Virusi vya corona: Je, tunaweza kupata virusi vya corona kupitia macho?

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
7,223
12,943
Inawezekana kupata SARS-CoV-2 kupitia macho

Daktari wa kwanza duniani kufariki dunia kwasababu ya ugonjwa wa Covid-19 alikuwa daktari bingwa wa macho Li Wenliang: na tangu wakati huo, macho yamekuwa yakihusishwa kwa karibu sana na janga la corona.

Ingawa moja ya njia inayofahamika katika maambukizi ya ugonjowa wa corona ni matatizo katika mfumo wa kupumua, lakini pia unaweza kusambazwa miongoni mwa binadamu kwa mikono na kushika maeneo machafu.

Lakini kisichofahamika ni virusi vinavyopatikana katika machozi ya binadamu pamoja, seli za konea na utando wa kamasi.

Kupata maambukizi ya virusi vya corona kupitia macho na machozi ni jambo linalowezekana kabisa.

Virusi vilivyopata maambukizi ya erosoli yaani umajimaji hukutana na eneo la jicho na baadaye huingia katika mfumo wa upumuaji kupitia njia iliyo kama mfereji.

Seli za binadamu ambavyo virusi vya corona hutumia kuingia mwilini zipo pia katika macho

Uchunguzi wa awali umeangazia sana maambukizi ya njia ya kupumua. Hata hivyo, ushahidi wa maambukizi ya macho unazidi kuongezeka.

Baadhi husababishwa na virusi vyenyewe huku mengine yakitokana na janga ama kwasababu ya mabadiliko ya kimaisha au kwasababu ya watu wanaokaa sana kwenye vyumba vya kuhudumia wagonjwa mahututi ambako wanaweza kuwa huko kwa wiki tatu hadi sita wakitumia vifaa vya kusaidia kupumua.

Ni muhimu kuepuka kugusa au kufuta macho yako

Kwa upande mwingine, kujifungia kwa muda mrefu na ulazima wa kutumia barakoa kumeongeza visa vya macho kuwa makavu na magonjwa mengine ya macho.

Maambukizi ya macho yanayotokana na SARS-CoV-2 hutokea sana na yanajumuisha kikope, jicho kuwa kavu, kuwasha, kutoona vizuri na kutostahamili wanga mkali kama wa kupiga picha.

Dalili hizo zinaweza kujitokeza kama ishara za awali za ugonjwa wa virusi vya corona.

Kipindi cha kuatamia cha virusi ni kuanzia siku 5 hadi 14.

Unahitaji kuhakikisha mikono yako ni misafi kabla ya kuosha na kuvaa lenzi za macho

Pia wakati wa maambukizi ya macho, neva zinazosaidia misuli ya jicho zinaweza kushindwa kufanya kazi.

Katika visa kidogo pia huwa kunatokea uvimbe kwenye neva za macho.

Lakini mbali na konea, virusi vya corona pia vimebainika kwenye retina za jamaa za waliofariki dunia kwasababu ya maambukizi ya virusi vya corona.

Chanzo:- BBC SWAHILI
_117367902_ojos2b.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Raisi wetu mpendwa mtukufu wa Taifa ajiuzulu tu kwa hili janga amefeli sana sana
 
Dawa pekee ya kupona korona ni kuwa na kinga bora tu ,life styles zetu hauwezi kuishi bila kujiambukiza korona eti kwa kuvaa barakoa au kunawa na maji tiririka.
 
Back
Top Bottom