Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,233



Kumekucha!!Ni siku nyingine tena,Mkuu wa Mkoa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa wa Dsm,ndugu Paul Makonda ataongea leo na waandishi wa habari kuhusu muendelezo wa vita ya madawa ya kulevya ktk jiji la Dsm.

Mkuu wa Mkoa atakuwa mubashara Azam Tv mara ifikapo saa 05:00 asubuhi leo hii.

Tetesi ni kuwa,mkutano huo unaweza kuwa ni kujibu tuhuma za kuwa anawakabili "dagaa" na wakati "mapapa" wa biashara hiyo wapo.Na majibu ya mkuu wa mkoa yatakuwa ni kuwataja hao mapapa na kuelezea hatua zitakazochukuliwa...

Tega usikie....(Stay Tuned)

=======
UPDATE:
=======

ORODHA KAMILI:

IMG_3050.JPG

IMG_3051.JPG

IMG_3052.JPG

16425859_1869827136623498_8089691789862529236_n.jpg

Ameanza kwa Kumshukuru Rais wa Jamuhuri.

Paul Makonda asema anataka wauzaji wa dawa za kulevya wajulikane hadharani na hakuna sababu ya kuficha.

Paul Makonda asema vita vya dawa za kulevya vilianza muda mrefu kwa kufutilia hali ilivyo mitaani.

'Kuna watu nilitaka nikutane nao polisi, kuna tofauti kati ya kukamatwa na kuitwa, unapoitwa unapewa nafasi ya kusikilizwa'-RC Makonda


'Kampeni hii dawa ya dawa za kulevya si ya kufanyika kimyakimya tunataka hata watoto wadogo wajue dawa hizi ni hatari kwa afya'-RC Makonda

'Asante kwa watu kama TID, nawapongeza kwa kukiri na kusema kuwa wanatambua namna walivyoingia na kuomba serikali kuwasaidia'-RC Makonda

'Tumemaliza awamu ya kwanza vita ya dawa za kulevya, sasa hii ni awamu ya pili ambayo itakuwa si nyepesi itakuwa na mawimbi mengi-Makonda

'Awamu ya 2 ya vita ya dawa za kulevya tunaianza leo na tunaianza tukiwa tumekamilika, nimekuwa kwenye operesheni usiku na mchana- Makonda

'Watu wanafanya biashara za dawa za kulevya na meli zinazokuja na mafuta'-RC Makonda

'Kuna mama kazi yake ni kusafirisha watoto wa kike ambao wanapewa dawa za kulevya, wawili wako jela China na amewatelekeza'-RC Makonda

'Tukiendelea kuvutanavutana tutapoteza lengo la kupambana na dawa za kulevya'-RC Makonda

'Tukishindwa vita hii ya dawa za kulevya, hajashindwa Makonda au Rais Magufuli tumeshindwa wote'-Rais Makonda

'Tuko na majina 65, nitahitaji kukutana nao ijumaa, wako wanaosemekana wanatumia, wako wanasemekana wanazo taarifa zitakazotusaidia-Makonda

'Nawashukuru wenyeviti wa mitaa wameanza kuleta majina ya watu ambao wanawasiwasi nao kuhusu dawa za kulevya'-RC Malone's

'Kila tunayemuita tunamfahamu kuliko mnavyofikiri kazi yetu ni kuwasikiliza'- RC Makonda

'Zile nyumba mnazozitilia shaka, hamuelewi hata kinachoendelea ni wajibu wetu wananchi kutoa taarifa na taarifa zitakuwa ni siri-RC Makonda

'Kuna ambao tuliwaita wako nje ya DSM, wapo waliotoa taarifa na watafika ila wapo waliokimbia tunawafuatilia na tutawapata wote'- RC Makonda

'Nawashukuru ndugu zangu walioko nchi mbalimbali kwa kunipigia simu na kunipa taarifa mbalimbali'-RC Makonda



Pia soma:
 
Anaongea nini sasa.
Na yeye akareport central akahojiwe. Tuhuma zake sio za kwenda kwenye media kujisemesha.

Hii tuhuma ya yeye kuwa na mahusiano ya kmapenz na dealer wa kmataifa wa madawa sio ndogo. Magufuli hapashwi kulifungia macho hili.

Na mali alizo nazo sasa zifanyiwe auditing. Huyu kwa mwaka mmoja inasemekana ameaccumulate mali kumzidi hata Raisi wake. Hata mawaziri hawamfikii. Sasa awataje wahisani wake wachunguzwe.

Na wale wauza shisha waliotaka kumuhonga awataje nao wahojiwe. Msitufanye sisi wajinga

Huyu atakuwa anashirikiana na gang flani la wauza unga ila kaja na project ya kuwaeliminate dealers wengne ili watakaobaki wawe monopoly ili wamake abnormal profit. Tusidanganyane hata siku moja mkuu wa mkoa ambaye ni kada wa CCM et kupambana na madawa ya kulevya. Huku ni kujitaftia mazingira ya kupewa rushwa tu na biashara mwisho wa siku itaendelea as usual.

Kuna mwaka USA ilipata tuhuma za kutumia madawa ya kulevya kama source of Government income. Ni kwamba USA ilikuwa vbya kwenye uchumi. Serkal ikaja na mbinu kali za kutyte wauza madawa. Bei ya madawa ikapanda. Wao walikuwa na special depertment kwenye kitengo cha CIA/ Polisi waliojulkana kama bad cops ambao walikuwa wanachukua percent kutoka kwa drag dealers. Hii percent ilienda serkalini. Katika hiyo miaka madawa yalisafirishwa mpaka na ndege za jeshi.Allegations of CIA drug trafficking - Wikipedia

43f5dd645d2131afae370625a6bdbe00.jpg


Sasa isije ikawa na tz ikaelekea uko.
 
Aache chuki binafsi....kamkomalia wema kwa sababu hakunyamaza...huwezi kupambana na ufisadi ukiwa na ubinafsi na huwezi kuweka hisia zako pembeni.
Amesuia wema asiende mahakamani huku siro alikua tayari ametamka kuwa watapelekwa mahakamani..
Amekosa moral authority ya hii vita
 
Aache chuki binafsi....kamkomalia wema kwa sababu hakunyamaza...huwezi kupambana na ufisadi ukiwa na ubinafsi na huwezi kuweka hisia zako pembeni.
Amesuia wema asiende mahakamani huku siro alikua tayari ametamka kuwa watapelekwa mahakamani..
Amekosa moral authority ya hii vita
Huyo WEMA anaandaliwa mashtaka mengine ya kumtukana Mkuu wa mkoa na kutoa lugha zilizokosa maadili, Ili akipandiswa mahakamani ajibu tuhuma zote!
 
Imani na nchi yangu imebaki kwenye kugombana na Wanyasa tu wakisema ziwa Nyasa ni lao.

Lakini hapa tulipofika ni mtihani. Misri walitatua mtihani wao wenyewe.
Libya walitatua mtihani wao wenyewe.
Marekani wanahangaika kutatua mtihani wao wenyewe.
 
Kuna baadhi vyama mpaka leo havieleweki vinasimamia maslahi ya nani, kuna wawakilishi wao walikuwa wanapiga sana kelele juu ya madawa ya kulevya leo mtu anasimamia wao wanakuja juu kutetea hao wahusika kila siku mapovu yanawatoka juu ya mapapa wa madawa hamjui kuwa viongozi wenu pia ni wahusika wakuu wa madawa nani asiye urafiki wa Lowassa na Rostam, rostam na familia yake ni mmoja wa wahusika wakuu.
Je nani hajui kuhusu GWAJIMA ambaye ndiye alkua mlez wa CHADEMA nani hajui juu ya haya.

Naona humu tunashabikia tunapiga kelele juu ya kitu ambacho hatukijui, msifuate upepo nyie bendera.
 
Back
Top Bottom