"Virungu" vimezidi...

The Donchop

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
294
376
Ndugu zangu habarini?

Siku hizi imezuka tabia ya watu kuomba pesa hovyo especially ikifikia mwisho wa mwezi.

Yan mtu akisikia una kazi, kila mwisho wa mwezi lazima atengeneze shida.

Tunapenda sana kusaidia ndugu, jamaa na marafiki lakini tambueni hata sisi tunaofanya kazi tuna yetu.

Wengine hatupendi kuombaomba sio sababu sina matatizo ila sababu najiheshimu na ninajitambua. Kuombaomba ni tabia mbaya.

Sikatai kuwa kuna siku nawakopa wenzangu lakini ni mara chache sana na hadi nilazimike kufanya hayo.

Mnapoona tupo kimya, msidhani tuna pesa. Tuna madeni lukuki, tuna makodi, tuna mahitaji binafdi, wategemezi nk.

Mtatuchukia bure na kutusababishia tupate dhambi ndogondogo za kudanganya kuwa tumetimuliwa kazini.
 
Toka yaliyonikuta siku hizi sisaidii watu kabisa zaidi ya wazazi au mzaliwa mwenzangu mwenye uhitaji sana tofauti na hapo wewe kama unataka kulewa twende bar nitakununulia ukilewa rudi ukalale
 
Kwahiyo sisi wenye shida na ela za kula ndo tutajiju au sio?
Sawa mkuu tumekupata
 
Omba omba sio wa kuwaendekeza, saidia wale ambao unaona kweli wana shida.

Bora wakuite mchoyo kuliko kukuchuna kila wanapojiskia utashtukia hufanyi maendeleo hela zinaishia kugawa kwa watu wasio na faida.
Surely yaani kuna watu daah , afu heri wakuombe kidogo wanaomba kikubwa kukumalizia kabisa😅😅

Its okay kua stingy n mean
 
Ni shida tu mkuu hatupendi kuomba tusamehe ni mitihani tu ya dunia ndo inatufanya tuwe wasumbufu, ila msaada wako haupotei utabaki kama fadhila na iko siku tutalipa
 
Vp kuhusu michango ya harusi mleta mda anaongelea virungu kutoka kwa ndugu au jamaa na marafiki, harusi watu wanachangia sana kadi kama 10 unapokea na zote unachangia ila ndugu akiomba msaada malalamiko kibao basi na harusi tuache kuchangia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom