Serikali corrupted kama tuliyonayo haina uwezo wa kuwachukulia hatuwa wahalifu, hata tume milioni kumi za uchunguzi wa skendo mbalimbali zikiundwa. Serikali ya CCM haina nia kusaidia Tanzania zaidi tu ya kuwa mfumo wa kulindana kati yao kati ya wakubwa. Ni skendo ngapi zilizotokea hapa Tanzania ambazo serikali zikaziundia tume za uchunguzi? Asilimia 99.99 za taarifa za tume hizo hazikuleta manufaa yoyote kwa taifa na hakuna maamuzi wala hatua zozote yoyote zilizochukuliwa kutokana na ripoti za uchunguzi wa tume zilizoundwa. Sasa tungetegemea nini juu ya hilo la Jairo na akina Luhanjo? Tena wahusika wenyewe ni swahiba wakuu wa JK? Unatarajia nini kingetokea? Mbona hatujajiuliza nini matokeo ya uchunguzi wa tume za Mv Bukoba, Richmond, milipuko yan mabomu ya Mbagala na Gongo la Mboto, na meli iliyoua watu kule Zanzibar na nyinginezo? Nini kilifanyika baada ya matokeo ya tume zile za uchunguzi? Kama si kulindana tu kwa viongozi wetu? Nani alijiuzulu? Nani alifikishwa mahakamani? Kumba basi ni nani mwenye uwezo ndani ya CCM na serikali yake ya kumnyoshea kidole mwingine? ,JK anaweza ? Je CCM inaweza? Siamini! Hawana uwezo wa kuwachukuliwa hatua wahalifu ambao wanakula nao sahani moja. Kwa kesi ya Jairo, Luhanjo, Mkaguzi mkuu wa Serikali na hata waziri wa Nishati na madini kwa jinsi ripoti ya hiyo bunge ilivyoeleza kila mtanzania alitegemea kuwa kungekuwa na tsunami ya watu kujiuzulu na kuchukuliwa hatua... lakini hadi leo kimya na JK mwenyewe hasemi chochote juu ya skendo za watu wake. Luhanjo bado yuko ikulu na anaendelea kucheka naye. Je Jk. ni kipofu namna gani asione yote yaliyosemwa kwenye ripoti za tume hizi? Mbona anazidi kuwakumbatia watu hawa..? Anangojea ushahidi gani zaidi? Anataka kutuambia nini watanzania? Tumechoka na hii Serikali corrupted ya CCM ambayo haina maamuzi yoyote. ndio maana tunapigania mabadiliko Tanzania. Akina Jairo, Luhanjo na wengineyo...peteni tu sasa chini ya muhimili huu wa serikali ya CCM. Lakini siku zinakuja, mabadilio yanakuja, na uhuru wa kweli wa Tanzania na wa watanzania unakuja, wote mtachukuliwa hatua kwa maovu yenu dhidi ya wananchi. Endeleeni kulindana tu! Watanzania tumechoka na hii serikali yetu inayolala usingizi wa pono.