junior mbani
Member
- Sep 16, 2014
- 52
- 59
Vipi kama tunavyo dhani sivyo mambo jinsi yalivyo?, mimi sina uhakika na lolote najaribu tu kufikiria.
- Tulipata uhuru bila kumwaga damu, kupitia Raisi wetu wa kwanza Mwalimu Nyerere,Je aliwashinda kwa hoja wazungu na kweli wakakubali kumpa nchi na uhuru!? Kwasababu alikua hana hata kitu cha kuwatishia, vip kama kuna makubaliano yalikuwepo ambayo hatuyajui? Maana mzungu kuachia lasilimali kizembe!
- Afrika nchi zetu zina migogoro mingi sana,ya kiuchumi na kiutawala pia. Watu mbali mbali wanatoa sababu zao ambazo wanadhani ndio chanzo cha matatizo yetu. Vipi kama chanzo ni watu fulani ambao wanajua Africa wakitulia vizuri nchi zao zikawa na siasa nzuri basi kuna vitu ambavyo ni faida kwao watavikosa kwaio njia sahihi ni nchi za Africa siziwe na utulivu?.
- Magonjwa yamekua mengi sana duniani, mengine yalikuwepo tangu enzi za zamani kwenye historia, na sayani imekua suluhisho kubwa la magonjwa mbali mbali kwa jinsi inavyozidi kuku. Vipi kama nyuma ya pazia kuna magonjwa yanayo tengenezwa ulimwenguni kwa manufaa ya watu fulani? Mfano UVIKO 19, huwenda ungonjwa huu ukawa ni manufaa kwa watu fulani.
- Nchi za Africa kwa sasa haziko chini ya wakoloni kwa maana vitabu vya historia vinasema ukoloni umepita Je ni kweli?, huu ukoloni mambo leo ni kitu cha kufikirika au kipo kweli?, Je kweli hatutawaliwiiii? Tunauwezo wa kufanya maamuzi makubwa wenyewe katika bara letu Afrika kama kuanzisha fedha ya pamoja yenye nguvu kama Euro? Bila kuingiliwa na mataifa ya njee?
- Mimi sijawahi kusoma nchi za njee wala sifahanu mitaala yao ikoje,lakini sisi kwenye historia tulisoma kuwa binaadamu wa kwanza alikua ni sokwe. Je na wao wanasoma historia hiyo hiyo? Na kama si hivyo walikua wana lengo gani hasa maaana tunatumia mitaaala waliotupa wao. Vip kama kuna mizizi fulani ambayo imewekwa kwa makusudi maaalum?.