vita vya nyuklia vyanukia peninsula ya korea.

vita vya nyuklia vyanukia peninsula ya korea.

Chibolo

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
5,768
Reaction score
8,041
ni baada ya zaidi ya miaka 60 ya vita ya maneno,sasa wanakaribia kuingia uwanjani kuanza vita kamili.
 
Mkuu labda ungetoa toa ushahidi kuliko kuweka sentensi like that
 
Bwana mdogo ameshadeclare war against US teh!
 
Mwehu huyu...ujana unamsumbua!!!!nafasi aliyopewa imemzidi umri na kimo!!!
 
Haijajulikana kama ni bahati mbaya au ni propaganda, lakini mpango wa Korea Kaskazini kuishambulia Marekani Kijeshi umevuja.

Katika mpango huo anaonekana kiongozi wa Korea N Kim Jong Un akiwa katika chumba maalum ( Command Post ) akitoa maelekezo kwa makamanda wake, huku nyuma yake ukutani kukiwa na ramani inayoonyesha mpango wa kuishambulia Marekani yenye maneno "Mpango wa Kuipiga Nchi ya Marekani".

Na wakati huo huo kiongozi wa Korea N Kim Jong Un ametangaza hali ya vita (State of War) na kuweka kila zana katika utayari.

Korea Kaskazini inaungwa mkono na China na Russia, wakati Korea Kusini inaungwa mkono na Marekani na imekuwa ikifanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi na nchi hiyo sambamba na kupokea zana za kivita.

Swali Gumu;
Je, Marekani itavumilia kuelekezewa makombora yanayoweza kujibu muda wowote ya Korea Kaskazini ?

N.B;
Vita kati ya Korea Kas na Korea Kus ni Vita kati ya China na Marekani

north-korea-jong-2_2522858b.jpg

North Korea plan to attack US mainland revealed in photographs - Telegraph
 
Sisimizi anajaribu kuangusha tembo! Hawa watu wa Asia sijui wana matatizo gani, walianza japan kuwashambulia marekani yalio wakuta mungu anajua kwa sisi tunaoishi japan tuliowahi kutembelea Nagasaki na Hiroshima ndugu zangu hayo mabomu yasikieni tu! Na hiyo ilikuwa atomic bomb sijui mziki wa nyuklia unakuwaje! Miaka Leo wajapan wanawataka marekani waombe msamaha kwa vita walioianzisha wenyewe! Kama North Korea anataka kuwachokonoa wamarekani awaulize ndugu jirani zake wajapan, ila watajuta Kama sio kulia na kusaga meno, wamarekani wameshapeleka ndege tatu mpaka sasa zenye uwezo wa kubeba nyuklia, ndege hizo zilizosafiri umbali wa karibu 20,000 kilomita non stop! Huu mziki Kama utaanza nikupanda ndege faster kurudi bongo kupumzika, kwani Nina uhakika north korea atapiga japan pia kwani wajapan ni washirika wa kubwa wa wamarekani.
 
Ni vita kuu ya tatu ya dunia, na hii vita ki-ukweli ni kati ya hawa wanaodhamini pambano, ila mmoja wapo atashindwa mapema kulingana na uadui aliojijengea paoja na ubabe wake!!

Mungu tuepushie mbali na kadhia hizi maana Umasikini, Njaa pamoja na Maradhi bado ni vita tosha hapa barani Afrika
 
Hakuna vita ww, Biashara ya China na Marekani ni kubwa sana kuliko Biashara ya China na North Korea, hivyo China hatakuwa mjinga wa kukubali vita iktokee na yeye amsapoti NK; never
 
Sisimizi anajaribu kuangusha tembo! Hawa watu wa Asia sijui wana matatizo gani, walianza japan kuwashambulia marekani yalio wakuta mungu anajua kwa sisi tunaoishi japan tuliowahi kutembelea Nagasaki na Hiroshima ndugu zangu hayo mabomu yasikieni tu! Na hiyo ilikuwa atomic bomb sijui mziki wa nyuklia unakuwaje! Miaka Leo wajapan wanawataka marekani waombe msamaha kwa vita walioianzisha wenyewe! Kama North Korea anataka kuwachokonoa wamarekani awaulize ndugu jirani zake wajapan, ila watajuta Kama sio kulia na kusaga meno, wamarekani wameshapeleka ndege tatu mpaka sasa zenye uwezo wa kubeba nyuklia, ndege hizo zilizosafiri umbali wa karibu 20,000 kilomita non stop! Huu mziki Kama utaanza nikupanda ndege faster kurudi bongo kupumzika, kwani Nina uhakika north korea atapiga japan pia kwani wajapan ni washirika wa kubwa wa wamarekani.

Tatizo la marekani ameshajenga hii kitu'inferiority complex'..tushamuona mmarekani kama super kutokana na hiyo iroshima na nagasaki...inawezekana kabisa mmarekani kudondoshwa na alliance ya n korea!
 
Personally nakerwa na tabia ya USA kujifanya yeye ndie kidume wa dunia.
Kwa kuwa CHINA NA RUSSIA wako upande wa NK wanaweza tumia nafasi iyo kuidhoofisha marekani ili hawa masocialist wawe dominant
 
Hizo ni ndoto za mchana ndugu yangu kufikiria North Korea atamshinda mwamerika.
 
Let them fight......pitfall so to speak.
 
vITA NI MBAYA ITATUATHIRI SANA HATA SISI HUKU, EEE MUNGU UKIONA VYEMA TUEPUSHE NA HAYA, ILA MAPENZI YAKO YATIMIE!!
 
RUSSIA na CHINA wakiwa upande wa N korea mpira utakuwa mtamu, ni kweli tutayumba kiuchumi lakini naona bora kuyumba kwa miaka michache kuliko kuendelea kutawalwa na wamarekani ambao wanawa shauri vibaya WB na IMF kutukandamiza kwa sera zao mbaya ktk chumi zetu. akiangushwa USA raha dunia nzima hasa amerika ya kusini, angekuwepo CHAVEZ angekuwa kasha nena tayari.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom