mafimboo
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 2,415
- 977
Baada ya kampeni kuisha ,na kupata kiongozi aliyejiita ni mtetezi wa wanyonge watanzania tulifarijika sana,hasa pale alipoonyosha hasira dhidi ya matumizi mabaya ya fedha za umma na kuwajibisha wakurugenzi kadhaa.
Lakini ghafla vita hivi vimechukua sura mpya baada ya vita vya ufisadi kuhamia kwa watumishi wadogowadogo(hawa wanajifunza ufisadi ni wanafunzi wa ufisadi) na kuwakimbia mafisadi wakubwa, hayati baba wa taifa aliwahi kusema kuwa kiongozi anayechukia ufisadi mtazame usoni kama kweli sura yake inamaanisha.
Kimsingi mheshimiwa anapaswa kujua kwamba watumishi anaowatwisha zengwe la ufisadi sio saizi yake hiyo ni kazi ya tume ya utumishi wa umma na bunge. Haiwezekani hata kidogo mheshimiwa atangaze kwenye vyombo vya habari eti kumsimamisha mkurugenzi mtu mdogo kabisa huku ni kukimbia majukumu yake ya kazi,mbaya zaidi kaminya hata uhuru wa vyombo vya habari kwa kuficha bunge gizani.
Bado tunahatua ndefu ya kupata kiongozi imara na shupavu asiogopa mafisadi mapapa.