Vita hewa vya kiuchumi na Dhuluma kwa wawekezaji wazawa

Mtu wa Asali

Senior Member
May 9, 2022
152
291
Kuna kitu huwa najiuliza wakati wote kuwa sisi Tanzania kipindi cha 2015-2021 pale Mungu alipo amua ugomvi tuliaminishwa kuwa kuna vita ya kiuchumi!

Huu ulikuwa ni uongo na uzandiki wa wazi kabisa. Tanzania hatukuwa na vikwazo vyovyote vya kiuchumi bali tulikuwa na vikwazo vya kisheria kutokana na kuvunja mikataba kiholela na wawekezaji.

Magufuli alituaminisha kuna vita ya kiuchumi si kweli tulikuwa na mkwamo wa kidiplomasia, nchi iliendeshwa kama familia palipokuwa na migogoro haikusuluhishwa kwa maslahi ya nchi bali iliamuliwa kibabe. Sakata la kuchoma vifaranga, sakata la kuwauwa wavuvi wa nchi jirani.

Ukitazama haya mambo yote Magufuli hakuwa anajali hata kidogo ni mtu katili ambaye alithubutu kula hata rambirambi za wahanga wa tetemeko pale Kagera.

Nchi hii ilikosa mfariji kabisa, Nchi iliendeshwa kwa akili ya Rais anavyotaka Task force ziliwafilisi watoto wa kitanzania waliowekeza kwenye Bureau waliingia kwenye umaskini mkubwa.

Magufuli hakujua diplomasia hakujua Mahusiano mazuri yanavyojenga na kukuza uchumi. Hakujua Sadam Hussein kuwa ni Rais wa Iraq.

Namnukuu “Rais wa Libya sadam husein hapana wa Libya gadafi, Sadam husein wa Kuwait.” Tangu siku hii nilifahamu kidiplomasia tunaingia kwenye tope.

Licha ya kuboronga kidiplomasia hata ndani alishindwa kujenga Mahusiano na wawekezaji wazawa aliwachukia walikuwa maadui mfanyabiashara Vicent Lasway mmiliki wa Kibo Palace hadi leo yupo taabani kiuchumi, alikwapua kila kitu jamaa ameisha.

Mfanyabiashara Mohamed Dewji alikamatwa na kutekwa kwenye hotel ya kifahari na Watekaji walikaa naye zaidi ya siku sita.

Msanii Roma mkatoliki alitekwa siku ya tatu akapatikana ununio na majeraha kibao. Serikali yake ilikuwa katili kwa Vijana wa kitanzania.

Mwandishi Kabendera hadi mama yake mzazi alifariki Dunia kwa kesi ya mchongo chini ya serikali ya Magufuli kosa lake kuandika Habari kwenye magazeti ya mabepari juu ya serikali suala lile lilimchukiza Rais. Kabendera akatupwa Jela.

Tajiri Yusuph Manji alinyang’anywa kampuni ya Tigo aliyoinunua kihalali kwenye soko la hisa kijana mdogo, Paul Makonda alimsweka ndani wiki hadi Manji kukimbia nchi.

Watoto wa kitanzania waliotafuta kwa jasho walichukiwa ndani ya ardhi ya kwao wakalazimishwa kuishi kama mashetani wakateswa kwa kudra walizojaliwa na Mungu kuwa matajiri kwa kiongozi aliyejinasibu ni Mcha Mungu.

Baba Askofu Severine Niwemugizi alipo unyanyua mdomo katika baraza la maaskofu alitishiwa siyo Raia.

Askofu kakobe alipounyanyua mdomo wake juu dhidi ya serikali, TRA walibisha hodi Kanisani. Baba Askofu aliufyata hadi kukimbia uhamishoni South Africa.

Aliwaumiza wale waliojaliwa kudra za Mwenyezi Mungu aliwanyonga kwa siri wale waliomsema pembeni.

Mfanyabiashara mmoja kule Kanda ya Kaskazini mmiliki wa Kerai Construction hadi leo anajiuliza Rais yule alikuwa Mtanzania au tulimwazima toka nchi Jirani sababu matendo aliyoyafanya yalikuwa kinyume na sisi watanzania wenyewe tulivyo. Kosa lake ni kumfadhili mgombea wa Urais Mwaka 2015.

Alikwiba, akadhulumu akatapanya mali kwa mahawara akapenda sifa kuliko kiumbe mwanamke akataka atukuzwe akagawa vyeo kama njugu kwa vibinti vidogo umri wa watoto wake ilibakia kuitwa Mtakatifu Jiwe.

Aliuza nyumba za serikali baadaye alizinyang’anya rejea sakata la mwanaume wa mkoa wa Tarime yule anaitwa Zakaria alitupwa Jela. Kuna mzee alinyang’anywa nyumba aliyonunua kihalali pale Ilala alilazimishwa kusarenda nyumba ile au atupwe Jela chini ya mtutu wa bunduki.

Hivi ndivyo vita vya Kiuchumi hewa vya Mhe. Mungu kwa sauti ya Profesa Majalala.

Legacy ya Magufuli ndiyo hii daima tutamkumbuka kwa vituko vyake.
 
Jiwe kaondoka zaidi ya mwaka sasa. Wengi humu mna hali mbaya kuliko alivyowaacha. Wachache ndio wanajiona afadhali kumbe ni kama panya tu wanaoambulia vipande vya mikate kwenye sakafu ya jiko chafu!
Wee Hali mbaya ipi? Mwenye Hali mbaya hawezi fanya kufuru ya kujenga msingi kwa Mawe,blocks na concrete 👇
 
Attachments

  • IMG_20220718_185131_551.jpg
    IMG_20220718_185131_551.jpg
    920 KB · Views: 6
Approach ya serikali ya awamu hii ni kuwakandamiza wazawa na kuwafurahisha wageni.

Hii ni approach mbaya.

Wapiga kura ndio wa kupewa kipaumbele na sio hao wanaokuja kujinufaisha na kuondoka.
 
Jiwe kaondoka zaidi ya mwaka sasa. Wengi humu mna hali mbaya kuliko alivyowaacha. Wachache ndio wanajiona afadhali kumbe ni kama panya tu wanaoambulia vipande vya mikate kwenye sakafu ya jiko chafu!

Nashukuru umemtambua kwa jina lake kamili. Mtakatifu Jiwe a.k.a Mhe. Mungu.
 
Kuna kitu huwa najiuliza wakati wote kuwa sisi Tanzania kipindi cha 2015-2021 pale Mungu alipo amua ugomvi tuliaminishwa kuwa kuna vita ya kiuchumi!

Huu ulikuwa ni uongo na uzandiki wa wazi kabisa. Tanzania hatukuwa na vikwazo vyovyote vya kiuchumi bali tulikuwa na vikwazo vya kisheria kutokana na kuvunja mikataba kiholela na wawekezaji.

Magufuli alituaminisha kuna vita ya kiuchumi si kweli tulikuwa na mkwamo wa kidiplomasia, nchi iliendeshwa kama familia palipokuwa na migogoro haikusuluhishwa kwa maslahi ya nchi bali iliamuliwa kibabe. Sakata la kuchoma vifaranga, sakata la kuwauwa wavuvi wa nchi jirani.

Ukitazama haya mambo yote Magufuli hakuwa anajali hata kidogo ni mtu katili ambaye alithubutu kula hata rambirambi za wahanga wa tetemeko pale Kagera.

Nchi hii ilikosa mfariji kabisa, Nchi iliendeshwa kwa akili ya Rais anavyotaka Task force ziliwafilisi watoto wa kitanzania waliowekeza kwenye Bureau waliingia kwenye umaskini mkubwa.

Magufuli hakujua diplomasia hakujua Mahusiano mazuri yanavyojenga na kukuza uchumi. Hakujua Sadam Hussein kuwa ni Rais wa Iraq
Namnukuu “Rais wa Libya sadam husein hapana wa Libya gadafi, Sadam husein wa Kuwait.” Tangu siku hii nilifahamu kidiplomasia tunaingia kwenye tope.

Licha ya kuboronga kidiplomasia hata ndani alishindwa kujenga Mahusiano na wawekezaji wazawa aliwachukia walikuwa maadui mfanyabiashara Vicent Lasway mmiliki wa Kibo Palace hadi leo yupo taabani kiuchumi, alikwapua kila kitu jamaa ameisha.

Mfanyabiashara Mohamed Dewji alikamatwa na kutekwa kwenye hotel ya kifahari na Watekaji walikaa naye zaidi ya siku sita.

Msanii Roma mkatoliki alitekwa siku ya tatu akapatikana ununio na majeraha kibao. Serikali yake ilikuwa katili kwa Vijana wa kitanzania.

Mwandishi Kabendera hadi mama yake mzazi alifariki Dunia kwa kesi ya mchongo chini ya serikali ya Magufuli kosa lake kuandika Habari kwenye magazeti ya mabepari juu ya serikali suala lile lilimchukiza Rais. Kabendera akatupwa Jela.

Tajiri Yusuph Manji alinyang’anywa kampuni ya Tigo aliyoinunua kihalali kwenye soko la hisa kijana mdogo, Paul Makonda alimsweka ndani wiki hadi Manji kukimbia nchi.

Watoto wa kitanzania waliotafuta kwa jasho walichukiwa ndani ya ardhi ya kwao wakalazimishwa kuishi kama mashetani wakateswa kwa kudra walizojaliwa na Mungu kuwa matajiri kwa kiongozi aliyejinasibu ni Mcha Mungu.

Baba Askofu Severine Niwemugizi alipo unyanyua mdomo katika baraza la maaskofu alitishiwa siyo Raia.

Askofu kakobe alipounyanyua mdomo wake juu dhidi ya serikali, TRA walibisha hodi Kanisani. Baba Askofu aliufyata hadi kukimbia uhamishoni South Africa.

Aliwaumiza wale waliojaliwa kudra za Mwenyezi Mungu aliwanyonga kwa siri wale waliomsema pembeni.

Mfanyabiashara mmoja kule Kanda ya Kaskazini mmiliki wa Kerai Construction hadi leo anajiuliza Rais yule alikuwa Mtanzania au tulimwazima toka nchi Jirani sababu matendo aliyoyafanya yalikuwa kinyume na sisi watanzania wenyewe tulivyo. Kosa lake ni kumfadhili mgombea wa Urais Mwaka 2015.

Alikwiba, akadhulumu akatapanya mali kwa mahawara akapenda sifa kuliko kiumbe mwanamke akataka atukuzwe akagawa vyeo kama njugu kwa vibinti vidogo umri wa watoto wake ilibakia kuitwa Mtakatifu Jiwe.

Aliuza nyumba za serikali baadaye alizinyang’anya rejea sakata la mwanaume wa mkoa wa Tarime yule anaitwa Zakaria alitupwa Jela. Kuna mzee alinyang’anywa nyumba aliyonunua kihalali pale Ilala alilazimishwa kusarenda nyumba ile au atupwe Jela chini ya mtutu wa bunduki.

Hivi ndivyo vita vya Kiuchumi hewa vya Mhe. Mungu kwa sauti ya Profesa Majalala.

Legacy ya Magufuli ndiyo hii daima tutamkumbuka kwa vituko vyake.
Kwa umri ulio nao fanya kazi, acha porojo. Una safari ndefu ya kuyaelewa maisha.
 
Kumchukia Magufuli wakati huu akiwa hayupo ni zaidi ya ukahaba

Mtanzania pekee wa kumsema Magufuli ni Tundu Lisu kwa sababu alikuwa akimsema tangu akiwa hai!
 
Wewe umekandamizwa sehemu ipi? Jiwe aliwainua Wazawa kama akina nani?
Awamu hii imejikita kwenye kuwahamasisha wawekezaji wa nje kuja kuwekeza.

Hakuna mkazo katika kutengeneza mazingira ambayo wazawa watakua wanufaika wa kwanza wa hizo investments.

Kumpa uhuru mwekezaji afanye anavyotaka ni makosa kwani anayetakiwa kunufaika wa kwanz kabisa ni yule aliyepo katika mazingira ya uwekezaji husika. Hata kanuni ya asili inataka hivyo.

Sheria zinabadilishwa tu ili kuwafurahisha wawekezaji badala ya kuboreshwa ili sisi tunufaike na huo uwekezaji.
 
Ndio wa Nje wakija wanaleta mitaji,teknolojia na ajira nk..

On top of that wananchi wananufaika kwa local content,soko na ajira.

Serikali inafaidika kwa mapato na exports.

Bila FDI hakuna maendeleo
 
Tanzania sio wageni kwa FDI tumekuwa nazo na hazijawahi kuwa na manufaa yoyote.

Kodi ndogo na ajira za kubangaiza hazina maana yoyote.

Tuna hitajika kuwa sehemu ya uwekezaji wowote na sio kuokoteza makombo ya kodi na ajira za kuonewa huruma.

Nchi kama Botswana na nyinginezo zina mifumo mizuri ya uwekezaji ambayo inawanufaisha wananchi na approach ya awamu ya tano ilikua ni kutupeleka huko.

Ila sasa kinachofanyika ni kurudi kule kule Misri ambapo watanzania wanageuka watumwa kwenye nchi yao wenyewe.
 
Tuonyeshe kwa takwimu ajira ambazo sio za kubangaiza mlizoandaa wewe na Jiwe
 
Magufuri alijitahidi kuleta ukombozi wa fikra, alijua ukimkomboa mwanadamu kifikra umemkomboa kiuchumi!

vita ya kiuchumi aliyopigana magufuri ni pamoja kuondoa mianya ya kukwepa kodi kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya tanzania, na hili alifanikiwa

na kilichomsaidia hakuangalia mtu usoni, hakujali ulimsaidia kwenye kampeni zake au lah, mfano kuna radio pale mwanza ilimpa airtime sana wakati wa kampeni kumbe wale jamaa ni wakwepa kodi, alichofanya kila mtu anajua

kwahiyo ukiangalia wafanyabiashara ambao wanalalamika waliumizwa na magufuri, wengi ni wakwepa kodi wakubwa na walizoea wakajua kukwepa kodi ni kawaida hivyo alivyowazuia wakamuona mtu wa ajabu

for me Magufuri was the best president we ever had after nyerere.
 
Aliondoa mianya ya kukwepa Kodi au sio?

Na huu wizi wa 1.2 T aliouganya umewahi fanywa na utawala gani?

Kama aliondoa mianya ya Kukwepa Kodi inakuaje alikuwa anapika Takwimu za mapato?

Kama alifanya yote hayo iweje miaka 6 ashindwe kumaliza hata sgr km 200?

Kama alifanya yote hayo iweje afukize watumishi,achukie pesa za wastaafu kwenye mifuko ya pensheni na kuacha kuwalipa,iweje ashindwe kuajiri na iweje aue kilimo?

Toeni ujinga wenu hapa na mkadanganye wake zenu.
 
wizi 1.2 tillion niwekee na ushahidi usio na shaka

weka ushahidi wa takwimu alizopika

wewe na wapumbafu wenzio mliwahi kuwaza hata kujenga sgr ya 1km?

hakuna mtumishi mwenye cheti halali aliyefukuzwa

kilimo kipi alikiua? kwamba kwenye awamu yake hakukuwa na shuguri za kilimo?
 
Kwa hiyo hujaona taarifa ya CAG? Na kwa nini hadi leo hii Serikali haileti majibu ila inajizungusha tuu?

Ndio maana Wadau wanaitaka serikali ifanye uchunguzi inaruka ruka tuu 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220415-072852.jpg
    Screenshot_20220415-072852.jpg
    122 KB · Views: 4
  • 1650491737485.png
    1650491737485.png
    60.6 KB · Views: 3
  • Screenshot_20220415-140726_1.jpg
    Screenshot_20220415-140726_1.jpg
    49.3 KB · Views: 3
Kwa hiyo hujaona taarifa ya CAG? Na kwa nini hadi leo hii Serikali haileti majibu ila inajizungusha tuu?

Ndio maana Wadau wanaitaka serikali ifanye uchunguzi inaruka ruka tuu 👇
Hivi vijigazeti uchwara na vi-tweets vya vibaraka wa mabeberu ndio ushahidi? Mtumiage akili hata kidogo. 😁
 
Back
Top Bottom