Vita vyaathiri elimu ya watoto Sudan Kusini

Primier

Member
Dec 16, 2015
86
14
Shirika linaloshughulikia watoto la Umoja wa Mataifa limesema zaidi ya nusu ya watoto Sudan kusini hawako shule.

Kwa mujibu wa UNICEF, idadi hiyo ni kubwa kuliko nchi yoyote ile duniani.

Shirika hilo limesema watoto wa kike na wakiume wapatao milioni 1.8 hawajapata elimu darasani.

Shirika hilo limesema toka kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013 zaidi ya shule mia nane zimeteketea.

Serikali mjini Juba ilisaini mkataba na waasi mwezi Juni, lakini hata hivyo ghasia katika maeneo mengine ya nchi bado hazijakoma.


Chanzo: BBC
 
Last edited by a moderator:
Ebhana africa tuna laaana gani.....??
Na bado watu wanasema mungu yupo na anatupenda sana...inamaana hawaoni viumbe wake wanavyoteseka huko.
 
Back
Top Bottom