Vipengele vya kumshitaki Trump kutangazwa

Vipengele vya kumshitaki Trump kutangazwa

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,362
Reaction score
4,818
Wabunge wa Democrat nchini Marekani wanatarajiwa hivi leo kutangaza vipengele viwili vya hatua za kumshitaki Rais Donald Trump, baada ya kukamilisha kujenga hoja yao juu ya kile wanachosema ni "hatari ya wazi na ya sasa" kwa usalama wa taifa.

Vipengele hivyo vitajielekeza kwenye matumizi mabaya ya nguvu na kulizuia bunge kufanya kazi zake, kwa mujibu wa gazeti la Washington Post lililowanukuu maafisa watatu wanaolifuatilia suala hilo.

Gazeti hilo limesema kuwa Baraza zima la Wawakilishi litapiga kura juu ya vipengele hivyo wiki ijayo, kabla ya kesi kuwasilishwa kwenye Baraza la Seneti. Hata hivyo, kituo cha televisheni cha CNN kimeripoti kwamba kipengele cha tatu bado kingali kinajadiliwa na kwamba bado hakujawa na makubaliano.

Spika wa Baraza la Wawakilishi, Nancy Pelosi, amesema kamati za sheria na ujasusi zitazungumza na waandishi wa habari leo kutangaza hatua zifuatiazo kwenye kesi hiyo ya kumuondoa Rais Trump madarakani.
 
Wa Democratic wanataka washinde Uchaguzi wa Mwakani kabla ya muda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom