Vipi ni vikwazo katika mchakato wa ajira za Tanzania?

Baba Jotham

Member
Mar 6, 2012
84
40
Wanajamvi,wengi wetu tunaamini swala la ajira Tanzania ni changamoto.Wasomi wa fani mbali mbali hawana cha kufanya,na wengine wamekata tamaa za maisha.Napenda kuleta uzi huu ili vijana tujadiliane na tujikumbushe.Nina amini wapo wenye mawazo chanya ambayo yanaweza yakatufumbua macho wengi wetu tuliokata tamaa.

Naomba tujadili kwa kujibu maswali haya :-"Unadhani vipi ni vikwazo katika mchakato wa ajira za Tanzania?,nini kifanyike kuboresha upatikanaji wa kazi, kukabiliana na kukosekana kwa usawa katika kuajiri?"

Maoni binafsi pia ni muhimu,
 
Mpwa rekebisha kidogo heading hakuna neno "unazani" bali kuna neno "unadhani" na hili huenda ndio sababu ya kwanza kukosa ajira kwenye mchakato maana tuna matatizo ya uandishi.

Elimu yetu kwa kiasi kikubwa sana imebadilishwa na kuwa elimu ya kukariri na kufaulu, kwa mfano, leo hii hakuna shule tena za michepuo ya Kilimo, Biashara, Ufundi na Mapishi, miaka ile shule kama Tanga technical ilitoa technicians wa ukweli, Magamba Boys (now Sebastian Kolowa Memorial University) ilikua shule ya Mchepuo wa kilimo na ufugaji na kweli Vijana walitoka hapo walikua Wakulima na Wafugaji kweli kweli, Kaka yangu aliwahi kuja nyumbani likizo na akajenga banda zuri sana la kuku, Korogwe Girls ilikua Kilimo, Mapishi na Ushonaji. Kwahio kila mwananfunzi alietoka hapo kabla ya kuendelea na chuo alikua tayari alikua na ABCs za nini cha ku-specialize. Leo hii hata Walimu hao hawapo tena.

Kuruhusu kila shule itumie vitabu vyake pia imekua bonge la mistake, watoto wetu na vijana wetu leo hii wanatumia vitabu ambavyo havina sifa hata ya kuitwa vitabu, je unatarajia nini kitokee? Lakini pia shule hazina vifaa muhimu hebu pata picha mwanao anasoma kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita hajui Spatula au Bunsen Burner ilivyo! Kisha anakwambia akifika chuo atafanya mambo ya Labaratory.

Walimu nao vipi? Hawana makazi wakati miaka ile walimu walikua wakiishi jirani na shule na huku wakipewa plots za kulima na kufanya mambo mengine, leo hii Mwalimu anatakiwa afanye kila kitu mwenyewe, kwa mfano huwa najiuliza kwanini huu utitiri wa shule usinge unganishwa na kujengwa shule za Boarding kubwa na zenye vifaa na walimu competent mara moja? Sijui.

Ninayo mengi ambayo naweza kuyaweka hapa ila tuna tatizo pia la kutokupenda kusoma vitu virefu virefu na hili pia hutufanya tusifanye vizuri kwenye INTERVIEW maana ukiona JD (Job Description) ndeefu hutaki kuisoma na kuilewa wewe unakimbilia tu ku-apply, usipochaguliwa unalalamika. Good day ntarejea baadae kama utapenda niendelee kueleza.
 
Mpwa rekebisha kidogo heading hakuna neno "unazani" bali kuna neon "unadhani" na hili huenda ndio sababu ya kwanza kukosa ajira kwenye mchakato maana tuna matatizo ya uandishi.

Elimu yetu kwa kiasi kikubwa sana imebadilishwa na kuwa elimu ya kukariri na kufaulu, kwa mfano, leo hii hakuna shue tena za michepuo ya Kilimo, Biashara, Ufundi na Mapishi, miaka ile shule kama Tanga technical ilitoa technicians wa ukweli, Magamba Boys (now Sebastian Kolowa Memorial University) ilikua shule ya Mchepuo wa kilimo na ufugaji na kweli Vijana walitoka hapo walikua Wakulima na Wafugaji kweli kweli, Kaka yangu aliwahi kuja nyumbani likizo na akajenga banda zuri sana la kuku, Korogwe Girls ilikua Kilimo, Mapishi na Ushonaji. Kwahio kila mwananfunzi alietoka hapo kabla ya kuendelea na chuo alikua tayari alikua na ABCs za nini cha ku-specialize. Leo hii hata Walimu hao hawapo tena.

Kuruhusu kila shule itumie vitabu vyake pia imekua bonge la mistake, watoto wetu na vijana wetu leo hii wanatumia vitabu ambavyo havina sifa hata ya kuitwa viabu, je unatarajia nini kitokee? Lakini pia shule hazina vifaa muhimu hebu pata picha mwanao anasoma kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita hajui Spatula au Bunsen Burner ilivyo! Kisha anakwambia akifika chuo atafanya mambo ya Labaratory.

Walimu nao vipi? Hawana makazi wakati miaka ile walimu walikua wakiishi jirani na shule na huku wakipewa plots za kulima na kufanya mambo mengine, leo hii Mwalimu anatakiwa afanye kila kitu mwenyewe, kwa mfano huwa najiuliza kwanini huu utitiri wa shule usingenunganishwa na kujengwa shule za Boarding kubwa na zenye vifaa na walimu competent mara moja? Sijui.

Ninayo mengi ambayo naweza kuyaweka hapa ila tuna tatizo pia la kutokupenda kusoma vitu virefu virefu na hili pia hutufanya tusifanye vizuri kwenye INTERVIEW maana ukiona JD (Job Description) ndeefu hutaki kuisoma na kuilewa wewe unakimbilia tu ku-apply, usipochaguliwa unalalamika. God day ntarejea baadae kama utapenda niendelee kueleza.
Thanx kaka mkubwa,nitarekebisha nazani kuwa nadhani,tatizo tumezoea viswahil vya mtaani na kufupisha maneno kwenye uandishi na haya ndiyo madhara yake.SHUKRANI
 
Thanx kaka mkubwa,nitarekebisha nazani kuwa nadhani,tatizo tumezoea viswahil vya mtaani na kufupisha maneno kwenye uandishi na haya ndiyo madhara yake.SHUKRANI
Umeshafaulu maana umekubali kurekebishwa! Hilo nalo ni tatizo wengi wetu hatutaki kukoselewa ili tujirekebishe! Kila unachosema au kuamini au kutenda au kuandika unataka kila mtu awe kama wewe! Ila Mpwa wewe umefanya vizuri kukubali. Ngoja na mimi nirekebishe baadhi ya maneno hayasomeki vyema.
 
Hatuko competent, Undugulization, kuchagua kazi, kukosa refa, kukosa pesa za kufanyia application......
 
vijana wengi tumeandaliwa kuwa "job seekers" na sio "job creators" ukiuliza kwa nini vijana hatujiajiri utaambia hatuna mtaji, lakini ukifanya utafiti kwa sample ya wajasiriamali wachache tu walioendelea walianza na mtaji tzs ngapi??, atakwambia ni pesa ndogo tu ambayo sisi pesa hiyo tunanunua smart phone za gharama na laptop
 
Tupe mawazo mbadala kaka watu waweze kujiajir na kutengeneza ajira pia.
 
Tupe mawazo mbadala kaka watu waweze kujiajir na kutengeneza ajira pia.
Wazo mbadala watu ni kua job creators sasa hivi vijana wengi kila mwaka wana graduates ila job opportunities ni zilezile so lazima unemployment, kutatua ilo ni kwa vijana kutengeneza ajira (kilimo,uvuvi,,ufugaji,handcraft,n.k) ajira zitakua ila sisi sote tukisubiri kuzunguka na bahasha bado shida itabaki kua palepale
 
Mpwa rekebisha kidogo heading hakuna neno "unazani" bali kuna neno "unadhani" na hili huenda ndio sababu ya kwanza kukosa ajira kwenye mchakato maana tuna matatizo ya uandishi.

Elimu yetu kwa kiasi kikubwa sana imebadilishwa na kuwa elimu ya kukariri na kufaulu, kwa mfano, leo hii hakuna shule tena za michepuo ya Kilimo, Biashara, Ufundi na Mapishi, miaka ile shule kama Tanga technical ilitoa technicians wa ukweli, Magamba Boys (now Sebastian Kolowa Memorial University) ilikua shule ya Mchepuo wa kilimo na ufugaji na kweli Vijana walitoka hapo walikua Wakulima na Wafugaji kweli kweli, Kaka yangu aliwahi kuja nyumbani likizo na akajenga banda zuri sana la kuku, Korogwe Girls ilikua Kilimo, Mapishi na Ushonaji. Kwahio kila mwananfunzi alietoka hapo kabla ya kuendelea na chuo alikua tayari alikua na ABCs za nini cha ku-specialize. Leo hii hata Walimu hao hawapo tena.

Point mkuu, Elimu yetu imebaki kusoma kwa kukariri ili uone banda kwenye cheti hatuendi shule kupata knowledge ya kutusaidia katika kuendesha maisha pasipo kuajiriwa.

Vilevile na familia/walezi/wazazi nao huchangia "SOMA UTAAJIRIWA, USIPOSOMA UTAKUA NA MAISHA MAGUMU" Moja ya kauli inayotufanya watu tuogope hata kujaribu fursa zingine tangu tukiwa wadogo kama biashara, kilimo, ufugaji nk.

Aidha, wengi wetu hatufikrii kutumia professional zetu kujiajiri.
 
Ha ha ha ha hapo kwenye "SOMA UTAAJIRIWA, USIPOSOMA UTAKUA NA MAISHA MAGUMU" umegusa sana.Hiyo imeua sana vipaji vya watu
 
Post yako ya mwanzo ulisema watu hatuko vompitent,pia ukaongeza watu hawana refa dats y nikakuuliza if upo compitent refa ana msaada gani?
Ina maana huijui kazi ya refa mkuu? Ndo maana nikakuuliza unadhani waliopo kitaa wote hawapo competent? Wengine wamekosa watu wa kuwapigia mapande mkuu, na sio kila aliyepo kazini ni competent wengine wanajulia humohumo baada ya kuwa na marefa
 
Point mkuu, Elimu yetu imebaki kusoma kwa kukariri ili uone banda kwenye cheti hatuendi shule kupata knowledge ya kutusaidia katika kuendesha maisha pasipo kuajiriwa.

Vilevile na familia/walezi/wazazi nao huchangia "SOMA UTAAJIRIWA, USIPOSOMA UTAKUA NA MAISHA MAGUMU" Moja ya kauli inayotufanya watu tuogope hata kujaribu fursa zingine tangu tukiwa wadogo kama biashara, kilimo, ufugaji nk.

Aidha, wengi wetu hatufikrii kutumia professional zetu kujiajiri.
nusura nilie hicho ulichokiandika,, nimeumia sana maana kuna mtu nimebishana nae na kila siku ni ugomvi, anaamini kwenye kusoma ndio kuna kila kitu. Ok niishie hapa kwa sasa, barikiwa sana
 
vijana wengi tumeandaliwa kuwa "job seekers" na sio "job creators" ukiuliza kwa nini vijana hatujiajiri utaambia hatuna mtaji, lakini ukifanya utafiti kwa sample ya wajasiriamali wachache tu walioendelea walianza na mtaji tzs ngapi??, atakwambia ni pesa ndogo tu ambayo sisi pesa hiyo tunanunua smart phone za gharama na laptop
Na wewe pia umeongea ukweli mchungu, sidhani kama kuna mtu atakuelewa ambaye hana mtazamo kama huo, jana nilikua naongea na mtu flani nikamwambia nataka kuacha kazi nisimamie miradi yangu, KHA! Utadhani nimetukana au nimetangaza kuuwa mtu. Yaani kanisihi hadi nikajskia vibaya kwanini nilimwambia, hahahah WOGA wako ndio umaskini wako....
 
nusura nilie hicho ulichokiandika,, nimeumia sana maana kuna mtu nimebishana nae na kila siku ni ugomvi, anaamini kwenye kusoma ndio kuna kila kitu. Ok niishie hapa kwa sasa, barikiwa sana
Amen mkuu kinachotakiwa ni kufanya kitu unachoona utafurahia na mafanikio ya mtu hupimwa na mtu mwenyewe sio watu wa nje.......kila la kheri kiongozi
 
Back
Top Bottom