo itapanuka basi Efm Radio itakuwa na ushawishi mkubwa Kwake na kufanikisha mambo yake.

Huko nyuma Makonda amekuwa akisika wazi wazi na hata kwa kificho akisema kuwa anaipenda mno Clouds fm kwakuwa inatetea maslahi makubwa ya Vijana ambao kimsingi ndiyo wengi na ambao Yeye anapambana kuwakomboa na hakuwahi kuficha mahaba yake kwa Bosi Ruge, Watangazaji wote wa Clouds fm na hasa hasa Mtangazaji Shafii Dauda.

Jana alipofanya ziara rasmi katika Kituo cha Redio cha Efm Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa Ndugu Nape Nnauye ambaye na yeye imejulikana kuwa kumbe ana ukaribu sana na Bosi Tajiri mwenyewe wa Efm Francis Ciza a.k.a Dj Majey au Majizo aliweza kutoa kauli ambazo kimsingi zimeweza kuwa ni jibu tosha kwa adui yake Makonda na kuonyesha kuwa sasa Wawili hawa wameamua kununua Uadui uliopo wa hizi Redio mbili pendwa za jijini Dar es Salaam na kuuhamishia katika Vita vyao vya Kisiasa na Kimaslahi.

Kauli za Waziri Nape za jana ni kama zifuatazo katika nukuu zake:

  • " Efm mmeonyesha kuwa nyie ni Watu mahiri Kiutangazaji "
  • " Unapomwona Mtu amewekeza namna hii usikurupuke tu huko ulikotoka na kuanza kumsakama sakama "
  • " Nitakuwa mtetezi namba moja wa Redio yenu pendwa ya Efm na msiogope wala kutishwa kwani nipo nanyi "
  • " Kwa uwekezaji huu mkubwa Serikali itailinda kwa nguvu zote Efm Radio "
  • " Na nyie TCRA msiwe wakali sana kwa Efm na muda mwingine mkiona wanakosea muwe mnawakumbatia kwani hawa ni kama Mtoto mdogo ambaya bado anajifunza kukaa "
  • " Nimefurahi sana kusikia kuwa Efm imepewe ruhusa ya kujipanua ndani ya Mikoa 9 kwani naamini itaweza kupendwa na kukubalika sana na Watanzania "
  • " Kuonyesha kuwa naipenda Efm hata juzi wakati natengeneza Kamati maalum ya Hamasa kwa Timu zetu za Taifa nchini niliamua kumuweka Mtangazaji maarufu Maulid Kitenge na nakumbuka nilipata changamoto nyingi kuwa kwanini kuna Watangazaji wengi wa Michezo lakini nikaamua kumuweka Kitenge na Mimi nikawajibu kuwa ukiona hadi nimemweka Kitenge basi jua ya kwamba ndiyo nimemwona anafaa, anaweza na anajua kuliko hao wengine "
Baada ya matukio haya ya hawa Majabali wawili wenye Uadui mkubwa sasa ni rasmi kuwa Vita yao imeanza na itazidi kuwa kubwa na pengine hata kuwa na madhara nchini kwani siyo siri kuwa Tanzania ina Vituo vingi vya Redio ila Clouds fm na Efm kwa sasa ndiyo Washindani wakubwa ambao ushindani au upinzani wao unaweza ukawa kama wa Vilabu viwili Vikongwe nchini Tanzania vya Mnyama Mnyamani ( Simba SC ) na Chura Churani ( Yanga FC ).

Niwatakie tu kila la kheri wawili hawa katika hii vita yao na kizuri zaidi ni kwamba wote wawili wanakubalika na huwa wanasifiwa kila mara na Mteule wao Mkuu.

Nawasilisha.
 
vita vya panzi furaha ya kunguru, acha migambo iruke na kukanyagana:D:D:D
 
Kwanza Efm sio radio kubwa nchini, zaidi ya hapo Dar es Salaam hakuna sehemu nyingine yeyote inakosikika ukilinganisha na Mawingu fm.

Pili, kama ni ushindani nahisi unafanyikia huko huko DSM.

Tatu, Efm bado ni radio changa huwezi fananisha kiushindani Efm na Mawingu kama simba na yanga walau ungesema Simba na Mbeya city uzi wako ungekuwa na maana kidogo.

Mwisho, acha uchochezi haya uliyoyaandika ni hisia zako binafsi na hata kama Makonda na Nape wana "bifuu" ww yakuhusu nn? Fanya yako mkuu.
 
acha uongo huku mikoani tunaisikiliza EFM Vizuri sana kupitia king'amuzi cha AZAM
 
Tanzania hakijatokea kituo cha redio kukizid clouds FM,,kwanza inajiendesha kibiashara tofauti na vituo vingine vingi,halaf ni cha kijanja,,na mbaya zaidi kina mtoto nakuja kwa kasi sana. Efm waanze kuwatengeneza watangazaji wao wenyewe kama mawingu wanavyofanya,,,then wajipambanua nchi karib yte ndio tuwape maksi zao kama wanaweza fikia hata nusu ya mawingu
 
Back
Top Bottom