Vita ni vita, pigana rais wangu

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
Siku moja nilisikia Rijamaa Rimoja Rinasema , "VITA NI VITA MURA", sikujua huyu jamaa alikuwa na maana gani?. Kumbe vita ya maneno ndiyo mbaya kuliko hata ile ya kushika SILAHA. Nadhani hii inatokana na ukweli kwamba, kabla ya vita ya kushika mtutu ni lazima ianze ile ya maneno ambayo madhara yake ni makubwa.

Ni vita hii ya maneno mengi yakiwa ya uongo kutoka vyama vya upinzani na nyingine ndani ya CCM wenyewe ndiyo inasababisha watanzania wengine tudanganyike na kuamini eti Serikali ya JK haifanya kitu na hakuna jambo la msingi la kufanya vita hii iwepo bali tu RAIS wangu JK awe ndiye wa kulaumiwa na lengo haliishii hapo bali eti mwisho wake na wengine wapate kuingia IKULU baada ya kushinda vita hii ya maneno.

Kuna nini jipya katika vita ya maneno inayoendeshwa na makundi ndani ya CCM kama siyo chuki inayotokana na baadhi ya watu hao kukosa nafasi walizoaidiwa huku wengine wakiwa na hasira ya kupoteza nafasi zao baada ya kuonekana wazi hawakujiandaa kwa moyo wa dhati kuwatumika watanzania bali matumbo yao. Tujiulize swali hapa, hivi kweli wote wangeweza kupata kazi kwa ujumla wao? aidha kwa wale waliopoteza nafasi zao wanataka kutuambia kwamba walionewa au ni chuki ya kunyang'anywa tonge mdomoni? na kama walionewa si waseme wazi sisi tulionewa na ukweli ni huu.
Nikija upande wa UPINZANI ambao una macho mawili lakini umefunga jicho moja lillokuwa linaona mazuri yaliyofanywa na RAIS wangu KIKWETE na kubakiza jicho lile ambalo si kwamba linaloona mabaya tu bali linadiriki hata kukonyeza watanzania kuwa kataeni kufanya kazi zinazoelekezwa na Serikali ya JK. Yapo mambo mengi ambayo yamesemwa na wapinzani kuhusu Serikali na bila hata haya, hatua tunazoshauriwa na wapinzani hawa kuchukua ni kuandamana, kugoma, kukataa kushiriki shuguli za maendeleo, kukataa kutii kuheshimu sheria na taratibu za nchi, kuwazomea viongozi kila wanapopita na pale wanapokuwa na wananchi kutekeleza majukumu yao. Je ndilo suluhisho? ama ni njama za kutaka tupoteze muda bila kufanya kazi ili lawama zizidi kumwendea Rais wangu?

Sitaki kusema sana kuhusu hili la wapinzani kwa vile najua wao malipo yao yapo. Nasema malipo yao yapo kwa vile tayari wameshatufundisha kuwa Rais hatakiwi kusafiri, kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo ni ya Serikali na siyo wananchi wenyewe, migomo ni haki ya kila mtu, maandamano ni haki bila kujali ni halali au la. Wameshatufundisha kuwa ni marufuku kuheshimu sheria za nchi na zaidi wameshatufundisha kuwa kuwazomea/kuwakashfu/kuwadhihaki viongozi ndiyo demokrasia ya kweli. Watambue kuwa hii ni sawa na dhambi ya kula nyama ya mtu, haitaishia hapo. Hivyo, watakapoingia madarakani japo naamini hilo wananchi hawatalirusu kwa sasa , wakatugeuka kutekeleza hayo basi itabidi wakabiliane na nguvu zaidi.




JK PAMBANA VITA NI VITA TU, TUNAKUAMINI.
 
Sijaona pointi hapa. Ngoja nisubiri wengine labda wataona chochote.
 
Mura wetu,Amang'ana.Umepoteza muda mwingi kuandika hutuba kama sa mukuu wa kitengo cha upererez,rakini nisikufunje moyo,tafuta mhariri na mushauri kuhusu ritopic hiri mura wetu.
 
Ndugu yangu anapigana vita yeye dhidi ya yeye hana adui mwingine zaidi yake mwenyewe acheni kutafuta mchawi kwani angekua kafanya mazuri msinge subiri wapinzani wayatangaze mngeweza kuyatangaza nyie wenyewe lakini kwakuwa hayapo mnaomba huruma ya wapinzani wasiwambie wananch yaliyopaswa kufanyika na hayajafanyika huu muda wakutangaza na kuhubiri miaka hamsini ya uhuru nadhani kama mnayajua mazuri yake basi yatangazeni pia usisahau kuwakumbusha wananchi maisha bora kwa kilamtanzania aliyoahidi alafu usisubiri wapinzani waseme waulize wananchi wewe mwenyewe je wameyapata? kisha njoo hapa utujulishenini umejibiwa
 
wewe si ndiyo wale wanaoelewa kutumia MASABURI, sasa utaelewa kweli?
Mkuu Wang'ayo hizo ni changamoto za humu Jf, zivumilie tu mkuu acha misemo ya jicho kwa jicho. Songa mbele kutetea nukta zako
 
mmm madhara ya kufikiri kwa kutumia tumbo,wewe ndo unmdhalilisha Rais,umewezaje ukijiknyagakanyaga bila hata kueleza hayo ambayo wapinzani walitakiwa wamsifie kwayo.
yaeleze yatakiwayo asifiwe nayo,then uhoji wanaomponda,unaandika mambo kijumla jumla yaelekea mwenyewe huna hata ulijualo kumsifu nalo,basi ungemsifu hata kwa picha na 50cent basi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom